RCFI. FM

RCFI. FM

Partager

La radio communautaire Fizi FM,

28/12/2021

DRC: Usalama/ Ituri/ Kivu Kaskazini.

WANAMGAMBO 7 WA ADF WAMALIZIWA MAÏSHA NA SILAHA NYINGI ZA KAMATWA NA VIKOSI VYA FARDC./ By Madiba Mahoye
"""""''""""""""""""""""""""""""""""""""""""

Vikosi vya jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimetangaza( FARDC ), vimetangaza siku ya jumatatu tare 27 Desemba 2021i kua vimetia nguvuni waasi 7 wa allied demokratic forces ADF katika kijiji cha bandibese kwenye umbali wa karibu kilometa 18 na eneo la Komanda, tarafa la Irumu, jimbo la Ituri.

Katika mazungumzo na vyombo vya habari luteni Jules NGONGO msemaji wa jeshi la Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo FARDC jimboni Ituri, amesema kua silaha mbili za aïna ya AK47 na mabomu ya kienyeji yamek**atwa na jeshi la serikali ya Congo toka mikono ya wanamgambo wa ADF.

Asisitiza kwa kusema kua silaha hizo zimek**atwa na vikosi vya usalama baada ya mapambano yalio dumu kwa muda wa masaa kadhaa dhidi ya wanamgambo wa ADF.

Photos from RCFI. FM's post 27/12/2021

FIZI: Usalama/ GUMINO YASHAMBULIA KITUO CHA FARDC HUKO KAMOMBO NA RAÏA WAKIMBIA MISITUNI/ By Madiba Mahoye.
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""

Mapigano makali yameripotiwa mapema asubuhi ya jumatatu tare 27 Desemba 2021, tarafani Fizi kijiji cha Kamombo, sekta ya Tanganyika groupementi Balala Kaskazini ( Balala Nord ).

Wapiganaji wanaodhaniwa kua ni wanamgambo wa Gumino na wash*tika wao wamekivamia mapema asubuhi vituo vya Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC ) vinavyopatikana katika vijiji vya Kamombo, Namara na Tchakira kwenye umbali usiozidi kilometa 17Kms mahariki na kijiji cha Mikenge. Duru nyingi zenyekuaminika zathibitisha kua vijiji hivyo vitatu vimetekwa na wanamgambo wa Gimino wanaongozwa na kanali muasi Michel Rukunda akijulikana kwa jinamaarufu MAKANIKA. Upande wa msemaji wa sekta ya operesheni Sokola ya pili kanda ya kusini mwa jimbo la Kivu Kusini Meja Dieudonné Kasereka kwa ush*tikiano na mkuu wa sekta ya Tanganyika John Mulondani wamethibitisha taarifa hizo lakini bilakutoa idadi ya vilivyo haribika.

Wanamgambo hao wa Gumino wameteleza mashambulio hayo dhidi ya vituo vya FARDC mapema alfajiri majiri saa kumi kwa kush*tukiza ambapo wanamgambo hao wamekilenga kituo cha wanajeshi wa bataliani ya 122 ya FARDC ikiongozwa na kanali YAUNDE ambao walikua wametia kambi sehemu hiyo hivi karibuni. Taarifa ambazo zimetufikia za eleza kua kiongozi wa bataliani hiyo kanali YAUNDE ameiyaga dunia kwenye mapambano hayo.

Kwa mujibu wa duru zetu kutoka Kamombo zasema kua raïa wamekimbilia msituni huku baadhi yao wakikimbilia Mikenge na Mikalati maeneo ya Itombwe katika tarafa la Mwenga wakiyatoroka makabiano.
>, ametaja hivo mkuu wa sekta ya Tanganyika bwana John Mlondani Mwimiwa.

Hadi mdahuu tunaandika taarifa hii, hali ya sintofahamu inaendelea kuripotiwa Minembwe - Centre, ambapo taarifa zaendelea kutujia zikisema kua wanamgambo wa Gumino wanaendelea kusonga mbele wakielekea kwenye makao makuu ya jeshi la FARDC brigade ya 12 inayo patikana Minembwe.

Kwa upande mwengine taarifa kutoka kwenye vyanzo vya kiusalama za eleza kua kikosi cha 121 cha bataliani ya makomando imekua mbiyoni kwa kujielekeza Mikenge eneo la Kamombo

15/11/2021

Kivu - Kusini/ Usalama - Fizi

WANAMGAMBO WA GUMINO WATEKELEZA MAUAJI MAPYA KIJIJINI MIKENGE SEKTA YA ITOMBWE./ By Madiba Mahoye.
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""

Wapiganaji wa muungano wa vikundi vya wanamgambo wa Gumino / Twigwaneho, Androïde na Ted Tabara waasi wa Burundi wametekeleza mauaji dhidi ya raïa usiku wa tariki 15 Novemba 2021majira ya saa tano, katika kijiji cha Mikenge kinachopatikana ndani ya sekta ya Itombwe Kitongoji cha Bashimukinji 1er) tarafa la Mwenga jimboni Kivu Kusini.

Watu watano ndio wameuawa na wengine tisa wamejeruhiwa, huku nyumba kadhaa zimechomwa moto. Duru za mahali zimearifu.

Shirika jipya la raïa wa Congo NSCC eneo la Kusini mwa jimbo la Kivu limelaani washambulizi hayo huku likilaumu jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo FARDC na vikosi vya jeshi la umoja wa taïfa MONUSCO kwa kutokutoa msaada na kuwahami raïa.

