Rubondofm
District radio station
provide News content, sports, music and current affairs.
Chama Kikuu Cha Ushirika Geita (GCU LTD) kimefika katika viunga vya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza Kwa ajili ya kununua zao la Mpunga kwa wakulima
Hatua hii ni sehemu ya jitihada za kuhakikisha malighafi ya kutosha yanapatikana ili kiwanda Cha kuchakata mpunga Cha GCU LTD kilichopo Kasamwa Manispaa ya Geita kinafanya kazi muda wote n kuongeza pato la wakulima na vyama vya Msingi vya Ushirika AMCOS.
Afisa shughuli wa chama Kikuu Cha Ushirika Geita (GCU LTD) Charles Nyasi, akiwa na timu yake katika Kijiji Cha Kalangalala Wilayani Sengerema ameeleza kuwa amefanya ziara ya kutembelea Katibu wa AMCOS wa eneo hilo ili kuona utendaji kazi wake baada ya kuaminiwa na chama ili akusanye mpunga kutoka kwa wakulima.
Bwana Nyasi amesema ameridhishwa na utendaji kazi wa Katibu huyo kwani alipewa shilingi milioni mbili kununua mpunga magunia 20 na mpaka kufikia Sasa tayari amekusanya mpunga magunia 19.
Kwa upande wake Katibu wa AMCOS Kalangalala Wilayani Sengerema bwana Alphonse Mapinduzi John ameipongeza chama kikuu Cha Ushirika Geita GCU LTD kwa kumuamini kufanya kazi hiyo na kuahidi kuwa ataendelea kutekeleza wajibu wake kwa weledi Mkubwa ili kufikia lengo lililokusudiwa.
05/06/2026
HALMASHAURI ya wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita imeweka mpango maalum wa kushirikisha wadau wa maendeleo ili kumaliza uhaba wa madawati kwa shule za sekondari.
Mpango huo umeazimia kufikia mahitaji la madawati 3,000 kwa mwaka wa masomo 2026 katika shule za sekondari za serikali 20 ambazo zimepokea wanafunzi wa kidato cha kwanza 3,056.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Husna Toni amesema hayo katika taarifa yake kwa mkuu wa mkoa alipokagua na kupokea madawati 1,200 yaliyopatikana hadi kufikia Mei 2026.
Husna amesema madawati hayo ni mafanikio ya awamu ya kwanza ya mpango huo unaolenga kupata madawati 1,500 ambapo juhudi zinaendelea ili kufikia nusu ya mahitaji yaliyopo.
Amesema upungufu wa madawati umetokana mwitikio mkubwa wa wazazi kupeleka watoto shule baada ya sera ya elimu bila bure inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita.
“Ninaamini utoaji wa madawati haya utaboresha utoaji wa huduma ya elimu kwa wanafunzi wetu, na hatimaye kuongeza ufaulu shuleni”, amesema Husna.
Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale, Grace Kingalame amesema wadau wakubwa walioshirikishwa kuunga mkono mpango huu ni wawekezaji katika sekta ya madini na wameonyesha mwitikio.
Amesema mpango huo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto na kuendana na kasi ya ujenzi wa madarasa inayotekelezwa na serikali.
Mkuu wa mkoa wa Geita, Martine Shigela amepongeza mpango huo huku akizitaka halmashauri zingine kuiga mfano wa Nyang’wale kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta ya elimu.
“Huu ni ujumbe kwa wengine hususani kwa viongozi na watendaji kuhakikisha kwamba wanaiga mfano wa Nyang’hwale katika kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapata madawati.
“Shule ambazo zitapokea Samani hizi, ni vyema wakapokea na kuthamini mchango huu, na kubwa zaidi kutunza na kuhakikisha pale panapotokea uharibifu, marekebisho yafanyike”, ameelekeza.
Habari Na .yohana.jr
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Website
Address
Geita
30101