Benjamin the seer
BOWL OF DIVINE HEALING,REVIVAL AND RESTORATION MINISTRY
25/12/2025
Katika ulimwengu wa roho,amekwisha kuwa MKIMBIZI anayekimbia hata pasipo kufuatiwa na mtu.Nalimuona akijificha na kuviziavizia akiwa katika mavazi ya kawaida sana.
Amekwisha kuwa RAIA wa daraja la kawaida asiye kuwa na ulinzi wowote.
Danieli 2:47
Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, awezaye kufumbua siri, kwa kuwa wewe uliweza kuifumbua siri hii.
The king answered unto Daniel, and said, Of a truth it is, that your God is a God of gods, and a Lord of kings, and a REVEALER OF SECRETS, seeing thou couldest reveal this secret.
Patience is the key
Subra ni ya muhimu
Kutoka 14:14
BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
The LORD shall fight for you, and ye shall hold your peace.
UJUMBE TOKA KWA MUNGU
Baada ya kushuhudia yote yaliyotokea katika taifa letu siku chache zilizopita.
Nikiwa k**a MWONAJI(SEER),niliamua kuutafuta uso wa Mungu nakuomba kwa ajili ya taifa letu na kwa damu zilizomwagika.
Ndipo Mungu akanijibu kwa ndoto ifuatayo.
Naliona maji(mafuriko) yameizingira NYUMBA Moja ambayo mlango wake ulikuwa wazi na usingeweza kufungwa kutokana na Yale maji.Nje ya ile NYUMBA kulikuwa na gari ambalo nalo lilikuwa limezingirwa na maji pia.
Nikaona Kwa mbali MAMA mmoja ambaye alikuwa k**a mzungu kwa mwonekano akaniomba nimsaidie kulitoa lile gari kwenye yale maji na lilikuwa ni gari la kubonyeza button(vitufe fulani).LAKINI kitu cha ajabu ni kwamba yule MAMA licha ya kumsaidia akasema nikiligongesha gari lake itabidi tuchangie gharama ya kulitengeneza mimi na yeye.Nikamshangaa sana ana moyo wa namna gani huyu!
Wakati natafakari kuhusu hayo maji ikiwa ni mafuriko au laa!Roho mtakatifu akanipa tafsiri kupitia Ufunuo 17:15 ya kwamba Yale MAJI ni WATU wa jamaa,makutano na lugha anapoketi yule MAMA.
Nilimfikishia yule MAMA gari lake akaondoka nalo.
Mwenye kuelewa NENO hili alilonifunulia BWANA na aelewe.
LIPO TUMAINI,JIPENI MOYO ENYI TAIFA LA MUNGU.
UJUMBE
Bwana kanikumbusha Tena usiku wa leo habari za Nebukadneza,mfalme wa Babel na namna alivyochukuliwa kwenda uhamishoni mbali na makao ya wanadamu akaishi na wanyama wa mwituni.
Akapoteza kiti chake Cha ufalme ingawa Mungu alimrudisha Tena.Kilichompoza Nebukadneza ilikuwa ni KIBURI.
Mara ya mwisho Bwana kunisemesha habari za Nebukadneza ilikuwa ni mwaka 2020 February na nilipost kwenye ukurasa wangu na siku chache zilizofuata Mungu akamwadhibu Nebkadneza.
Mwenye akili na afahamu jambo hili alilosema Bwana Mungu wa majeshi.
CODED.
Hiki alichonionesha Bwana ni majibu ya maombi niliyoyafanya kwa siku kadhaa nikiwa sili chakula mchana na usiku kwa siku kadhaa.
Amosi 3:7
Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.
Surely the Lord GOD will do nothing, but he revealeth his secret unto his servants the prophets.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Kibwabwa
Iringa