Mr Meshacking
MUNGU NI MWEMA
(GOD IS GOOD)
13/06/2026
ya kutisha iliyowaacha hoi polisi.
Huko Cambridge, Massachusetts Marekani, mwaka 1969, kulitokea tukio lililobaki kuwa moja ya mafumbo yasiyo na majibu hadi leo.
Kwenye barabara tulivu ya Brattle Street, watu walianza kumuona mtu wa ajabu mwanaume aliyekuwa amevaa suti ya kawaida nyeusi, lakini uso wake haukuonekana kabisa.
Alikuwa amevaa mask ya plasta nyeupe, iliyofunika uso mzima isipokuwa macho na mdomo.
Alikuwa akija, akinunua vitu vidogo k**a aspirini au bandeji, analipa cash, kisha anaondoka kimya kimya.
Wafanyakazi wa duka la dawa la Star Pharmacy walishangaa, lakini wakaanza kumzoea… au walidhani hivyo.
Watu wakaanza kumuita jina moja tu:
“The Plaster Man” — Mtu wa Mask ya Plasta
Lakini hofu ilianza kukua.
Maana Kila wiki alikuwa anarudi.
Mask ile ile.
Kimya kile kile.
Tabia ile ile isiyoelezeka.
Baadhi ya watu walisema alikuwa mgonjwa anayeficha uso wake.
Wengine wakasema ni mhalifu anayejificha.
Lakini kuna waliodai kitu cha kutisha zaidi kwamba hakuwa mtu wa kawaida kabisa.
Kisha mambo yakaanza kubadilika.
Februari 28, 1969, mwanamke mmoja aitwaye Ellen Grayson alidai alimwona Plaster Man akiingia kwenye nyumba ya zamani iliyotelekezwa.
Nyumba hiyo ilijulikana k**a “nyumba ya laana” pale mtaani hakuna aliyethubutu kuikaribia.
Ellen alipojaribu kusogea karibu… alisikia hatua za haraka ndani ya nyumba, Kisha kimya kikuu.
Hakuna aliyethubutu kuingia tena siku hiyo.
Machi 3, 1969, polisi walipokea taarifa ya harufu mbaya kutoka kwenye nyumba hiyo.
Walipoingia ndani, waliganda.
Ndani ya chumba kulikuwa na mwili wa mwanaume amekaa kwenye kiti, akiwa amevaa mask ya plasta ile ile.
Lakini alikuwa amekufa.
Hakuna damu. Hakuna jeraha.
Karibu naye kulikuwa na chupa ya aspirini na karatasi ndogo iliyoandikwa kwa mkono:
“I’m done.”
Uchunguzi ukaanza, lakini kila kitu kikawa kisichoeleweka:
Mask ilikuwa imetengenezwa kwa mikono, na ilimkaa uso k**a ilitengenezwa kwa ajili yake pekee
Hakuna alama za vidole zililingana na mtu yeyote
Hakukuwa na kitambulisho
Sababu ya kifo: sumu isiyojulikana
Gazeti lililopatikana karibu naye lilionyesha habari za ajali ndogo wiki moja kabla lakini hakuna uhusiano uliopatikana.
Polisi walipojaribu kumtambua, hakuna aliyejitokeza.
Picha yake ilichapishwa magazetini kimya.
Hakuna aliyejua alikuwa nani.
Baada ya miezi, alizikwa k**a:
“John Doe – Mtu Asiyejulikana”
Baada ya tukio hilo, minong’ono ilienea mtaani k**a unavyojua midomo hailali na njaa.
Alikuwa jasusi wa Vita Baridi aliyeshindwa
Alikuwa mtu mwenye ugonjwa wa akili uliomfanya ajifiche
Au alikuwa mtu aliyekimbia maisha yake mwenyewe… hadi akayamaliza kimya kimya
Nyumba hiyo ya Brattle Street ilibomolewa miaka ya 1970…
lakini watu wa Cambridge bado wanadai kwamba usiku wa giza, kivuli cha mtu mwenye mask nyeupe huonekana barabarani.
Hadithi ya The Plaster Man imebaki kuwa mojawapo ya mafumbo ya kutisha zaidi ya Marekani kisa cha mtu aliyekuja kimya… akaishi kimya… na kufa bila kujulikana.
Just a boy From chamangi.The man in plaster mask; hadithi ya kutisha iliyowaacha hoi polisi.
Follow me Mr Meshacking
13/06/2026
ALIKUWA MWAMINIFU SANA KWA MWANAMKE.
mwanamke huyo anaweza kuondoka kwenda mizunguko yake kisha anamuacha mtoto nyumbani huku mbwa huyo mpole, mtiifu, na mnyenyekevu akimlinda mtoto na kucheza nae na mwanamke huyo anaporudi anakuta mtoto kalala usingizi mzito pamoja na mbwa huyo.
Siku moja mwanamke alienda sokoni na k**a kawaida yake akamuacha mtoto pamoja na mbwa.
Aliporudi, aligundua kuna jambo la kutisha sana, vitu vilikuwa vimevurugika ndani hatari, mbaya zaidi mtoto hakuwa kwenye kitanda chake cha kubembea. Damu zilikuwa zimetapakaa kwenye kitanda cha mtoto na kwenye kabati yaani kwa ufupi chumba kizima kilikuwa na damu.
Mwanamke huyo alianza kumtafuta mtoto chumbani humo kila kona, Ghafla mbwa huyo akajitokeza kutoka chini ya kitanda akijilamba ulimi na akitikisa mkia na kichwa k**a umbwa alietoka kula msosi wa hatari.
Moja kwa moja mama huyo akafikiria kuwa mbwa atakuwa k**aliza kumla mtoto wake, akachukua ukuni mkubwa akampiga kipigo cha adabu mbwa huyo mpaka akamuua.
Kisha aliendelea kumtafuta mtoto wake huku akiwaza kuwa hata akipata kiungo kimoja cha mtoto wake itakuwa afadhari tu.
Ghafla tena chini ya kitanda humohumo akamuona mtoto wake akiwa salama kabisa bila kovu lolote huku akiwa na tabasamu,
Kwa hofu kubwa tena akaona nyoka wawili wakubwaaa wakiwa wanavuja damu huku vichwa vyao vikiwa vimetengana na miili. Ilikuwa ni vita kubwa kati ya nyoka hao na mbwa, na yote haya mbwa alifanya ili kuhakikisha usalama wa mtoto.
Lakini tayari kutokana na kutokuwa mvumilivu pamoja na kuwa na hasira za haraka akawa amemuua mbwa mwaminifu, mpole, mnyeyekevu.
--------------
Ni mara ngapi tunawahukumu watu kwa maneno mabaya na kuwatendea vitendo vya uovu bila kuchukua mda na kufanya tathimini????
Kwako wewe unaesoma post hii, Naomba Mungu akusamehe kwa neema yake kutokana na makosa ambayo unafanya bila kujua ama kufikiria lakini bado anakupenda na unazidi kupata neema ya uhai. Mungu atubariki.
Toa maoni yako umejifunza nini? Usisahau kuni follow Mr Meshacking
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Telephone
Website
Address
Arusha