Nct arusha
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Nct arusha, College & University, Sakina, Arusha.
30/01/2024
CHUO CHA TAIFA CHA UTALII CHAZIDI KUNG'ARA KATIKA UTOAJI MAFUNZO KWA VITENDO .
Chuo cha Taifa cha Utalii NCT kimefanya mafunzo jumuishi kwa vitendo kwa wanafunzi wa Idara zote za Chuo, Wanafunzi wa Uratibu Matukio, Ukarimu ikiwa ni pamoja na Mapishi na Uokaji katika Makao Makuu ya Chuo hicho posta jijini Dar es salaam.
“Chuo cha Taifa cha Utalii ni Kitalu kizuri katika swala nzima la kuboresha na kuongeza thamani katika Sekta nzima ya Utalii hapa nchini ,hivyo naomba kutoa rai kwa watanzania wote hususani kwa wazazi wawalete Watoto wao katika Chuo chetu ilikuweza kuendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia na maboresho ya utoaji huduma katika Sekta hii adhimu.
NCT inatoa wataalamu waliobobea katika fani ya Utalii na Usafirishaji,Uratibu wa Matukio,Mapishi,Udobi na Usafi wa nyumba halikadhalika Ukarimu.
Fani hizi zote zinatolewa katika ngazi ya cheti na diploma.-amesema Mh. Angellah Kairuki (Mb),Waziri wa Maliasili na Utalii alipotembelea kujionea namna wanafunzi wanavyonolewa kwa vitendo.
Meneja Taaluma wa Chuo hicho Marry Maduhu, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanafunzi hao na kuwapa uelewa mpana ili kuendeleza walichojifunza Darasani.
"Katika Muhula mzima, kila Idara imekuwa ikifanya mafunzo kwa vitendo kwa namna yake, lakini tunapohitimisha tunafanya kwa pamoja ili wanafunzi wajifunze kufanya kazi k**a timu wawapo kazini" amesema Maduhu.
Amesema kuwa taaluma waliyoipata chuoni hapo itakwenda kuongeza tiza katika mnyororo mzima wa thamani katika utoaji wa huduma bora katika maeneo mbalimbali, ikiwemo sekta ya Utalii ambayo imeendelea kukua hapa nchini.
"Chuo chetu kipo katika kumuunga mkono Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake, katika kuhakikisha sekta ya Utalii inazidi kuimarika, na watalii wanaongezeka hadi kufikia milioni tano ifikapo mwaka 2025"
"Katika kuhakikisha hilo tunashirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Kutoka katika Sekta ya hoteli kusimamia mafunzo hayo ili kuwaongezea ujuzi wanafunzi hao" amesema Mad
08/03/2023
KHERI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, “UBUNIFU NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA, CHACHU KATIKA USAWA WA KIJINSIA”.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Address
Sakina
Arusha