KINGDOM MindSet INTERNATIONAL
We exist to influence change in people’s mindsets and inspire full utilization of one's potential to positively impact their communities. Areas of Interest:
1.
16/03/2016
Wise words from Brother Nick
25/12/2015
“Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa KIFALME utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake…”,
MSHAURI WA AJABU: Nimuoe au niolewe na nani, nisomee fani gani, nifanye biashara ya namna gani ili nipate faida, nifanye huduma gani, nifanyeje ili niweze kufanikiwa katika maisha, niishi wapi na mambo yote yanayokuacha njia panda; yapatie muelekeo kwake.
MUNGU MWENYE NGUVU: Ukimwi una nguvu, saratani ina nguvu, wachawi wana nguvu, matajiri wana nguvu, roho ya umasikini ina nguvu, laana za ukoo zina nguvu, hata dhambi ulizowahi kutenda hapo kabla zina nguvu, lakini ipo NGUVU ipatikanayo katika jina lake pekee ambayo inaweza kunyamazisha nguvu nyingine zote na kukufanya kiumbe kipya.
BABA WA MILELE: Umekuwa mpweke maishani, umekosa mahitaji yako ya msingi, umeitwa yatima, umeitwa mjane, umekosa ulinzi na upendo, huna nguzo ya kushikilia maishani; yeye yupo kwa ajili yako leo na hata milele kwa kila hitaji ulilo nalo.
MFALME WA AMANI: Je ndoa yako ina mgogoro, biashara na kazi yako vipo mashakani, maisha yako yamejaa taabu na masumbufu, masomo yako yapo kwenye mgogoro, familia yako inasambaratika, afya yako ipo kwenye mgogoro; mfalme wa amani amekuja, mruhusu atawale na kusema shalom kwako.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Contact the business
Telephone
Website
Address
P. O. Box 523
Arusha