El Gospel Power
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from El Gospel Power, Full Gospel Church, .
28/07/2025
El Gospel Power Online TV ni Televisheni mpya ya mtandaoni inayojikita katika kuhubiri na kutangaza Injili ya Yesu Kristo kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu. Imebeba dhamira ya kuleta mapinduzi makubwa katika ulimwengu wa Online TV za Injili, kwa kutumia teknolojia ya kisasa, vipindi vyenye ubunifu, na sauti ya kipekee ya kiroho kwa kizazi cha sasa.
El Gospel Power haijaanzishwa tu k**a chombo cha habari njema, bali k**a jukwaa la kuinua huduma, kuinua vipaji vya kiinjilisti, na kufikia mataifa kwa Neno la Mungu.
Online TV hii itaanza rasmi kufanya kazi hivi karibuni ikiwa imejipanga vyema kuwa sauti mpya ya nguvu ya Mungu katika mitandao ya kijamii na ulimwengu wa kidigitali.
El Gospel Power – Preach the Power of God Through the Gospel.