Arusha One Fm 101.7

Arusha One Fm 101.7

Share

Arusha one Fm Redio Ni moja ya redio bora kabisa kutokea kaskazini mwa Tanzania, huku ikiwa inapatikana katika mikoa Ya Tanga, Kilimanjaro, Singida na Arusha

03/06/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amesema ziara yake ya siku tatu nchini Urusi ina umuhimu mkubwa kwa Tanzania na itaimarisha ushirikiano na Taifa hilo.

Dkt Samia ameeleza hayo leo Jumatano Juni 3, 2026 katika Ikulu ya Kremlin muda mfupi baada ya kukaribishwa na mwenyeji wake, Rais Vladimir Putin. Pamoja na mambo mengi ziara ya kiongozi jhuyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi baina ya mataifa hayo mawili.

Kwenye mazungumzo yake na Rais Putin, Dkt Samia amesema ziara k**a hiyo ya kitaifa mara ya mwisho ilifanywa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1969.

“Ni historia kwangu mimi kuja Urusi kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo kwa ajili ya Watanzania. Kwa niaba yangu na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nawasilisha salamu zao za upendo kwa mwaliko huu.”

‘Nataka tujadiliane kuhusu masuala mbalimbali, lakini kabla ya kuendelea mbele ningeipenda kuishukuru Urusi kwa mchango wake wa harakati za kupigania uhuru wa Afrika”

Dkt Samia aliwasili jjini Moscow Juni 2,2026 kufuatia mwaliko wa Rais Putin ambapo akiwa nchini humo, anatarajiwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Peoples’ Friendship.

Want your business to be the top-listed Media Company in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address


Arusha