Goodlyfetz Sports
Page hii ni kwa habari | Michezo | Matokeo | Misimamo | Ligi zote
18/02/2026
ππππππππ: UEFA imejiandaa kuwasilisha kesi ya ubaguzi wa rangi ya Vinicius-Prestianni π
"Kesi itafunguliwa na wachezaji kuripoti mambo yote waliyosikia na kuona uwanjani", anasema El Larguero.
"Itakuwa vigumu kuwa na uamuzi iwapo matusi ya ubaguzi wa rangi na unyanyasaji wa moja kwa moja hayataonyeshwa" βοΈ
18/02/2026
Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) imeidhinisha rasmi marekebisho ya Katiba ya klabu ya Simba baada ya kukamilika kwa mchakato wa kisheria uliokuwa chini ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Michezo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Februari 18, 2026, Msajili wa Vyama vya Michezo nchini, Abel Ngilangwa, amesema marekebisho hayo yamefanyika kwa kuzingatia Sheria na Kanuni zote zinazosimamia vyama vya michezo nchini.
Haya yanajiri siku mbili tu baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda mnamo Februari 16, 2026 kumuagiza Msajili wa Vyama vya Michezo kuhakikisha kuwa mchakato wa marekebisho ya Katiba ya Simba unapatiwa majibu kabla ya mwezi kumalizika.
"Napenda kuufahamisha umma kuwa mchakato wa uchambuzi, tathmini na uidhinishaji wa marekebisho ya Katiba ya Klabu ya Simba umekamilika kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa Sura ya 49 na kanuni zake," - amesema Ngilungwa
Ngilangwa ameongeza kuwa Katiba hiyo iliyorekebishwa iliwasilishwa kwa mujibu wa Kanuni ya 11 ya Kanuni za Msajili wa Vyama vya Michezo T.S Na. 441 ya mwaka 1999 kwa ajili ya kupitiwa na kuidhinishwa.
Aidha ameeleza kuwa Msajili alitekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Kanuni ya 11(3)(a) ya Kanuni za Msajili wa Vyama vya Michezo T.S Na. 441 ya mwaka 1999, inayomtaka kuhakikisha marekebisho yoyote ya katiba hayaathiri usalama, hayavurugi amani miongoni mwa wanachama au jamii kwa ujumla, wala kuathiri maendeleo ya chama.
14/02/2026
π¨ ππππππππ: Kylian MbappΓ© ameachwa benchi kwa Real Madrid usiku wa leo! β οΈπͺ
Hatacheza dhidi ya Real Sociedad!
14/02/2026
π¨ RASMI: Trent ANAANZA Klabu ya Real Madrid!
Amerudi kwenye kikosi cha kwanza cha X
Winga wa zamani wa Liverpool, Man City, Chelsea na Arsenal, Raheem Sterling ametangazwa k**a mchezaji mpya wa klabu ya Feyenoord ya nchini Uholanzi kwa mkataba mpaka mwisho wa msimu.
Sterling 31, raia wa England anajiunga na timu hiyo inayonolewa na Robin van Persie k**a mchezaji huru baada ya kuachana na Chelsea mnamo Januari 28 akishindwa kupata nafasi ya kucheza huko Darajani.
Sterling anaondoka kwenye Ligi kuu England baada ya miaka 14 tangu acheze mechi yake ya kwanza kwenye Ligi hiyo mnamo 2012 ambapo amefunga magoli 123 kwenye mechi 396 kwenye Ligi hiyo.
14/02/2026
Mradi huu ni mradi wa Yanga SC na GSM sio mali ya mtu bali ni mali ya taasisi hizi mbili. Mradi huu utaendelea kujengwa iwe mimi ni Rais wa Yanga ama lah. GSM na Yanga wanaowajibu wa kuhakikisha kuwa mradi huu unakamilika chini ya Kiongozi yoyote ambaye atakuwa Rais wa Yanga. Nimejenga msingi bora na imara ambao utafanikisha jambo hili bila kumtegemea mtu. Ikitokea mimi sio Rais wa Yanga, atakayechukua wadhfa huu anapaswa kujua analo jukumu la kuhakikisha ndoto ya Wananchi inatimiaβ Hersi Ally Said
14/02/2026
: Nyota wa Manchester United Matheus Cunha amefunguka kuhusu shabiki maarufu wa Man United aliyeshindwa kunyoa nywele zake kutokana na United kutoshinda michezo mitano mfululizo akidai anachojali ni alama 15 tu na siyo nywele zake.
"Watu wana wasiwasi zaidi kuhusu kupata ushindi mara tano kwa sababu ya kukata nywele kuliko kuhusu pointi 15. Kwa hivyo, mimi hupendelea zaidi pointi 15, sijali kuhusu kukata nywele kwake hata kidogoβ β Cunha.
Unakubaliana na Mtazamo wa Cunha?
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Arusha