AFro-feeds

AFro-feeds

Share

Afro-feeds Tunatoa huduma za mifugo pamoja na kutoa Mafunzo ya ujasiliamali na ushauri wa biashara kilimo mifugo Tanzania

10/07/2025

UGONJWA UKITOKEA, MFUGAJI HUJUA KIWANGO CHAKE CHA MAARIFA

“Wengine huogopa kuku wao wakiugua – wengine huongeza uelewa kila tatizo linapotokea.”

CHUKUA HATUA HII LEO:

1. Tengeneza ratiba ya chanjo ya kuku wako – na uifuate kwa ukamilifu.

2. Weka dawa muhimu za dharura – k**a Antistress, Coccidiostat, Glucose.

3. Uliza, jifunze na andika kila ugonjwa utakaokutana nao – si mara zote utampata mtaalamu haraka.

📌 Ugonjwa hauachi taarifa – bali hutoa somo la dhati kwa mfugaji mwenye malengo.

Photos from AFro-feeds's post 07/07/2025
15/06/2025

Njia sahihi za kutumia dawa za kuua kupe (acaricides) kwenye mifugo.

Tunalenga kupunguza pengo lililopo kati ya maarifa, mitazamo na vitendo vya wafugaji kuhusu udhibiti wa kupe.

📌 Kumbuka:
🔴 Magonjwa yanayosababishwa na kupe bado yanaongoza kwa kuleta hasara kubwa kwenye mashamba ya ng’ombe nchini.

💡 Kwa hiyo, matumizi sahihi ya dawa ya kuua kupe yanaweza kupunguza hadi 70% ya gharama zinazotumika kudhibiti magonjwa ya kupe k**a East Coast Fever, Anaplasmosis n.k.

🟢 Fuga kibiashara, tenga muda wa kujifunza — Afya ya mifugo ni msingi wa faida yako!

Want your practice to be the top-listed Clinic in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Arusha
0000