Story funzo

Story funzo

Share

Karibu katika ukurasa wa simulizi, riwaya na jumbe za maisha kutoka kwa mtunzi Daniford ben

24/12/2025

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Mos Quito, Felistus Kim, Mligo John Vanny, Violeth Ndoss, Thobias Wilison, Gideon Wabuge, Franco Bernard, Nassor Salim, Agnes Philimoni, Milaji Omari, Theophil Theofrey, New Mick Msuya, Abdhallah Kassim, Mzungu Jrii, Masuha Mataba, Republica De Mocambique, Ammir Ke, Bismark Naut, Rubare Kwetu RB, Hilarious Hillas, Joshua Mrema, Mandevu Jonas, Joseph Kiangi, Zacharia Stephano, Master Plane

29/09/2025

TABIA 10 ZA SINGLE MOTHER ASIYE NA SHUKRANI
Katika jamii za sasa, kuna wanawake wengi wanaishi k**a single mothers (wazazi wa k**e wanaolea watoto peke yao). Wapo ambao ni wenye hekima, heshima na moyo wa shukrani, lakini pia wapo wengine wanaoonyesha tabia za kutokujali na kukosa shukrani. Tabia hizi hujitokeza waziwazi, na huwaathiri wanaume wanaohusiana nao kwa namna tofauti.

Wanaume wa kiume wenye misimamo imara (masculine men) mara nyingi huwakwepa wanawake hawa, lakini wanaume tegemezi kihisia (emotionally dependent men) hujikuta wakiwapenda sana hata k**a wanateseka.

Hapa chini kuna ishara 10 za tabia za single mother asiye na shukrani, kisha tutajibu kwa nini wanaume wa kiume wanawakwepa, na kwa nini wanaume tegemezi kihisia huwapenda sana.

1. Kutojali Msaada Anapopewa

Single mother asiye na shukrani hupewa msaada wa kifedha, kimawazo au kimwili, lakini badala ya kushukuru, huona ni wajibu wa kila mtu kumsaidia.
Hii inamfanya mwanaume wa kiume ajisikie anadharauliwa na humkwepa. Lakini mwanaume tegemezi kihisia huamini atathaminiwa baadaye, hivyo ataendelea kumpa msaada bila kikomo.

2. Kuchukulia Wanaume K**a ATM

Wanawake wa aina hii huona mwanaume si mtu bali ni chanzo cha pesa. Hawana mapenzi ya kweli, bali hufikiria zaidi faida.
Mwanaume wa kiume atakimbia kwa sababu hataki kutumiwa. Lakini mwanaume tegemezi huamini akitoa pesa nyingi zaidi, ndipo ataaminiwa na kupendwa.

3. Kutoonyesha Shukrani Ndogo Ndogo

Hata mambo madogo k**a zawadi ndogo au msaada wa ushauri hawajali. Hakuna thank you, hakuna tabasamu, hakuna kuthamini.
Kwa mwanaume aliye na heshima ya kiume, hii ni ishara ya hatari. Lakini mwanaume tegemezi husema moyoni, “labda hajafurahishwa vya kutosha, ngoja nijitahidi zaidi.”

4. Kuwashutumu Wanaume Wote
Mara nyingi single mother asiye na shukrani huwa na historia ya kulalamika kuhusu wanaume wote: “wanaume hawana maana, wote ni wabaya, hakuna wa kuaminika.”
Mwanaume wa kiume atajua huu ni mtego na ataepuka. Mwanaume tegemezi huona ni nafasi ya kuthibitisha yeye ni tofauti na wengine.

5. Kujiona Mwathirika wa Maisha

Badala ya kuchukua jukumu la maisha yake, hujiona mwathirika kila mara – akilaumu ex wake, serikali, au mazingira.
Mwanaume mwenye nguvu ataona hana nafasi ya kusaidia mtu anayeishi kwenye lawama. Lakini mwanaume tegemezi hupenda nafasi ya kuokoa mtu, na hapo ndipo huingia kwenye mtego wa kihisia.

6. Kutumia Watoto K**a Silaha
Single mother asiye na shukrani mara nyingi hutumia watoto wake k**a chombo cha kulazimisha mwanaume kumpa msaada au kubaki kwenye uhusiano.
Wanaume wa kiume huchukia kutumia watoto k**a chombo cha maumivu. Lakini mwanaume tegemezi huona ni jukumu lake kufidia pengo na anajitolea kupita kiasi.

