Isack Jonas Jr.
Fashion Designer •||• Gospel Singer •||• Songs Writer •||• Models Trainer •||• Born
04/06/2022
HESHIMA HUGHARAMIKIWA ila haupatikani kwa Fedha.
Nimejifunza kuwa, ukitaka kuheshimiwa kubali kuishi ndani ya kanuni kuu tatu.
1. Kwa wadogo zako Mara zote tafuta kuwa mfano mzuri, hakikisha hautengenezi mazingira ya walioko chini yako kiumri kujifunza au kukunukuu kwa mambo yasiyofaa. Penda kuwa taswira njema unayotaka kuiona kwao.
2. Kwa watu wa rika lako onesha utofauti. Mara zote usipendwe kubebwa na mambo, jenga misimamo yako itakayokutofautisha nao, wanapokuona wawe na jambo la kujifunza. Kuwa mtu anaetengeneza trend sio anaefuata trend zilizopo.
3. Kwa waliokuzidi umri kuwa msikivu. Kuna tofauti sana kati ya mtu mwenye ujuzi na mwenye uzoefu. Mwenye ujuzi atakuelezea kitu kilivyo ila mwenye uzoefu atakuelezea kunavyofanya kazi. Wazee hata k**a hawajui mengi ila wana uzoefu mwingi na huo uzoefu ni hazina yenye faida kubwa sana ukiweza kuipata na kuitumia. Jua sana ila usijue kupita wenye uzoefu.
Heshima HUGHARAMIKIWA.
27/05/2022
KUWA NA STRESS KWENYE HAYA MAISHA NI LAZIMA
Unaweza kustress saivi ukashindwa kuanza unachotaka kufanya hizi ni stress mbaya ila ukianza saivi baadae utakuwa na stress ya jinsi ya kuendeleza ulichoanza hizo ni stress nzuri.
SASA Chagua unataka stress zipi.
26/05/2022
Kuna msemo wa Ijue Thamani yako ila kwangu nadhani kujua kusudi la kuwepo kwako duniani INA faida kubwa kwani thamani yako huletwa na wewe kuliishi kusudi lako duniani.
Tafuta kujua wito wako.
Click here to claim your Sponsored Listing.