imacrobot

imacrobot

Share

Ujue ulimwengu wa sasa na ujao.

10/08/2021

CYBERSECURITY.
Cybersecurity ni jaribio la kulinda mifumo ya kidigitali, networks pamoja na program zisiingiliwe au kuharibiwa na mashambulizi ya kidigitali ambayo tunayaaita cyberattacks.Mashambulizi hayo hufanyika kwa lengo la kuharibu au kubadili taarifa muhimu zilizopo katika mfumo wa network au kuhamisha fedha toka katika account ya mtu bila yeye mwenyewe kujua.kwa kifupi kitendo hichi ndio hufahamika k**a udukuzi au ku-hack.

Cybersecurity ilikuwepo kwa lengo la kudhibiti uhalifu huo wa kimitandao ila sasa changamoto kubwa iliyopo na inayosababisha mpaka leo kuendelea kuwepo kwa ripoti za udukuzi wataalamu wanasema kuwa, kutengeneza ulinzi madhubuti kabisa wa kukomesha vitendo hivyo ni changamoto kwa sababu kwa sasa vifaa ni vingi sana na pia kila siku kadri teknolojia inavyozidi kukua, ndivyo jinsi washambulizi wa kimitandao wanazidi kuongeza na kuvumbua mbinu mpya.Ni vigumu kuwazuia wasiendelee na uhalifu huo.

Mafanikio yanayolenga kufikia ulinzi madhubuti wa cybersecurity una matabaka mengi ambayo yamejigawanya katika sehemu nyingi k**a vile katika kompyuta, networks, programmes au data, hivyo basi itakuwa bora zaidi kuunganisha na kutengeneza mfumo mmoja tu madhubuti ambao utazuia mashambulizi hayo.Tuchukulie mfano katika makampuni itakuwa bora zaidi k**a watu wote watakaa na kuamua kutengeneza mfumo mmoja wa ulinzi ambao utakuwa madhubuti kabisa, hii kwa kiasi fulani itasaidia kudhibiti uhalifu huu.

Mfumo huu unapaswa kutumika kikamilifu kabisa katika miaka ijayo baada ya magari ya umeme kusambaa sehemu kubwa ya dunia.Ndio, ni kweli magari ya umeme yanatunza mazingira ila je, vipi k**a mfumo wake wa cybersecurity utaingiliwa na wadukuzi?.
Hili ni swali ambalo unapaswa kujiuliza kwani kitu chochote kile kitakachounganishwa tu na internet ni rahisi sana kushambuliwa na wadukuzi.
Unaweza ukawa upo ndani ya gari yako na ukashambaa ghafla mifumo ya utendaji kazi ndani ya gari inabadilika bila wewe mwenyewe kugusa sehemu yoyote ile, hii ni hatari kubwa sana kwani ajali huweza kutokea.
Japo unaweza kupata viashiria vitakavyokufanya uhisi kuwa gari yako imeingiliwa na cyberattackers.🤔

Next time nitakupa viashiria hivyo.

🙏Like
🙏follow

10/08/2021

JE, UNAWEZA KUNUNUA GARI LA KUCHAJI NNJE YA NCHI, ILHALI UNAISHI KATIKA NCHI ISIYO NA VITUO VYA KUCHAJI GARI HILO?.
Hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia makampuni mengi ya magari yanayotumia mafuta kutangaza kuachana na biashara ya utengenezaji wa magari hayo na badala yake magari mengi yatakayokuja miaka ijayo ni yale yanayotumia umeme.Sababu kuu iliyopelekea uamuzi huu ni kutokana na uchafuzi mkubwa wa mazingira duniani kwani, magari yanayotumia petroli yamekuwa yakizalisha kiwango kikubwa cha hewa ya ukaa (CO2) ambayo imekuwa ikiharibu tabaka la ozon kwa muda mrefu sana.
Mataifa mbalimbali duniani kwa sasa yamekuwa yakiwekeza nguvu nyingi katika kujenga miundombinu itakayosaidia magari hayo kutumika katika nchi zao mfano ni ujenzi wa vituo vya kuchaji.

Watu wengi wanaoishi katika mataifa ambayo bado hayajaanza kuwekeza katika mabadiliko haya wamekuwa wakijiuliza je, itawezekana kwao kumiliki magari haya ilhali bado hakuna vituo vya chaja katika nchi zao?.
Bahyad Jafari ambaye ni CEO wa ELECRIC VEHICLES COUNCIL, alipokuwa anatoa maelezo kuhusu magari haya alisema kuwa, "wamiliki wa magari ya kuchaji hutumia magari hayo tofauti na yanayotumia petroli kwani wataweza kuyachaji wakiwa nyumbani au kazini endapo tu k**a kutakuwa na kifaa maalum cha kuchaji".Mfano ni hapo juu katika picha ambayo inaonyesha gari la umeme likichajiwa nyumbani katika chaja yake.
Ni sawa na unavyounganisha simu yako na chaja yake iliyoweka katika soketi.
Hivyo basi utatakiwa kuwa na soketi yake ambayo utaiweka nyumbani au ofisini.
Dr. Whitehead alisema kuwa "ukiongelea kuhusu chaji ya nyumbani basi unapaswa kufahamu kuwa ni chaji inayochukua saa moja kila usiku", akimaanisha kuwa, utatakiwa kuchaji gari lako kwa muda wa saa moja kila usiku.

