Radio5tz
Radio 5 is one of Tanzania's most popular Swahili speaking radio station, broadcasting news and entertainment
26/05/2026
Eid Al Adha njema!
Na Semio Sonyo – Radio 5
Klabu ya Arsenal hatimaye imetangazwa mabingwa wa Ligi Kuu England baada ya kusubiri kwa miaka 22, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa mwisho wa msimu uliochezwa Uwanja wa Selhurst Park.
Baada ya Manchester City kupoteza dhidi ya Aston Villa, Arsenal walithibitisha ubingwa huo na kumaliza msimu wakiwa kileleni kwa tofauti ya pointi saba. Nahodha Martin Ødegaard aliliinua kombe hilo mbele ya mashabiki waliokuwa katika shamrashamra kubwa, huku kocha Mikel Arteta akiongoza sherehe za kihistoria.
Ubingwa huo ni wa kwanza kwa Arsenal tangu mwaka 2004, ukiwa ni mafanikio makubwa kwa Arteta na kikosi chake baada ya miaka mingi ya changamoto na presha ya ushindani.
Mbali na kutwaa ubingwa, Arsenal pia wameweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza katika historia ya Premier League kumaliza msimu bila kuruhusu penalti wala kupata kadi nyekundu.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Website
Address
Njiro Block J
Arusha
P.O.BOX15883