Jesus Power Ministry
Jesus power ministry ni huduma ya Mungu yenye makusudi ya kurejesha hatima za watu wake mahala alipo
21/09/2024
THE DIVINITY LEADERSHIP (UONGOZI WA KIUNGU)
Bwana Yesu afisiwe wana Mungu popote pale mlipo.
Bwana Yesu anasema mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na la kushoto,wengi sana hawajui kwanini Bwana Yesu alitumia neno hili kuwa mojawapo ya kiungo muhimu kwenye uongozi.
Hapa Bwana Yesu alikuwa anamaanisha kunyamaza nyakati za hatari,kwenye hatari yoyote huwezi kuhimili hisia zako binafsi lazima utataka kujipambania iwe utapona au hautapona.
Ikimbukwe kwenye uongozi wa Bwana Yesu, aliletewa habari ya kukatwa kichwa kwa mtu wake wa karibu sana ambaye ni Yohana mbatizaji.
Bwana Yesu alijitenga kwa Muda kwenye kundi kubwa la watu.
Kwanini alijitenga kwa muda baada ya kuletewa taarifa hiyo.
Yeye alienda kufanya tafakuri binafsi na Baba yake aliyemtuma alafu baada ya kuludi hakuja na jawabu la kwamba waingie mtaani yeye,wanafunzi wake na wafuasi wake kuandamana dhidi ya ukatili aliyofanyiwa mtumishi wake Yohana,akaendelea na shughuli yake k**a kawaida.
Hapa ibilisi alikuwa anatafuta hisia binafsi za Bwana Yesu namna atakavyoweza kuonyesha ghadhabu yake dhidi ya ukatili ule lakini matokeo yake akanyamaza,shetani alikuwa anampima yeye ambaye anasema vita yake si katika mwili bali ni katika ulimwengu wa roho je ataweza kuhimili kuzuia hisia zake kwa huyu mpendwa wake.?
Ndugu zangu tunapozungumzia uongozi wa kiungu ni uongozi teule,usiondeshwa na mihemko bali unaendeshwa kwa ufahamu,hekima na akili,haya mambo makuu matatu yanakusaidia kujua chanzo halisi cha tatizo na kutokea hapo unajua chanzo sahihi cha suruhisho.
Watumishi wa Mungu wakijitokeza kwenye vyombo vya habari wakihamaki k**a ulimwengu unavyoenda manake unalivunja daraja la amani,upendo na ustahimilivu katika Taifa.
Watumishi wa Mungu wao wamepewa neema ya kuonyeshwa mambo yaliyoko sirini yanayotendeka na ambayo yataweza kutendeka baadae,na kwahivyo siyo watu wa kukulupuka hovyo hovyo kutoa majawabu na majawabu yao huleta suluhisho la kweli kiasi cha aliyetenda uovu huo kujiona yu uchi ndicho kilichofanyika kwa mtumishi wa Mungu Suleiman dhidi ya mabinti wawili makahaba waliokuwa wakigombania mtoto ile kesi ilisuluhishwa kihakili sana na amani ikatawala pande zote.
Bila kujua chanzo cha tatizo ni ngumu kupata utulivu wa kweli wa kudumu kwa mtu binafsi,jamii,au hata Taifa.
PUT GOD FIRST FOR EVERYTHING YOU DO!!!.
Geofrey Julius-Jesus power ministry Tz
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the place of worship
Telephone
Address
Usa-River
Arusha
255