dr_jupiter_
HEALTHY DIET
18/09/2020
UNAMFAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA CANCER AU SARATANI #
Kansa ni ugonjwa unaotokea baada ya kuharibika pia kubadilika kwa seli na kuanza kuzaliana katika mili nazo huitwa seli za kansa, Kansa hutokea kwa binadamu, wanyama na viumbe hai wengine. Seli huharibika,hurekebishika au kufa, ila seli zisipokufa au zisipo rekebishika huwa seli zisizo za kikawaida (hazihitajiki mwilini) ndipo huanza kuzaliana na kuwa seli za kansa. Seli za kansa hutumia seli za kawaida kuzaliana, kusafiri kwa kutumia damu na lymph. Seli za kansa huzaliana na kuhama tokea upande mmoja wa mwili kwenda mwingine hii hali huitwa metastasis
Kansa ni ugonjwa unaouwa kwa kiasi kikubwa duniani, idadi ya watu millioni 8.2 walikufa (Ikiwa ni asilimia 22% ya vifo vyote; Hizi ni taarifa kutoka Shirika la Afya duniani (World Health Organization,2016)). Na ikikadiriwa kufika mwaka 2030 idadi ya vifo kuwa million 13.1. Aina ya kansa zinazoongoza kuua kila mwaka ni pamoja na kansa ya mapafu, kansa ya tumbo, kansa ya ini, kansa ya utumbo, kansa ya matiti
AINA ZA KANSA
Kuna aina zaidi ya 100 za kansa,
Aina za kansa na idadi ya Vifo iliyofanyika na Taasisi ya kansa duniani (National Cancer Institute 2016)
Aina ya Kansa Makadirio ya Vifo Mapya Makadirio ya Vifo 2016
Kibofu 76,960 16,390
Matiti/Kifua (Female — Male) 246,660 — 2,600 40,450 — 440
Utumbo mdogo 134,490 49,190
Endometriamu (Kizazi) 60,050 10,470
Kibofu 62,700 14,240
Leukemia (Aina zote) 60,140 24,400
Mapafu 224,390 158,080
Ngozi (Melanoma) 76,380 10,130
Damu (Lymphoma) 72,580 20,150
Kongosho (Pancreatic) 53,070 41,780
Tezi Kibofu (Prostate) 180,890 26,120
Dundumio (Thyroid) 64,300 1,980
CHANZO CHA UGONJWA WA KANSA
Kuna vyanzo vingi vya ugonjwa wa kansa, viashiria vinavyoweza kuharibu seli na kujiunda mwilini kwa kasi huweza sababishwa na mazingira pamoja na mitindo ya maisha, hivyo vyanzo ni pamoja na;
Kemikali au Sumu kuingia mwilini: Huingia kwa mifumo tofauti k**a chakula, hewa, vimiminika. Kemikali zenyewe ni k**a Benzene, asbestos,
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Arusha