Msumba News Blog
Blog hii inajihusisha na machapisho ya kuhabarisha,kuelimisha na kuburudisha.
05/04/2025
MATIBABU YA MACHO KUFANYIKA BURE JIJINI TANGA.
TAASISI ya Bilal Muslim Mission of Tanzania Leo April 5,2025 imeanza zoezi la matibabu ya macho Bure kwa wananchi wa halmashauri ya Jiji la Tanga ikiwa ni katika jitihada za kukabiliana na matatizo mbalimbali ya macho ikiwemo mtoto wa jicho ambapo tafiti zilizofanyika zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 50 ya wananchi Mkoani Tanga wamemeathirika na tatizo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu amesema kuwa taasisi hiyo ambayo inafanya kambi hiyo kwa mara ya pili jijini hapa kutoka ile ya mwaka 2019 ambapo zaidi ya wananchi 3,000 waligundulika na tatizo la mtoto wa jicho na walipatiwa matababu, dawa pamoja na Miwani bure.
"Wadau wetu kutoka Bilal Muslim Mission of Tanzania wanakuja tena Tanga kwaajili ya kuiendesha kambi hii kubwa ya macho bure tulifanya mwaka 2019 niliwaomba na nashukuru Wamekubali ombi letu la kuja kutoa huduma hii kwa siku tatu kuanzia jumamosi hadi jumatatu katika viwanja vya shule ya Sekondari Usagara"
"Huduma zitakazotolewa katika kambi hii kubwa ni kupima na kupewa Miwani bure, watu wana kumbukumbu 2019 tulitoa Miwani zaidi ya elfu tatu kwa wakazi wa Jiji la Tanga ambao walipimwa na kukutwa na changamoto za macho"
"Lakini kambi hii itatoa dawa bure kwa watu ambao watapimwa na kukutwa na changamoto za macho na kutoa ushauri wa afya ya macho bure kutoka kwa madaktari bingwa wa macho na pia itatoa huduma za kusafisha mtoto wa jicho nure kabisa" alisema Ummy
Aidha mbunge huyo ameipongeza na kumshukuru taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania Kwa utayari wao wa kuendeleza ushirikiano ili kuwasaidia wananchi Kwa kushirikiana na ofisi ya mganga Mkuu wa wilaya hiyo kupitia kambi hiyo ambayo imedhaminiwa na kampuni ya simu za Mkononi ya Yas.
"Napenda sana kuwaalika wakazi wote wa wilaya ya Tanga kujitokeza kwa wingi kuanzia saa mbili asubuhi mpaka sasa tisa na nusu, naomba watu wafike mapema wapewe huduma " alisisitiza Mbunge huyo.
"Mimi k**a mbunge wa Jimbo la Tanga niwashukuru sana Bilal Muslim Mission of Tanzania Kwa kukubali ombi letu kuja kufanya kambi hii bure lakini jambo hili tunashiriana na ofisi ya mganga ya wilaya ya Tanga chini ya
02/04/2025
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa akitoa maelezo wakati wa kikao cha majumuisho ya Uchambuzi wa Mpango na Bajeti ya Mafungu 28 yanayosimamiwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa mwaka 2025\/26 kwenye k**ati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) leo tarehe 02.04.2025.
02/04/2025
Wananchi wametakiwa kukopa mikopo inayotolewa na Serikali na Taasisi rasmi ili kujiepusha na udhalilishaji unaoweza kutokea kutokana na kukopa mikopo yenye masharti magumu kutoka kwa Taasisi zisizo rasmi na kwa Wakopeshaji Binafsi.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Bw. Binuru Shekidele, alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake, ambayo ipo mkoani Mwanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali.
Aliongeza kuwa mikopo rasmi inayotolewa na Serikali na Taasisi zilizoidhinishwa hufuata taratibu za kisheria ambazo zinalinda haki za wakopaji na kuhakikisha wanapata huduma za kifedha kwa masharti nafuu.
“Mikopo rasmi kutoka serikalini ina masharti nafuu, riba ya chini, na inalenga kuwawezesha wananchi kuboresha maisha yao bila kuingia kwenye matatizo ya kifedha”, alisema Bw. Shekidele.
Alifafanua kuwa ni muhimu kwa wananchi kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu masharti ya mikopo wanayochukua ili kuhakikisha wanakopa kwa uangalifu na kulipa kwa wakati bila kuingia katika changamoto zisizo za lazima.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha, Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Bw. Jacob Nkungu, aliwashauri watoa huduma za fedha kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi bila kuwakandamiza.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha mkazi wa Sengerema, Bw. Boniface Maxmilian, alishauri elimu ya fedha ifike kwa wananchi wote katika ngazi zote ili waweze kuwa na uelewa mpana wa masuala ya fedha ikiwemo kufahamu mikopo salama, kuwa na uelewa wa masuala ya bajeti na kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha.
Naye Afisa Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Santley Kibakaya, alisema kuwa baada ya kutoa mafunzo ya elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali wananchi watabadilisha utaratibu wa maisha, ikiwemo kuacha kukopa kwenye Taasisi ambazo sio rasmi, kuwashirikisha wenza wao kabla ya kuchukua mikopo na kutotumia mali za fam
29/03/2025
Waziri wa Madini na Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde ameshiriki uzinduzi wa ujenzi wa visima vya maji nchini ili kusaidia kuwezesha kilimo cha umwagiliaji .
Uzinduzi huo ulioongozwa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi .Rosemary Senyamule umefanyika hii leo katika kata ya matumbulu Mkoani hapa ikiwa ni mojawapo ya maeneo yaliyopo ndani ya mradi ambapo visima 68,000 vinatarajiwa kuchimbwa nchi nzima.
Aidha Mavunde ametoa pongezi kwa Waziri wa kilimo na Tume ya umwagiliaji kwa jitihada walizozionesha katika kuwasaidia wakulima wa zabibu mkoani hapa kuondokana na kazia ya ukosefu wa maji katika mashamba yao .
"Yote haya yanafanyika hapa lengo likiwa ni kuhakikisha mkulima wa zabibu anapata soko la uhakika ,natamani kumuona mkulima wa zabibu kawa na maringo na zabibu yake "alisema Waziri Mavunde .
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Arusha