Majembe12

Majembe12

Share

ISAYA 62:6d
👉Ninyi wenye kumkumbusha Bwana msiwe na kimya.

14/02/2024

👉Ukweli ni kwamba Watu Wengi tunakesha tunalia mbele za Mungu,tukiomba msamaha..na kupeleka haja zetu,Kuna mda tunapokea majibu yetu na Kuna mda hatupokei..
✓✓kuna sababu kadhaa...zinazosababisha tusipokee na tusijibiwe..Moja inawezekana tunaomba vibaya..si k**a Mungu
apendevyo..👇

Yakobo 4:3
[3]Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
((kwahiyo Kuna mda hatujibiwi kwasababu tunaomba vibaya...tunaomba kwa tamaa zetu...si k**a Mungu apendavyo..maana ukweli ni kwamba Mungu hutupatia kwa mapenzi yake..sio yetu..ndio maana Yesu alisema...👇

Mathayo 6:10
[10]Mapenzi yako yatimizwe,
hapa duniani k**a huko mbinguni.
((kwahiyo Kila mtu Kuna namna Mungu kampangia..mahitaji yake na kesho yake na njia yake...Je wewe unavyoomba unaombaje?? sawa sawa na mapenzi yake au Yako?? Yesu wakati anajua kuwa atasulubiwa na akijua yote...aliomba ivi..

Mathayo 26:39
[39]Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si k**a nitakavyo mimi, bali k**a utakavyo wewe.
(ukisoma mstari wa 38..anasema..👉Mathayo 26:38
[38]Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.
((kwahiyo ule mwisho wake ulimtia huzuni..aliogopa alitamaani isiwe hivyo..lakini unapoenda mstari wa 39..unaona anasema lakini mapenzi Yako yatimizwe,,kwahiyo vyovyote unavyopita...kwa namna yoyote Ile lazima uyajue mapenzi ya Mungu katika Hilo...! ujue kusudi la hilo jambo,linalokupata ndipo utagundua namna Gani wapaswa kumuomba Mungu Ili mapenzi yake yatimizwe na usiliondoe tumaini lako kwake.. )

Sababu ya pili inayoweza sababisha usijibiwe maombi Yako ni KUTOKUSAMEHE.
👉Yesu anasema katika kitabu Cha marko..👇

Marko 11:25
[25]Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
((kwahiyo simple ni hivi Ili Upokee majibu ya maombi Yako,,jifunze kusamehe...unapoomba Toba kwa Mungu..hakikisha nawewe umewasamehe waliokukosea..la sivyo Neno liko wazi..usiposamehe hutasamehewa,,..Tena Yesu anasema...👇

Mathayo 6:14-15
[14]Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
[15]Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

👉katika Yote kua,katika Hekima ya Mungu katika kulisoma Neno lake..Ili likae kwa wingi ndani Yako,Na ndipo utafahamu zaidi juu ya Mungu unayemtumikia....na Unayemuabudu.

BARIKIWA🙏🙏.

30/10/2023

NENO LA SIKU

30/10/2023

SOMO:KAMA MKIKUBALI NA KUTII MTAKULA MEMA YA NCHI

Ukikubali kuisikiliza sauti ya Mungu na kutii maagizo yake,utakula mema yake..Maana Kila tunachokihitaji Kiko mkononi mwa Mungu au ndani ya UWEZO wake..
Lakini ivi vitu huvipati kwa bahati mbaya,unavipata Kwa kufuata utaratibu wake Mungu,

👉UKUBALI VIPI NA UTII VIPI?
yaani mfano ukiitwa hatua ya kwanza unaitikia wito,
Hatua ya pili unasikiliza kilicho kwenye wito unaambiwa Nini au unaagizwa nini...
Baada ya kusikiliza wito,ukiiupokea na kuutendea kazi ndio tunaita UMEKUBALI NA UMETII

👉Kwahiyo Mungu ametuahidi mema ya nchi,lakini hayo mema tunayapata kwa kukubali sauti ya Mungu na kutii maagizo ya Mungu,Kila mtu Kuna namna kasemeshwa na Mungu lakini shida ipo kwenye kukubali kuisikiliza sauti unayoisikia na kutii maagizo ndani ya hiyo sauti.Kuna watu wamesikia sauti ya Mungu na wameipuuza,hao watu kwao baraka,au utajiri au mema ya nchi kwao ni ndoto kwa maana anasema..

👉BARAKA ZETU zote zipo mkononi mwa Mungu, **MITHALI 8:18 (utajiri na heshima ziko kwangu,Naam utajiri udumuo na haki pia.)**
Lakini ivi vitu vinakujia ukikubali na ukiitiii sauti ya Mungu wako.

Lakini usipoikubali sauti ya Mungu na kuitii...
Ni vigumu kula mema ya nchi
Tazama **ISAYA 1:20**
bali k**a mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya.
👉Ivo ni muhimu kuisikia ukisikia sauti ya Mungu uitii Ili ule mema ya nchi,vingine Biblia inasema myaangamizwa kwa upanga..na BWANA yeye mwenyewe kwa kinywa chake amenena hayo.

🌹GOD BLESS YOU🌹

Want your school to be the top-listed School/college in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address

Mbeya