Ps. Emmanuel Cliff
Turning People to Become God's Sons. Galatians 4:7
Hampati Kwa Sababu Hamuombi.
04/06/2026
✍ K**a Alivyoniambia [8]
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Luka 1:38 SRUV
[38] Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu k**a ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Mariamu alijua nini cha kufanya pale ambapo unapewa neno na Mungu; unatakiwa kulipokea kwa imani ili liweze kufanyika maishani mwako. Sio k**a Zakaria alivyodai ishara, unatakiwa kuamini.
Usikubali kuishi kwa kuona, kuangalia mazingira, kuamini yanayonekana, unayoyasikia, unayoyahisi nk; usiishi kwa mwili, ishi kwa imani kwa sababu wewe ni mzao wa Abraham.
Baraka zote za Mungu zinapokelewa kwa imani sio kwa kuona. Huwezi kuona kitu halafu ukasema nina amani, utaaminije kitu kinachoonekana. K**a kitu kinaonekana huhitaji imani, unahitaji macho.
Imani ni kuwa na uhakika wa mambo unayoyatarajia, mambo ambayo huyaoni; ukishaona huwezi kutarajia tena kwa hivyo huhitaji kuamini kitu ambacho unakiona.
Neno linasema kwamba Bwana Yesu alifanyika maskini ili mimi na wewe tuwe matajiri, unatakiwa kuamini kwamba wewe ni tajiri. Usisubiri kuwa tajiri ndipo ukubali, kubali sasa hivi ndipo utaona.
Neno linasema kwamba Bwana Yesu alichukua madhaifu yako na kuyatwaa magonjwa yako. Amini kuwa wewe ni mzima hata k**a unaumwa. Usisubiri upone ndipo ukubali, kubali umepona ndipo utapona.
Siri ipo katika kukubaliana na kile ambacho amesema Mungu pasipo kuangalia k**a tayari kinaonekana au hakionekani. Kubaliana na Neno la Mungu, amini ndivyo lilivyo maishani mwako, kisha litakuwa.
🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Baba Mpendwa Ninakushukuru Kwa Neema Yako, Umenipa Kila Kitu Kabla Hata Sijaomba na Kabla Sijazaliwa Umeshanitendea. Nina Amini Nimepokea Uponyaji na Baraka Inayotajirisha Kwa Jina la Yesu. Amen
🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Mwanzo 28:3-4 SRUV
[3] Na Mungu Mwenyezi, akubariki, akuzidishe, na kukuongeza, ili uwe mtu wa watu wengi. [4] Akupe baraka ya Abrahamu, wewe na uzao wako pamoja nawe, upate kuirithi nchi ya kusafiri kwako, Mungu aliyompa Abrahamu.
✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).
Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.
- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm
- Telegram:
https://t.me/+kVDJ2ssIox84ZmU0
- page:
https://www.facebook.com/aganojipyasociety
- Instagram:
https://www.instagram.com/invites/contact/?i=194gcl43r688e&utm_content=mv6ciwm
- TikTok
https://www.tiktok.com/.emmanuel_cliff?_r=1&_t=ZS-9465dMbTBnY
- X (Twitter):
https://twitter.com/AganoSociety?t=SejAk4faxnqppJI8ppfnOA&s=09
- YouTube:
https://youtube.com/?si=ecWrgqiv5_IgXMM1
03/06/2026
✍ K**a Alivyoniambia [7]
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Luka 1:18, 20 SRUV
[18] Zakaria akamwambia malaika, Nitajuaje neno hilo? Maana mimi ni mzee, na mke wangu ni mkongwe wa siku nyingi.
[20] Na tazama! Utakuwa bubu, usiweze kusema, mpaka siku ile yatakapotukia hayo, kwa sababu hukuyasadiki maneno yangu; nayo yatatimizwa kwa wakati wake.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Sio ajabu kuona mtu anajiuliza kwamba "Mungu atanipaje, ataniponyaje, atawezaje nk;" ni maneno yasiyo ya imani na wetu wengi wanadhani ni sahihi kujiuliza maswali hayo.
Maswali k**a hayo yanaletwa na adui, sio wewe unayewaza hivyo wala sio Mungu, ni shetani kwa sababu anajua akifanikiwa kukupa mawazo hayo atakutoa kwenye imani.
Zakaria alipopewa ahadi na Mungu kupitia Malaika, hakuamini kwamba inawezekana kwa kuangalia uzee aliokuwa anao; alitaka uhakika kuwa Mungu atampa mtoto. Uhakika gani zaidi ya neno la Mungu?
"Na tazama! Utakuwa bubu, usiweze kusema, mpaka siku ile yatakapotukia hayo, kwa sababu hukuyasadiki maneno yangu....."
