Maasai Channel

Maasai Channel

Share

๐— ๐—ฎ๐—ฎ๐˜€๐—ฎ๐—ถ ๐—–๐—ต๐—ฎ๐—ป๐—ป๐—ฒ๐—น
๐‘ป๐’†๐’๐’†๐’ƒ๐’ ๐‘ด๐’‚๐’•๐’†๐’”๐’‰๐’†๐’• ๐‘ถ๐’๐’๐’”๐’‰๐’ ๐‘ณ๐’‚๐’๐’ˆ

Photos from Maasai Channel's post 05/06/2026

"Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Longido, Papaa Nakuta, amewasihi Wakristo kumtegemea Mungu katika kila jambo, huku akishuhudia kuwa yeye mwenyewe amepata nafasi hiyo ya uenyekiti kwa kumtegemea Mungu pekee. Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa Semina na Mkutano wa Neno la Mungu katika Kata ya Mundarara, ambapo yeye na marafiki zake wamechangia zaidi ya Shilingi Milioni Mbili, ng'ombe mmoja, na mbuzi wanne."

"Semina hiyo ya kiroho inafanyika katika Kanisa la Free Pentecostal Church Tanzania (FPCT) lililopo Kata ya Mundarara wilayani Longido.

โ€‹Akizungumza kwa hisia mbele ya waumini na watumishi wa Mungu, Mwenyekiti Papaa Nakuta amewashukuru viongozi hao wa dini kwa kumpa heshima na nafasi ya kipekee ya kufungua semina hiyo kubwa.
โ€‹Katika hotuba yake, Papaa Nakuta ametumia nafasi hiyo kutoa ujumbe mzito wa kiimani kwa kuwasihi Wakristo kusimama imara na kumtegemea Mungu kwa kila jambo. Ameshuhudia wazi kuwa, mafanikio yake na nafasi ya Uenyekiti wa CCM Wilaya anayoishikilia hivi sasa, ni matokeo ya kumtegemea Mungu pekee na si kwa nguvu za kibinadamu.

โ€‹Katika kuunga mkono huduma hiyo kwa vitendo, Mwenyekiti huyo akishirikiana na marafiki alioambatana nao, wametoa mchango wa fedha taslimu na wanyama hao kwa ajili ya kugharamia semina. Ametumia fursa hiyo kuwashukuru kwa dhati marafiki zake kwa kukubali kuambatana naye na kuonyesha moyo mkubwa wa kusupport kazi ya Mungu.

โ€‹Kuhitimisha hotuba yake, Mwenyekiti Papaa Nakuta amewasilisha salamu za viongozi wakuu wa wilaya hiyo. Amewafikishia waumini hao salamu za upendo kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Longido ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Lemomo Kiruswa, pamoja na salamu kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Longido, Ndugu Salum Kalli, zikionyesha jinsi viongozi hao wanavyojali na kushirikiana karibu na jamii ya Mundarara."

โ€‹"Ushuhuda na mchango huo wa viongozi unazidi kuonyesha umuhimu wa mshikamano kati ya viongozi wa kijamii na taasisi za kidini katika kujenga jamii yenye maadili na maendeleo wilayani Longido.

29/05/2026

OSIRWA SAPUK๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

Want your business to be the top-listed Media Company in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address


Longido
Arusha
23501