Epak Capital
Our Goal is to Build a Fortress Investment Company That Creates 5X to 10X+ Investment Returns to Investors in Mid and Long Terms.
25/07/2024
HADI KUFANIKIWA, UTAFELI MARA NYINGI - KUFELI NI ISHARA KUWA UNAJIFUNZA NA UNAJARIBU MAMBO MAPYA.
Masomo 10 kutoka kwenye kitabu, "Jinsi ya Kufeli Kwenye Karibu Kila Kitu na Bado Uibuke Mshindi: Hii ni K**a Simulizi ya Maisha Yangu" ("How to Fail at Almost Everything and Still Win Big: Kind of the Story of My Life") cha Scott Adams, ambaye anatufundisha namna inayotekelezeka ya kutumia kufeli kuelekea kwenye mafanikio.
1. Jali Kujenga Mifumo Zaidi ya Malengo(Systems Over Goals): Weka fokasi yako kwenye kujenga mifumo badala ya kuweka malengo. Mifumo ni michakato inayoendelea inayokuongezea uwezekano wa kufanikiwa, wakati malengo ni shabaha mahususi ambayo yanaweza kupelekea kutofurahisha yanapofikiwa.
2. Weka Kipaumbele Kwenye Jinsi Unavyojisikia na Nguvu Yako (Prioritize Your Energy): Tawala nguvu yako kuliko muda. Weka fokasi yako kwenye mambo na majukumu yanayokuongezea nguvu na achana na yale yanayokunyonya nguvu.
3. Jifunze Kutokana na kufeli(Learn From Failure): Kumbatia kufeli k**a fursa ya kujifunza. Kila kufeli huwa na masomo yanayoweza kukuongoza hadi kwenye mafanikio.
4. Jijengee Maarifa(Skill Stacking): Jiendeleze hadi uwe na seti za mbalimbali za maarifa. Kuunganisha maarifa ya kawaida katika maeneo mbalimbali kunaweza kukufanya uwe na thamani kubwa na mwenye mafanikio kuli kuwa na maarifa makubwa kwenye eneo moja pekee.
5. Kukiri(Affirmations): Tumia njia ya kukiri mambo chanya juu yako na yale unayoyataka ili kuprogramu akili yako kubwa kwaajili ya mafanikio. Kurudia kauli chanya kunaweza kukufanya ufokasi kwenye malengo yako.
6. Mfumo wa Maisha Unaojali Afya Njema(Healthy Lifestyle): Jenga mfumo wa maisha unaojali afya njema unaojumuisha kufanya mazoezi ya mara kwa mara, mlo kamili na kulala vya kutosha. Afya njema hukuwezesha kuwa na nguvu, ubunifu na uzalishaji.
7. Badililika na Hali na Mazingira (Adaptability): Kuwa tayari kubadilika na hali na mazingira, badilika namna unavyofanya mambo pale ambapo hupati matokeo. Kuwa mwepesi ni ufunguo wa kushinda vikwazo na kupata njia mpya za kufikia mafanikio.
8. Weka Mkazo Kwenye Miradi yako Binafsi (Focus on Personal Projects): Jishughulishe kwenye miradi yako binafsi ambayo inakuvutia na inayoendana na uimara wako. Miradi ambayo mtu anaipenda inaweza kupelekea kwenye fursa na mafanikio.
9. Kumbati Utofauti Wako(Embrace Your Weirdness): Tumia uwezo wako wa kipekee na mitazamo yako. Kuwa mkweli na halisi kunaweza kukutofautisha na kuvutia mafanikio.
10. Kuhusiana na watu na kujenga mahusiano (Networking and Relationships): Jenga na kuwa na mtandao imara wa mahusiano. Mahusiano yanaweza kukufungulia milango ya fursa mbalimbali na kukupatia msaada pale unapohitaji.
Masomo haya yanasisitiza umuhimu wa kuwa mstahimilivu, kuendelea kujifunza, na kuwa na mkakati wa kukua k**a mtu binafsi na mweledi.
Asante kwa kusoma na kushea 🙏🙏🙏
22/07/2024
Utafikia yale unayoamini, yale unayoyasema, unayoyafikiri, unayojisikia(yanayokusisimua), unayoyatarajia, na unayoyafanya mara kwa mara.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
NSSF Mafao House, 7th Floor , Old Moshi-Arusha Road
Arusha
Opening Hours
| Monday | 08:00 - 17:00 |