7. Kutokuwa Mwaminifu Katika Mapenzi
Kuna single mother asiye na shukrani ambaye hucheza michezo ya kimapenzi, huficha mambo, na mara nyingi hana uaminifu.
Mwanaume wa kiume hatakubali kudharauliwa kwa heshima yake, lakini mwanaume tegemezi hupuuza ishara zote, akijifariji kuwa mapenzi ya kweli ni uvumilivu.

8. Kiburi na Kudharau
Hutumia maneno ya dharau, hujiona juu ya kila mtu na hawezi kushuka kusamehe au kushukuru.
Mwanaume wa kiume huona kiburi ni sumu ya mapenzi, lakini mwanaume tegemezi huamini uvumilivu wake utabadilisha tabia hiyo.

9. Kukimbilia Haki Badala ya Wajibu
Wanadai haki zao kila mara (“nina haki ya kuheshimiwa, kusaidiwa, kufadhiliwa”), lakini hawatoi wajibu wala kushukuru.
Hii humkimbiza mwanaume wa kiume, lakini humvutia mwanaume tegemezi ambaye anaamini kutoa bila kikomo kutaleta upendo.

10. Kuwatumia Wanaume Wema K**a Daraja
Single mother asiye na shukrani hutumia wanaume wema kupiga hatua kimaisha, lakini akifanikiwa hutupa uhusiano huo k**a kiatu cha zamani.
Wanaume wa kiume wanagundua mapema na huondoka, lakini mwanaume tegemezi huendelea kuvumilia kwa matumaini ya kuthaminiwa baadaye.

Kwa nini wanaume wa kiume wanawakwepa?

Kwa sababu wanaume wa kiume wanajua thamani yao. Wanajua mapenzi ya kweli lazima yawe na heshima, shukrani na uwajibikaji. Wanapomuona single mother asiye na shukrani, wanajua ni hasara ya muda na nguvu.

Kwa nini wanaume tegemezi kihisia huwapenda sana?

Kwa sababu wanaume hawa mara nyingi hubeba White Knight Syndrome – hamu ya kuwaokoza wanawake waliojeruhiwa. Huamini wakijitolea vya kutosha, hatimaye watapendwa. Upweke wao wa ndani huwafanya kuvumilia maumivu makubwa kwa matumaini ya kupata uthibitisho wa upendo.

👉 Hii ni somo kubwa kwa wanaume wote: mapenzi ya kweli hujengwa kwa shukrani, heshima na uwajibikaji. Wanaume wenye nguvu wanajua hii, na wanaume tegemezi wanapaswa kujifunza kujithamini kwanza kabla ya kujitolea kupita kiasi kwa watu wasiothamini.

05/09/2025

Story picha: NGUVU YA PENZI(03)
MTUNZI:DANifordy ben
MAWASILIANO: +255711444410

Tuliishia marko anamuona mpenziwe baada ya kumsubiri kwa muda mrefu sana, lakini anatambua kuwa yuko tofauti na siku zote....

Sasa tuendelee

Wakati zuhura akitoka nyumbani alimuacha mamaye akijianda kuondoka kwa kuhakikisha mjukuze wote wanakula vyema ili asimpe mzigo mwanaye wa maandalizi ya chakula, kwakuwa aliufahamu utundu wao. Na baad ya kuondoka ndipo zuhura alipopata nafasi ya kutoka kwenda kwa marko.

Kadri zuhura alipokuwa akisogea ndipo marko alikuwa akiona alama za uvimbe mwilini mwa mpenziwe, jambo lililomshangaza mno ijapokuwa hakuthubutu hata kutamka neno mpaka zuhura alipomkaribia kabisa.

"Vip kipenzi changu mbona hivyo leo harafu..."

"Usiniite hilo jina tena marko umenisababishia nimepigwa mwenzio mpaka nimeumia hivi, tafadhari mimi na wewe mwisho sasa na naomba tuachane kuanzia leo".

"zuhura".

"Aah staki bwana, niache".