André Byadunia Mashaka mwenyekiti wa shirika hilo jipya la raïa wa Congo jimboni amesema kua wanamgambo hao wametekeleza mauaji hayo karibu na kunako patikana kituo cha vikosi vya usalama .> amesema hiyo.

Duru hizo zinaïyomba serikali ya jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo kurahisisha ili kuoatikane uwezekano wakuwafikisha raïa walio jeruhiwa kwenye hospitali kuu ya Bukavu ili wapate matibabu.

Hakuna taarifa ambayo imekwisha tolewa na maafisa wa kijeshi kutokana na uvamizi huo dhidi ya raïa wa kijiji cha Mikenge.

Eneo la nyanda za kati na juu zinazo inukia milima ya matarafa ya Mwenga, Fizi na Uvira yamekua uwanja wa vurugu ambazo zinayo ya gharimu maïsha ya raïa wasio na hatiya.

Photos from RCFI. FM's post 19/10/2020

DRC: BURUNDI YA FICHUA NJAMA YA RWANDA DHIDI RDCONGO / by Madiba Mahoye
-----------------------------------------------------------------------------
Waziri wa ulinzi wa Burundi na wapiganaji wa zamani injinia Alain Tribert MUTABAZI, ameïshutumu Rwanda kwa kuwasajili kijeshi vijana wa Burundi kwa malengo ya kuihujumu kijeshi nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Zowezi hilo limekua likiendeshwa na Rwanda tangu mapigano mapya ya zuke huko katika nyanda za juu za vilima vya Fizi - Minembwe, Uvira - Bijimbo na Mwenga, kwa malengo ya kuwasaïdia wanamgambo wa Gumino ikiwa ni watutsi wenye asili ya Rwanda k**a inavyo daïwa na raïa wa Congo.
Taarifa hizo pia zimezunguziwa kwenye kikao cha mawaziri wa ulinzi wa nchi za jumuia ya ukanda wa maziwa makuu, kikao kilicho fanyika tare 14 Oktoba mwaka huu kwa njia ya vidéoconférence, kikiendeshwa na waziri wa ulinzi wa Congo-Brazzaville akiwa ndie mwenyekiti wa baraza hilo.
Nchi za Zambia ,Uganda, Burundi, Tanzania, Rwanda , Angola , Afrika ya kati, Sudani Kusini zilikuwa wenyeji katika mkutano wa nchi hizo zikiwa zimewakilishwa na mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo.

Katika mkutano huo wa mawaziri wa ulinzi,swala na mbinu za kumaliza uvunjifu wa amani katika ukanda wa maziwa makuu limepewa kipau mbele na kutafuta mbinu m'badala ili amani idumu. Mawaziri hao wa ulinzi pia wametizamia kwa pamoja jinsi ya kuongezea uwezo kwa kikosi cha kiukanda,FIB, ambacho kinatarajiwa kushika nafasi ya jeshi la MONUSCO linalo hudumu nchini DRC likiwa linamaliza muhula wa kusimamia amani nchi humo ifikapo Desemba mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumzia katika kikao hicho waziri Aimé NGOI MUKENA, waziri wa ulinzi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amekumbusha mawaziri wenzake wa ulinzi wa nchi za ukanda huu kufanya iwezekanavyo kwa kuziba pengo katika nyazifa zinazo baki kwenye ofisi hiyo n**i zote zifanyike k**a inavyo tarajiwa, huku waziri huyo akikazia kuimarishwa kwa kitengo kinacho husika na amani na usalama. Waziri NGOI MUKENA amependekeza DRC kuchukua tena nafasi ya uwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwenye muhula mwengine.

Rwanda imekua ikishotwa kidole mara kadha kwa kuyafadhili makundi ya watutsi wa kinyamulengo wenye malengo ya kujipatia nchi huru kutoka sehemu ya ardhi ya DRC tangu wakati wa uasi wa RCD Goma,iliokua ikiongozwa na Azarias RUBERWA myaka ya 1998 ambae ni waziri wa serikali za vijiji nchini. Kundi ambalo linalo fadhiliwa na Rwanda, ni kundi kundi la Gumino linalo ongozwa na kanali Michel Rukunda alias Makanika akishirikiana na waasi wa Burundi wa Red Tabara ambao wanayumbisha usalama siku hizi nchi Burundi kwa ushirikiano na Wanyarwanda, k**a zinazo ripoti duru zetu.

Itafahamika kuwa polisi ya Burundi imenya msako siku za hivi karibuni katika mikoa ya Gitega na Makamba na kuwak**ata mamia ya wanyamulenge ambao wamebainika kua ni wahamiaji haramu ambao wanaeshi bila vitambulisho nchini Burundi.

Wakuu wa mamlaka nchini Burundi wamekuwa na hofu dhidi ya watu wenye kuongea lugha ya kinyarwanda kutokana na uhusiano mdogo wa kidiplomasa kati ya nchi hizo mbili ulio haribika tangu wakati hayati raïsi Pierre NKURUNZIZA wa Burundi ajitangaze k**a mgombea kiti cha uraïsi katika uchaguzi wa mwaka wa 2015.

Burundi na Rwanda zimekua majirani wenye uhasamu mukubwa.

Vous voulez que votre entreprise soit Entreprise De Médias la plus cotée à Baraka ?
Cliquez ici pour réclamer votre Listage Commercial.

Téléphone

Site Web

Adresse

La Radio Communautaire Fizi FM, Est Situé à L'est De La République Démocratique Du Congo Au Sud Est De La Province Du Sud Kivu, Sur Le Litoral Du Lac Tanganyika
Baraka