CASFETA ARUSHA

CASFETA ARUSHA

Share

Karibu CASFETA Mkoa wa Arusha. Hapa utapata taarifa na mafundisho mbalimbali ya Neno la Mungu. Usipotee bure, njoo tushauriane, tujengane na kutiana moyo.

10/12/2020

CASFETA MKOA WA ARUSHA INAPENDA KUWAALIKA WOTE KWENYE MKESHA WA KUWAKARIBISHA MWAKA WA KWANZA WA VYUO VYOTE MKOA WA ARUSHA. UTAKUWA NI USIKU WA NGUVU USIPANGE KUKOSA.

11/08/2020

Wapendwa wana CASFETA na viongozi wa CASFETA ngazi mbalimbali Nawasalimu kwa salamu ya upendo katika jina la Yesu Kristo
Poleni kwa taharuki na sintofahamu iliyojitokeza kutokana na habari yenye nia ovu iliyoandikwa na gazeti lijulikanalo kwa jina la MWANZO kwa muda wa wiki tatu mfululizo.
Gazeti hili ni la mtu binafsi na ndiye muhariri mkuu anayejulikana kwa jina la Jackson Malungu, ni mtu aliye kinyume na huduma ya CASFETA kwa miaka mingi na amekua akiandika habari za kupotosha na kuweka maoni ya watu waliokinyume na CASFETA na kanisa linaloidhamini huduma hii yaani Tanzanian Assemblies of God.
Huduma ya CASFETA inatambuliwa kisheria na inafanya kazi kwa mujibu wa taratibu za kiserikali na maelekezo kutoka wizara ya Elimu. CASFETA na viongozi wake wanafanya kazi kwa misingi ya amani yenye nia ya kuujenga mwili wa Kristo.
Habari hizo ni za kupuuzwa na hazina ukweli, kwa sababu kwa mujibu wa gazeti hilo maelezo yaliyotolewa ni maoni ya mtu binafsi tena ni maoni ya upande mmoja uliokinyume na CASFETA.

Hivyo inaonyesha dhahiri nia ya chuki na maslahi binafsi ya muhariri na mmiliki wa gazeti hilo.
Pia ameamua kuirudia habari hiyo kwa wiki tatu mfululizo kwa sababu ya maslahi ya kifedha, kwa sababu habari hiyo alipoitoa wiki ya kwanza nakala nyingi zilinunuliwa kwa sababu habari ni hasi!, watu wengi walitaka kujua ni nini kiliandikwa ndani.
Hivyo uongozi unawaomba wadau wote wa CASFETA, kuendelea kumtumikia Mungu kupitia huduma ya CASFETA kwa amani na utulivu huku mkizidi sana kuifanya kazi ya Mungu bila kuyumbishwa na HILA za waovu wakati jambo hili likiendelea kufatiliwa kwa ukaribu kulingana na taratibu zilizopo.

"Basi, ndugu zangu wapendwa mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana Siku zote, kwa kua mwajua ya kwamba taabu yenu sio bure katika Bwana"
1korinth 15:58

Mungu awabariki sana!!
Uongozi

Photos from CASFETA ARUSHA's post 09/08/2020

CASFETA MKOA WA ARUSHA, Tunazo kila sababu ya kumshukuru MUNGU KUTUSAIDIA KUFUNGUA TAWI LA CASFETA CHUO CHA T. M.A MONDULI, WONDERFUL KUWA NA MAASKARI WETU.

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Address

PO BOX 1330
Arusha