Msheshe Rashid
Ukurasa wa msese wa kondeni Ukurasa huu waakisi kazi za uandishi unaokuza Kiswahili
sisi si maua wala,hatukai mabunduki,
sisi si manyau wala,hatupendelei dhiki,
sisi si mabomu wala,zana za kuzima haki,
tupo zaidi ya kito,utu huvai jeuri.
Kuwa na SUBIRA utahitaji IMANI.
Kuwa na imani utahitaji USULI WA MAMBO
Kuwa nao usuli wa mambo ndio MWANZO WA KUJITAMBUA.
Ishi maisha.
30/03/2022
K**A SITUNGI SHAIRI!!
Ni barua mwafulani,kwako wewe mahiri,
Utungae kila fani,mjuvi na mjasiri,
Leo waja na ughani,wanena bila kipuri,
K**a situngi shairi,nitungayo ni upupu!
/
Awali ninakiri,usemayo ni nasaha,
Ulo mwema na mzuri,tena usionihaha,
Kando na kushika hari,wanikosea furaha,
K**a situngi shairi,nitungayo ni upupu!
/
Sina haja na kaida,k**a ndugu ywapinda,
Yule kaka yule dada,nitungapo namwinda,
Mawi aasi kudoda,k**a mkosa mkanda,
K**a situngi shairi,nitungayo ni upupu!
/
Ni hofu kwa awashwaye,asomapo ywabipu,
Vibaya tumdhaniye,yu jitu bila ya zipu,
Yu mzaha aonaye,eti nafuma majipu,
K**a situngi shairi,nitungayo ni upupu!
/
Asijifanye dubu,wa jangwa mgeni,
Asutwapo yu bubu,akitenga masitoni,
Hoja zinapodhurubu,hujitia hamsini,
K**a situngi shairi,nitungayo ni upupu!
/
K**a nakubetua,vina chenga vyakupiga,
Ndipo wajibibitua,kwa kebehi za kukoga,
Mwenzio ninabenjua,hadi tungo zajibwaga,
K**a situngi shairi,nitungayo ni upupu!
/
Nakuasia mwenzangu,mimi si k**a wao,
washairi wenye majungu,watungao bila mwao,
Usitunge mapurungu,ukidhani una bao,
K**a situngi shairi,nitungayo ni upupu!
/
Waraka ninaufunga,ninaweka wasalamu,
Iwapo nimedhulumu,mniridhie kaumu,
Mja hapiki sumu,kunywa kisha kulaumu,
K**a situngi shairi,nitungayo ni upupu!
©msese wa kondeni.
16/08/2021
AUGUAYE HUANGALIWA.
//
Tatizo hutatuliwa,tata likatatuka,
Riziki hujuhudiwa,mlo ukatarazika,
Na baya huambuliwa,mbali likajizika,
Dama ndivyo hivyo huwa,muugua hwangaliwa.
//
Ni yakini maridhawa,ganga ganga kuganguka,
Muwele anouguwa,kutunzwa na kutunzika,
Ili nafuu ya kuwa,impate kwa haraka,
Dama ndivyo hivyo huwa,muugua hwangaliwa.
//
Auguaye suluhuwa,anayo tiba tibika,
Si Dawa tu kubuhuwa,na pia kushufahika,
Mathali gahugahu wa,gehugehu akiruka,
Dama ndivyo hivyo huwa,muugua hwangaliwa.
//
Kuseneka kukipowa,Siha na hutatarika,
Ukajyona Umetowa,zito lotasawarika,
Mwenye shida hutasuwa,maono kusaidika,
Dama ndivyo hivyo huwa, muugua hwangaliwa.
//
Khamsani natongowa,tongoo kutafitika,
Vina vinakoma vya Wa,vinasita pia vya Ka,
Takilifu ikikutuwa,kite si dhema kuwika,
Dama ndivyo hivyo huwa,muugua hwangaliwa.
©msese wa kondeni.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Bahati
Nairobi
Opening Hours
| Monday | 09:00 - 17:00 |
| Thursday | 09:00 - 17:00 |