Malenga Waefeso

Malenga Waefeso

Share

Mwalimu na mwandishi wa mashairi

19/06/2024

Shairi: JE MNGETUPENDA?
mtunzi: Chozi la samaki

🤔🤔SWALI KWA WANAUME🤔🤔

1.
Tusingekuwa na mat**i,je bado mngetupenda
Tukakosa usofti,kifinya Kwa vyenu vyanda
Je ngesimama kit**i,Nasi bila kututenda?
Ewe mwana wa Adamu,nambie ungetupenda?

2.
Tungekosa makalio,nyuma tukapigwa Randa
Je mungeshika sikio,na bado mkatuganda?
Je ngeeka azimio,kuwa mbali 'singeenda
Ewe mwana wa Adamu, nambie ungetupenda?

3.
Tungekosa nzuri Sura,zikawa k**a za punda
Miili imeparara,tukajawa na vidonda
Bado mngetupa stara,kasimama kutulinda?
Ewe mwana wa Adamu, nambie ungetupenda?

4.
Hebu waza Kwa akili,k**a tungekosa tunda
Tukawa hatuna asali,kakosa pakutukanda
Nambieni Kwa ukweli,je milele ngetuganda?
Ewe mwana wa Adamu, nambie ungetupenda?

5.
Je mwatupendea nini,mkisema mwatupenda
Je upendo u moyoni,au tamaa metanda?
Au t**i kifuani,na Yale yetu matunda?
Ewe mwana wa Adamu, nambie ungetupenda?

vicky

Photos from Malenga Waefeso's post 25/04/2024

😭💔CHOZI HILI CHOZI LAKO💔😭
1.
Nimeshapata meseji,umesema 'its over'😭
Langu chozi k**a maji,likajaa 'all over'😢
Kitanda mejaa maji,sio tena 'sleep over'🤔
Chozi hili chozi lako,ipo siku utalia💔

2.
Umesha pata mwandani,mie kwako ni kiraka
Kuniona hutamani,wafanya unavyotaka
Ni kidonda cha rohoni,hakiwezi kutibika
Chozi hili chozi lako,ipo siku utalia💔

3.
Nimekumbuka zamani,mapenzi tukianzia🤔
Na meseji themanini,'missed call' nazo mia😂
Ungenifuata dukani,njiani tukikimbia😢
Chozi hili chozi lako,ipo siku utalia💔

4.
Chakula ukinilisha,huku upo kifuani💑
Na usiku tukikesha,kwa michezo ya chumbani
Kwangu tena hukubisha,sebuleni na jikoni✔
Chozi hili chozi lako,ipo siku utalia💔

5.
Natamani kukutaja,matusi kukuandikia😧
Naona hakuna haja, na umekwishaamua😡
Ulikuwa namba moja,wengine nawatimua😿
Chozi hili chozi lako,ipo siku utalia💔

6.
Kwaheri ya kuonana,nahisi kizunguzungu😖
Na sitaki kukuona,nisije kupiga rungu🤕
Ni wazi umenikana,hautaki mambo yangu😷
Chozi hili chozi lako,ipo siku utalia💔

7.
Beti saba ninatua,huku nashika tama🙉
Usiwai nipigia,wala jumbe ku*ituma📵
Kwa muda nitaumia,ukivuja wangu mtima💘
Chozi hili chozi lako,ipo siku utalia💔

💔💔💔💔💔💔💔💔💔
Vicky

01/04/2024

🤔🤔😂😂🙈🙈
Ninalo swali wenzangu,leo muniweke wazi
Ninayo sindano yangu,nataka kuweka u*i
Mwanichanganya wenzangu,sio leo jana ju*i
NI WAPI NAPAKA MATE,NI U*I AMA NI TUNDU??

Photos from Malenga Waefeso's post 02/02/2024

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Denis Denox, Daniel Kibet, Charity Barasa, July Obondo

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Kitale?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address

Mitume
Kitale