Benedict Solver Msuya
bmsuyakid
28/03/2026
CONGLATULATION
CPA METHUSELA
10/01/2026
Focus on doing what is right, not being right. And stay humble. It will make you comfortable with who you are so you can let go of fear of making mistakes.
TAFAKARI YA JUMAPILI: HABARI YA NABALI NA ABIGAILI, JIFUNZE KABLA HAUJAHARIBIKIWA.
“…._Na jina la mtu huyo aliitwa Nabali na jina la mkewe aliitwa Abigaili, na huyo mwanamke alikuwa MWENYE AKILI NJEMA, MZURI WA USO bali yule mwanamume alikuwa HANA ADABU, tena MWOVU katika matendo yake….” (1 Samweli 25.3).
Nabali alikuwa tajiri, maarufu na mtu mwenye pesa. Alijipatia mke mzuri sana ila pia mwenye akili.Mwanamke huyu alimsaidia kulinda utajiri wake, kumuepusha na majanga na kumsitiri udhaifu wake.
Somo 1: Unaweza kuwa mwanamke MZURI na MWENYE AKILI, ila hiyo haikupi “guarantee” ya kuolewa na mtu ANAYEJITAMBUA. Anaweza kuwa na KAZI, MALI na PESA ila akawa mtu wa HOVYO atakayekufanya usiishi kwa AMANI.
Somo 2: Mwanaume akishakusanya MALI na PESA, atahitaji kuwa na Mwanamke mwenye AKILI na HEKIMA ili amsaidie kuzitunza. Abigaili angekuwa mtu asiyejielewa, utajiri wao wa familia ungepotea siku moja tu. Alifanya “MISSION” ya kuokoa utajiri wa kifamilia kwa kutumia AKILI SANA. Uzuri ni muhimu ila inabidi AKILI nayo iwepo.
Biblia inaposema uishi na mwanamke kwa akili, inamaanisha pia na yeye ana AKILI; unatakiwa UZITAMBUE na UZITUMIE.
Somo 3: K**a NABALI hakuthamini haimaanishi hauna thamani. Ukiangalia utaona kabia Mume wa ABIGAILI hakuwa anathamini MAWAZO na MCHANGO wa ABIGAILI. Ila baada tu ya KUFA, basi DAUDI aliamua kumuona FASTA. Maana yake, usipotumia ULIYENAYE, kuna siku atachukuliwa na wanaoona thamani yake.
Somo la 4: Inahitaji UNYENYEKEVU kuishi na mwanaume k**a NABALI. Sijui ABIGAILI alipenda nini kwa mumewe, inawezekana mali au pesa au kingine chochote. Ila gharama kubwa aliyohitaji kuingia ni UNYENYEKEVU. Yaani ilibidi ASHUKE chini ili ASAIDIE MUME wake asiaibike. Tena HAKUTANGAZA hata baada ya kufanya. Watu walimuona ABIGAILI anaenjoy sana kwa sababu ya UTAJIRI wao, ila alikuwa ana changamoto kubwa na za kila siku.
Ukiwa NABALI unamuhitaji ABIGAILI, ila ukiwa ABIGAILI jifunze njia bora ya kuishi na NABALI. K**a bado haujaingia kwenye MAHUSIANO, jitahidi kumuepuka NABALI.
Joel Arthur Nanauka
28/03/2025
NATURE
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Telephone
Website
Address
Iringa