"Nisikilize basi nitakacho kukwambia ijapo kwa dakika moja tu zuhura, ina maana umesahau ahadi zako zote? Hivi unadhani nitaishije bila wewe na huku tulipanga kuwa pamoja daima. Unatambua kuwa sina tofauti kabisa na majivu ya karatasi mbele ya upepo muda wote nitaishia kupepea nikipurizwa, kwanini uniache naangamia kwa kiu ilihali uko na maji? Pole kipenzi changu kwani si kusudio langu kukufanya uumie ni maisha tu! Amini kuwa hakuna mafanikio bila mapito ya kukupa ujasiri na hili ni jambo dogo tu twaweza zungumza hapaswi kugombana".

Marko alitumia ulimi wake vyema kuhakisha nduru za filimbi zinamtoa nyoka ndani ya pango, kutokata kwake tamaa kulifanya faraja upya ndani mwa zuhura ambaye ni dhahiri kipigo kile kilifanya maamuzi magumu pasi fikra. Wakati huo zuhura alikuwa amesimama wima, kando ya marko aliyekuwa bado amekaa katika jiwe kubwa akimtazama marko kwa jasho lililojaa husda. Kislani alichokuwa nacho kilizidi hata kile cha uke wenza mbele ya mme kipenzi cha wote. Nguvu kubwa aliyoitumia marko katika ushawishi mbele ya binti yule mchomovu katika mahusiano hatimaye ilifanikiwa kumlaghai zuhura mwenye mapenzi ya dhati kwa marko, naye akaingia kingi na kurudi katika mstari ambapo baada ya mazungumzo ya muda yenye kufarijiana wawili wale waliirejesha furaha yao upya k**a zamani na kusahau maumivu, kisha marko siku hii aliamua kumsindikiza nyumbani zuhura. Na kwakuwa siku hii zuhura alimjuza marko kuwa mama na baba yake hawapo nyumbani basi, baada ya kufika walikaa nyumbani hapo wakipiga story za hapa na pale mpaka usiku ukawakuta hapo, mwisho stori hizo zilifanya tamaa ya kimwili kumuingia marko ambaye alianza kutamani kula tunda la mpenziwe zuhura.

"Zuhura tafadhari mpenzi wangu, si umesema mama na baba yako hawapo? Basi naomba leo ijapo nidodose dodo kidogo mwenzi nishapata mshawasha".

Alizungumza marko kwa sauti ya huba iliyokwaruza kiasi kufanya isik**e vyema masikioni mwa mpenziwe ambaye alikuwa ametulia tuli kumsikiliza.
ITAENDELEA

Je atafanikiwa mpango wake marko? Usikose sehemu ijayo

23/08/2025

Story picha: NGUVU YA PENZI (01)
Mtunzi: DANIFORDY BEN
Mawasiliano:+ 255711444410

Zuhura alikuwa ni binti pekee kwa mamaye pamoja na babaye, zuhura alikuwa binti mrembo mno kwa muonekano hata tabia yake pia. Ukweli ni kuwa alichechefya mioyo ya wengi mno mtaani kwao, shuleni hata mjini alikokuwa akielekea kuuza mboga za majani alizokuwa akizilima baada ya kutofanikiwa kuchaguliwa kuendelea na kidato chakwanza, hakuwa mtu wa majigambo juu ya umbo na sura yake alivyokuwa amejaliwa kwani alikuwa msikivu kwa kila aliyekuwa akizungumza naye bila kujari, rika, kabira wala jinsia.

Zuhura alikuwa ni muaminifu mno mbele ya kipenzi chake marko ambaye alikuwa akisoma kidato cha nne shuleni itebe, mkoani sawe nchini nyumba nitu. Ndoto za wawili hawa ilikuwa ni kuhakikisha kuwa wanakuwa pamoja katika maisha yao yote. Hivyo ikawa marko akitoka shule tu anakwenda kumsubiri zuhura karibu na kisima katika jiwe kubwa lililokuwa chini ya mbuyu.

Walikuwa wakifurahi kila wakikutana kwani walikuwa wakisimuliana vingi vya ndani na kupanga malengo yao. Siku moja zuhura aliaga kuwa anaelekea mtoni k**a kawaida yake ambapo alifika kisimani akaiweka ndoo na kuanza kuita kwa sauti k**a kawaida yake kumjuza marko k**a alikuwa amefika. Lakini hakupata majibu hivyo ikamlazimu kuanza kumtafuta mpenziwe huku moyoni akiwa na hofu kubwa mno...
ITAENDELEA

yuko wapi marko na nini hatima ya kisa kibwagizo hiki?

Want your establishment to be the top-listed Arts & Entertainment in Iringa?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address

Njombe
Iringa