Ishi Njozi

Ishi Njozi

Share

JE UMEKATA TAMAA?..Hivi unajua kukata tamaa Ni Hali ya kawaida ya maisha? LAKINI K**a hatua muhimu hizita chukuliwa zaweza kuleta madhara makubwa?

22/03/2023

*Siri hii...*

Je unapitia changamoto ya kuanza Mambo na Kisha kuacha baada ya muda Fulani?

Au,

Unaanza na unakata tamaa unapo karibia hitimisho?

Leo Siri moja kubwa kutoka kwa waliofanikiwa,

Yaani Mabilionea zaidi ya Mia tatu Dunia nzima,

Nayo Ni *Uthubutu*

Kila unayemuona akiwa juu Leo alikuwa chini,

Kila unayemuona Ana furaha Leo alikuwa na huzuni,

Kila unayemuona Ana pesa leo alikuwa na nyakati za kutokuwa na pesa,

Kwa kila Hali ambayo unamuona mtu Fulani kuwa juu leo,

Naye alikuwa na nyakati zake za hali mbaya na kuumiza Sana,

Ila waliamua *Kuthubutu* kwa kwa kila Hali,

Kupambana hata K**a walipitia hisia za kukatisha tamaa,

Japokuwa walichekwa,

Walidharauliwa,

Walikejeliwa,n.k

Bado waliamua *kuthubutu*

Yaani kupambana mpaka Lengo litimie,

Haya naongea na wewe Sasa,

Amua *Kuthubutu*

Pambana mpaka Lengo lako litimie,

Natumaini umepata kitu hapa,

Mpaka Wakati mwingine,

Njozi Media.

04/02/2023

*Bustani ya Maajabu...*

"Hata usipopanda chochote bustani hii inatoa matunda..."

Umewahi kuiona bustani ya aina hiyo?

Naamin unashangaa kweli ipo?

Na K**a ipo ikwapi?

Cha kushangaza Ni kwamba kila mtu anayo bustani hii,

Lakini Ni wachache Sana wanajua kwamba wanayo,

Wewe unaijua bustani hiyo?

Fikiria kwa dakika moja...

Nahesabu muda ⏱️.

Haya tuendelee,

"Linda sana Moyo wako kuliko yote ulindayo..."

Lilimsikia siku moja mchungaji akisema,

Kwa Nini?

Nimeelewa vizuri zaidi baada ya kufahamu hili...

"Akili ya mtu Ni sawa na Bustani"

Hili linashangaza au sio?

Ngoja nikwambie zaidi,

Bustani hii hutoa kila aina ya matunda MABAYA kwa MEMA,

Lakini,

Bustani hii hutoa matunda ya aina moja kwa Wakati...

Matunda MEMA au MABAYA.

Matunda mema Ni K**a, Mafanikio,Furaha,Amani,Tabia Njema n.k

Matunda haya yanapatikana kwa juhudi za dhati,

Yaani kukazana kweli kweli,

Hii huhusisha,

•Kuwa makini na unavyosoma,

•Kuwa makini na unavyosikia,

•Kuwa makini na unavyoona.

Ndiyo,Inahitaji JUHUDI KUBWA.

Wivu,Ubinafsi,Wizi,n.k haya Ni baadhi ya Matunda mabaya.

Aina hii ya Matunda hauhitaji nguvu Sana,

Ukikaa tu unayapata,

Yaani,

•Utasoma kila kitu,

•Kusililiza kila kitu,

•Kuangalia kila kitu...

Swali la kujiuliza kwa kila kitu unachofanya Ni....

"Je Ni matunda gani nitapata kwa hiki ninachofanya?"

Na kadri unavyo SOMA,SIKIA na hata KUANGALIA ni MBEGU UNAPANDA.

Bado Kuna tumaini ndugu,

Anza Sasa,

Kwa Nini uje kujilaumu kwa kutoamua kuwa na matunda mema?

Nini kinachokuzuia Kuchukua hatua Sasa ya kuwa na matunda mema?

Amua Sasa.

Inawezekana!.

Jumamosi Njema!.

@ Ishi Njozi Media.

Want your restaurant to be the top-listed Restaurant in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address

Mbeya

Opening Hours

Monday 05:00 - 11:00
Tuesday 05:00 - 11:00
Wednesday 05:00 - 16:00
Thursday 05:00 - 11:00
Friday 05:00 - 11:00
Sunday 05:00 - 11:00