Abeid Mugeta

Abeid Mugeta

Share

from Allah, for Allah, to Allah

14/07/2026

If you succeed in deceiving someone do not think he is a fool, instead realize how much he trusted you

13/07/2026

Ikiwa Thamani ya kombe unaiweza usiingie kwenye hayo mashindano

11/07/2026

Niliwahi kuambiwa ukuu wa Mungu kupitia simulizi za wengine. Niliamini kwa masikio, lakini sikuuelewa kikamilifu hadi nilipokuwa shahidi wa rehema zake mwenyewe...

Nilisimuliwa utukufu na daraja za ufalme wake, sikuweza kusadiki hadi nilipoona mwenyewe...

Jana tarehe 10 July 2026 siku ilianza kwa utulivu kabisa mpaka jioni yake ile, hadi ulipo wadia wakati ambao sikujua ulipangwa katika Jana yangu....

Mimi na rafiki, kaka na mkuu wangu Mbowe, usiku wetu ulianza kwa changamoto isiyo tarajiwa...

Sekunde chache tu za uzembe wa dereva wa bajaj ile, almanusura ubadili majina yetu...

Speed kali sana Kisha unataka kuchati brother, kwani uliambiwa sisi tumechoka kuishi?...

Ghafla sana bajaji ilihama na kuingia kwenye mtaro, katika ile barabara iliyojengwa kwa lami...

Bila kujitambua tulikuwa tayari tupo chini huko mtaroni, Kila mtu akiomba dua kwa kadiri ya imani aliyojaaliwa...

wakati mwingine Mungu anaruhusu tupitie vitu, ili tuone ukuu wake kwa macho yetu wenyewe si kwa kusikia tu...

Alhamdulillah we survived, tuishi kwa wema na amani duniani tunaondoka ghafla...

Alhamdulillah

09/07/2026

Baada ya yote tuliyopitia,hatimaye upendo umeshida...

Nafsi zilipendana kwa mara ya kwanza tu, iweje tulitaka kuzikatili?..

k**a ningeweza wakati ule, ningeomba ugomvi wetu usiathiri hisia na upendo wetu...

Tumepita milima mito na mabonde, tambarare yetu ile pale mbele tushindwe kuserereka...

Ombi langu mara hii tofauti iwe kati yetu, na sio kuhusisha mioyo yetu utaniumiza...

Tukosane sie ila amani ya moyo wangu, hilo tabasamu lako hakika nimefia hapo...

karibu tena kwenye safari, yetu kuisaka milele yetu pamoja...

karibu tena kwenye nyumba ya marashi ya moyo wako, natumaini utakuwa Cleopatra wangu...

karibu nyumbani kwako📌
Maalim Mugeta Ukhty Maryam Žędÿ Ďe SįmßäTz

05/07/2026

Tunaishi na watu ambao furaha zetu zinawaumiza kuliko shida zao
usiache kuswali 📌
Maalim Mugeta

05/07/2026

Naikumbuka siku ile njema katika sehemu ya maisha yangu, siku ambayo mboni za macho yangu ziliinasa sura yako kwa mara ya kwanza...

K**a itatakiwa nyakati moja kuelezea kipindi muhimu kuliko vyote maishani mwangu, basi ukiachana na siku yangu ya kuzaliwa nitaitaja hiyo...

Wakati katika moja ya nyakati bora zaidi kuwahi kuziishi, Nilikuwa simba katikati ya mbweha wakali mno...

Ndio kumbukumbu zimenirejeshea taswira ile, muhimu na ya kuvutia sana mithili ya almasi...

Khadija nimezikumbuka zile moments za " kunywa nibakishie" ni lazima nikiri kwa dhati ya moyo na kinywa nimezikumbuka...

Waswahili walisema " k**a unakipenda kipambanie, wakaenda mbele na kusema zaidi " ukimpenda mtu mbadilishe awe unavyotaka"...

Isivyokuwa bahati ulinikatia tamaa iliniuma sana, lakini je ULISHINDWA NINI?nambie kipenzi ulishindwa wapi?

I never wanted a perfect relationship, I just wanted someone that isn't going to give up on me.....

Ile mawio ya upendo wetu iliyokuwa ya hisia za kweli, ghaafla sana wingu lilitanda na kupoteza nuru ya upendo ule sijui ni husda ila I miss you...

special thanks to
Ukhty Maryam
bin mbwana 📌

02/07/2026
30/06/2026

shukran za punda nimateke
waneni walinena

30/06/2026

Najiuliza, nilikuwa mjinga kiasi gani hadi nikazipuuza dalili zote. Wakati huo, meli ya penzi letu ilikuwa tayari inazama....

Licha ya dhoruba, mawimbi makali na kelele za baharia wenzangu, nilichagua kuwa kipofu kwa ishara zote za hatari katika safari yetu....

Wanasema ukiona manyoya ujue kaliwa, mwenzenu manyoya niliona ila nikajipa Imani ya kuwa yeye aliweza kuwa salama hivyo hakuliwa NILIJIDANGANYA..

Red flash ziliwaka mara nyingi kunionya, lakini kiburi na jeuri vilinipa maelfu ya sababu za kuamini kuwa zilikuwa njama za watu....

Leo nashindwa kujua k**a natakiwa kujilaumu au kushukuru kwa kuwa kaidi, hasa kwa wale wote walio nionyesha upendo wa kunielekeza njia wakati ule...

Nilipozinduka, nilikuta mabaki ya manyoya pekee, poor me sikuziba ufa nguvu ya kujenga ukuta Sina...

TOO LATE
Ukhty Maryam
Maalim Mugeta
Abeid Mugeta

22/06/2026

kipenzi mimi na wewe role model wetu awe nani, katika tasnia hii ya huba...

Kila siku tunchanganya kemikali za kicheko na mawazo yetu, vipi kioo chetu wawe Marie curie na piere walo kutana maabara...

Hatuna historia ya mapambano ya uhuru popote, ni vipi penzi letu mfano uwe wa Nyerere mtoto wa kizanaki na mkewe bi maria...

Hakuna harakati tunafanya wewe na mimi, vipi tuwaige Martine Luther king na mkewe Coretta Scott king....

Vipi kwa Queen Victoria na prince Albert wa uingereza, tatizo letu moja wote hatuna damu ya ufalme hata kidogo...

Cleopatra VII na Mark Antony wa misri historia yao ngumu, sie ya kwetu ni machozi ya samaki ndani ya maji...

Au la kwetu liwe k**a la kajala na mmakonde yule, tuachane bila sababu na kurudiana ghafla tuwachoshe washakunaku...

NIPE JIBU

Want your business to be the top-listed Media Company in Morogoro?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Address

Mazimbu Morogoro
Morogoro