Vituo vya bararani hivi vitakuwa maalum kwa magari yatakayohitaji kiwango kikubwa sana cha nishati hii, mfano ni k**a magari yatakayotembea kilomita 270 kwa muda wa nusu saa.

Huu ndio ulimwengu ujao na inatabiriwa mpaka kufikia mwaka 2040 hakutakuwa kabisa na magari yanayotumia nishati ya mafuta. Makampuni mengi kwa sasa yameona kuwa hili ni fursa kubwa ya biashara na kuamua kuanza mipango ya kuzalisha magari haya mfano mzuri ni kampuni ya APPLE.

10/08/2021

DISNEY, YOUTUBE PAMOJA NA NETFLIX ZAUNGANA KWA PAMOJA NA KUWA SEHEMU YA BURUDANI KATIKA MAGARI YA TESLA.
kwa muda mrefu kampuni ya utengenezaji wa magari yanayotumia umeme nchini Marekani ijulikanayo k**a TESLA MOTORS, imekuwa ikijiboresha mpaka kufikia hatua ya kuwa miongoni mwa kampuni bora zaidi za utengenezaji wa magari nchini marekani.Kampuni hiyo imekuwa ikitengeneza magari yenye sifa za kipekee ambazo huchochea ukuaji wa soko lake kwa kupendwa na watu wengi sana nchini Marekani na mataifa mengine mengi nnje ya bara la Marekani.
Miongoni mwa vitu vinavyowavutia watu ni muonekano wa magari hayo na pia, magari hayo ni rafiki wa mazingira tofauti na kampuni nyingine za magari kwani magari hayo hutumia umeme tu katika kujiendesha.

Hivi karibuni kampuni ya DISNEY ambayo ni maarufu kwa utengenezaji na usambazaji wa filamu duniani iliungana na mitandao ya NETFLIX pamoja na YOUTUBE na kuwa k**a sehemu ya burudani ndani ya magari ya TESLA.
Watumiaji wa magari hayo watakuwa na uwezo wa kutazama video mbalimbali pamoja na kupakua filamu,miziki na burudani mbalimbali zitakazokuwa zinapatikana ndani ya magari hayo.Hatua hii imetajwa kuongeza mvuto na thamani kwa kampuni hiyo kwani burudani hizo zitaongeza hamasa ya watu kutaka kumiliki magari hayo.

Please follow

10/08/2021

NEBULA, KIWANDA CHA NYOTA ANGANI.
NEBULA ni eneo linalopatikana umbali wa miaka ya mwanga 1,500 kutoka duniani ambapo eneo hili ndipo mahali nyota huzalishwa.
Katika eneo hili maelfu ya nyota huzalishwa ambazo baadhi ni kubwa na nyingine ni ndogo sana kiasi kwamba hatuwezi kabisa kuziona kwa kutumia macho yetu tukiwa huku duniani.

photo:NASA

Tafadhali like,comment pamoja na ku-follow ukurasa huu

10/08/2021

MNARA MPYA WA DUBAI.
Ukizungumzia mji wenye majengo marefu duniani huwezi acha kuitaja DUBAI.
Dubai ndipo mahali panapopatikana jengo refu duniani, BURJ KHALIFA lenye urefu wa mita 828.
Miaka iliyopita Dubai ilitangaza rasmi kuanza ujenzi wa jengo lingine refu zaidi ya BURJ KHALIFA ambalo litakuwa na shape inayofanana na rocket.Taarifa kamili za urefu wa jengo hilo bado hazijatolewa ila inatajwa kuwa na urefu unaozidi mita 828.
Kwa taarifa zisizo rasmi zinasema kuwa jengo hilo litakuwa na urefu wa takriban mita 1300 😮😮😮
Engineer maarufu SANTIAGO CALATRAVA ndie mchoraji wa ramani ya jengo hilo na pia ndie aliechora ramani ya burj khahila.
Kwa matarajio jengo hilo lilikuwa likamilike mwaka 2020 ila kutokana na COVID19 ujenzi wake ulisitishwa.
Nako pia nchini Saudi Arabia wanaendelea na ujenzi wa jengo refu kuliko yote nchini humo litakaloitwa JEDDAH TOWER,ambalo litakuwa na urefu wa mita 1007.

Please like, comment and follow our page for more contents😀💪👍

Want your school to be the top-listed School/college in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Arusha