Yuzzo Jr

Yuzzo Jr

Share

Asante kwa kutembelea ukurasa wetu wa habari za michezo za uhakika na makala kuhusu soka saa 24. sports

Photos from Yuzzo Jr's post 22/07/2026

Rais wa Simba SC, Mohammed Dewji amekutana na kufanya mazungumzo na wachezaji wapya watatu ambao tayari wametambulishwa Kelvin Nashon, Nathaniel Chilambo na Bakari Msimu.

Mo Dewji amewakaribisha wachezaji hao kwenye familia ya Simba na kuwaeleza malengo ya Simba ya ndani na kimataifa na hivyo kuwataka kujituma wakati wote wanapokuwa kwenye majukumu ya kuipambania nembo ya klabu.

Mwenyekiti wa Bodi, Crescentius Magori alikuwepo pia katika kikao hicho.

Photos from Yuzzo Jr's post 22/07/2026

Rais wa Yanga SC, Hersi Said amelikaribisha rasmi jopo linalounda benchi jipya la ufundi la timu hiyo likiongozwa na Kocha Mkuu Mangoba Mngqithi.

22/07/2026

MAKONDA: MKOA USIOLETA TIMU TAIFA CUP, UONGOZI WAKE UMEFIKA MWISHO

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, amesema viongozi wa mpira wa kikapu katika mikoa ambayo haitashiriki mashindano ya Taifa Cup wanapaswa kuondoka madarakani kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kuendeleza mchezo huo.

Makonda amesema Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kuendesha ligi za basketball katika mikoa, hivyo hakuna sababu ya baadhi ya mikoa kushindwa kuandaa timu zitakazoshiriki mashindano ya Taifa Cup.

“Kama kuna mkoa ambao hautashiriki Taifa Cup na una uongozi wa basketball, mjihesabu uongozi wenu umefika mwisho,” amesema Makonda.

Aidha, amewataka viongozi wa michezo katika ngazi za mikoa na wilaya kuhakikisha wanasimamia mashindano na programu za kukuza vipaji mwaka mzima, akisisitiza kuwa nafasi za uongozi zinapaswa kutumiwa kuendeleza vipaji vya vijana badala ya maslahi binafsi.

Photos from Yuzzo Jr's post 22/07/2026

Rais wa Simba SC, Mohammed Dewji na Mwenyekiti wa Klabu na Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Murtaza Mangungu wamekutana na kufanya mazungumzo kuhusu mipango ya timu kuelekea msimu wa 2026/27.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Bukoba?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address

Kibeta
Bukoba
P.O.BOX1652BUKOBA