ALFAKHA CONSULTING AGENCY

ALFAKHA CONSULTING AGENCY

Share

KWA USHAURI ELIMU NA UWEZESHAJI KWENYE BIASHARA NA UJASIRIAMALI TANZANIA.. USAJILI WA KAMPUNI NA TAASISI. ELIMU YA UCHUMI NA KANISA

28/03/2026

BARUA YA WAZI KWA VIJANA WOTE WA TANZANIA

Na Alphonce Leonard Alphonce

Leo ninawaandikia kwa moyo uliojaa matumaini na imani kuwa kila kijana anaweza kubadilisha maisha yake kupitia elimu ya ufundi stadi. Elimu hii siyo ya kujifunza mikono tu, bali ni msingi wa ajira, ujasiriamali, na maisha ya kujitegemea. Ni silaha ya nguvu ya kiakili na kifedha inayoweza kufungua milango ya fursa zisizohesabika. Kila kipaji ulichonacho, kila ujuzi unaojifunza, ni hatua ya kujiweka kwenye mstari wa mafanikio.

Vijana, elimu ya ufundi stadi inapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza katika maisha yetu. Haipendiwi kuangaliwa k**a chuo cha pili au mbadala wa shule za kawaida. Wenzetu Ulaya wamefanya wazi kuwa mazoezi ya vitendo na ufundi stadi ndiyo nguzo kuu ya ajira na maendeleo ya kijana. Hivyo, ni wakati wetu kuwa makini, kuthubutu kujifunza, na kutumia kila fursa ya mafunzo ya vitendo. Kila somo, kila stadi, ni uwekezaji wa maisha yako ya baadaye.

Kwa wazazi, wadau, na serikali, nawahimiza kwa dhati: heshimuni,wekeze, na himizeni elimu ya ufundi stadi. Vijana wetu wanahitaji rasilimali, mwongozo, na sera zinazowezesha kupata ujuzi halisi. Kila shilingi inayoenda katika mafunzo ya vitendo ni shilingi inayorudishwa mara kumi kwa taifa na kijana. Hatuna budi kuona kuwa elimu ya ufundi stadi si ya hiari, bali ni nguzo ya maendeleo ya taifa letu.

Vijana wenzangu, msisubiri mtu afanye kitu kwa niaba yenu. Chukua hatua sasa! Jiunge na mafunzo ya vitendo, jifunze ujasiriamali, tambua vipaji vyako, na jenge nidhamu, maadili na mwelekeo sahihi wa maisha. Hakuna nafasi ya kukosa mafanikio pale mtu anapothubutu, kujitahidi, na kutumia kila fursa kwa busara. Kila hatua ndogo inazalisha matokeo makubwa, na kila ujuzi ni chombo cha kuunda maisha yako.

Mwisho, napenda kusisitiza: Kijana + Ujuzi = Uhuru. Uhuru wa kuchagua maisha yako, uhuru wa kuunda familia yako na jamii yako, na uhuru wa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa. Tumia nguvu yako, amini ndoto zako, heshimu elimu ya ufundi stadi, na uwe mfano wa kizazi kinachojitahidi. Taifa letu linahitaji vijana wenye ujuzi, uthubutu, na mwelekeo wa mbele.

Kwa heshima na matumaini,
Alphonce Leonard Alphonce

27/09/2025
18/05/2025

"*Jifunze Kuishi Ndani ya Kusudi la Mungu*"

*Kila mwanadamu amezaliwa kwa kusudi maalum. Hakuna aliyeletwa duniani kwa bahati mbaya. Kila pumzi uliyopokea ni uthibitisho kuwa kuna jambo kubwa Mungu amekuweka ulimwenguni kulitimiza*.

Katika Waamuzi 6:11, tunamwona Gideoni—mtu ambaye, kwa mtazamo wa nje, hakuwa na dalili yoyote ya ushindi au ujasiri. Alikuwa akipepeta ngano shimoni, mahali pa kujificha kwa sababu ya hofu ya adui. Lakini Mungu alimwona tofauti. Alimwita kwa jina ambalo hata yeye mwenyewe hakujiita: "Wewe ni shujaa!"

Huu ni mfano mzuri wa jinsi Mungu huona kilicho ndani yetu hata tunapojificha katika mashimo ya hofu, mashaka, na maumivu ya zamani. Wakati mwingine, maisha huleta changamoto zinazotufanya tujione wadogo, tusio na maana, au tusiostahili. Lakini ukweli ni huu: wewe ni shujaa.

Acha kuishi kwa hofu.
Acha kujificha nyuma ya udhaifu na historia ya kukatishwa tamaa.
Simama kwa imani. Tambua kuwa umetumwa kwa kusudi.

Kuanzia sasa, chukua nafasi yako.
Amka toka shimoni la kukata tamaa.
Tazama mbele kwa matumaini mapya.

*Wewe ni mtu muhimu sana. Ushindi wako uko karibu pale unapoanza kuishi ndani ya kusudi la Mungu*.

16/05/2025

Sababu 7 Zinazokufanya Upoteze Fursa za Kiuchumi
Na: Alfred Mwahalende | Simu: 0758 051 641

Wengi hupoteza fursa muhimu si kwa sababu hazipo, bali kwa sababu ya vikwazo vya ndani k**a woga, uvivu, au kukosa maarifa. Hofu ya kushindwa huwazuia wengi kujaribu, wakati wengine hukosa mafanikio kwa sababu ya kufanya mambo kwa mazoea bila kujitolea kikamilifu.

Pia, kulalamika kila wakati badala ya kuchukua hatua ni kikwazo kingine kinachowazuia watu kuona nafasi za kubadilisha maisha yao. Kukosa maarifa ya soko au biashara kunasababisha hata mawazo mazuri kushindwa kuzaa matokeo chanya.

Dharau kwa ushauri wa wengine, kukata tamaa mapema, na kutokuthamini michango ya timu ni sababu nyingine zinazoangusha miradi mingi. Mafanikio ya kiuchumi yanahitaji ushirikiano, maono, na uvumilivu wa kweli.

Jifunze zaidi kupitia Fursa 99 za Kiuchumi Tanzania – kitabu chenye nguvu ya kukuongoza katika safari ya uhuru wa kifedha. Wasiliana sasa: Alfred Mwahalende | 0758 051 641.

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address

UYOLE
Mbeya
00000