Malaika amekutokea, anakwambia neno la Mungu, hutaki neno la Mungu unataka uhakika. Kilicho sababisha Zakaria kuwa bubu ni kwa sababu hakuamini, alitafuta ishara ya macho.
Alitaka Mungu afanye jambo mbele ya macho yake ndio aweze kuamini, hakuamini neno la Mungu aliloleta Malaika. Alikuwa bubu ili asizungumze maneno yasiyo ya imani.
Kwa nini kila unachoomba unakosa? Ni kwa sababu unatafuta ushahidi wa macho ili uweze kuamini kwamba ni kweli Mungu atatenda ulichomuomba. Neno linasema;
Rum 8:8 SUV
[8] Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
Waebrania 11:6 BHN
[6] Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu....
Mwili wako unaishi kwa kuona sio kwa imani, Mungu hapendi. Mungu anaishi na kufanya mambo yote kwa imani, k**a wewe unaishi kwa kuona basi unaishi kwa kufuata mwili. Mungu hapendezwi na hilo!
Amua Kuamini, Utampendeza Mungu na Utapata Unachotaka. Amen
🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Ninakataa Kuwa na Mashaka Kuhusu Neno Alilosema Mungu Kuhusu Mimi, Maisha Yangu na Kile Ambacho Mungu Anataka Nifanye. Kwa Jina la Yesu Nimeamua Kuishi Kwa Kushika na Kutenda Neno la Mungu Tu, Nikijua Kuwa Mungu ni Mwaminifu Kulitimiza Kwangu. Amen
🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Mwanzo 26:3 SRUV
[3] Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Abrahamu baba yako.
Mwanzo 26:12-13 BHN
[12] Mwaka huo Isaka alipanda mbegu katika nchi ile, akavuna mara mia zaidi, maana Mwenyezi-Mungu alimbariki, [13] naye akatajirika. Alizidi kupata mali hadi akawa tajiri sana.
✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).
Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.
- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm
- Telegram:
https://t.me/+kVDJ2ssIox84ZmU0
- page:
https://www.facebook.com/aganojipyasociety
- Instagram:
https://www.instagram.com/invites/contact/?i=194gcl43r688e&utm_content=mv6ciwm
- TikTok
https://www.tiktok.com/.emmanuel_cliff?_r=1&_t=ZS-9465dMbTBnY
- X (Twitter):
https://twitter.com/AganoSociety?t=SejAk4faxnqppJI8ppfnOA&s=09
- YouTube:
https://youtube.com/?si=ecWrgqiv5_IgXMM1
01/06/2026
✍ K**a Alivyoniambia [3]
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 1 Wafalme 17:16 SRUV
[16] Lile p**a la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa kinywa cha Eliya.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Kwa nini katika kizazi cha sasa cha Wakristo hatuoni matendo makuu ya Mungu, ni kwa sababu hakuna watu ambao wanataka kumtii Mungu ili aweze kuwatendea maajabu.
Mungu anazungumza na kila mtu katika kila hali, hata k**a kuna namna unapitia hali mbaya ya maisha lakini bado Mungu anaongea na wewe jinsi ya kutoka kwenye tatizo ulilonalo. Tulia utasikia!
Mwanamke mjane na mtoto wake walikuwa katika hali ya kufa kwa njaa, huyu hakuwa mtu wa taifa la Israeli, lakini Mungu alimsikia kilio chake na kumtuma Eliya kwenda kusababisha muujiza kwake.
Ili aweze kupata chakula alichomuomba Mungu, ilibidi akubali kumwamini Mungu kwa chochote atakacho ambiwa. Eliya alimkuta huyu mwanamke akifanya maandalizi ya chakula cha mwisho.
Chakula ambacho angekula cha mwisho, Eliya alimwambia akitoe ili Mungu akitumie kusababisha muujiza wa chakula. Sasa huyu mwanamke alikuwa na machaguo mawili, amuamini Mungu au asiamini.
Kwanza ana njaa ndio maana Eliya alimkuta alikusanya kuni za kwenda kupika, halafu hana chakula kingine tena; sasa aamue kula kisha asipate kingine au kukitoa kisha Mungu amtunze.
Tunajua kwamba alipoamua kutii neno la Mungu, Mungu alikuwa mwaminifu kutenda kile ambacho alikisema kupitia Eliya. Mwanamke mjane, na mtoto wake pamoja na Eliya walikula kwa miaka mitatu.
Tuna neno la Mungu kwenye Biblia zetu, neno zuri la baraka, afya na mafanikio; tunapaswa kuchagua, tuamue kuamini ili Mungu atutendee au tuache tusiamini tuendelee kuteseka.
Jambo moja muhimu kujua ni hili, Mungu ni muaminifu siku zote na hawezi kubadilika. Ukiamua kusimama katika neno alilosema, itakuwa kwako k**a ambavyo amesema. Hallelujah!
🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Nimuamini Mungu Kuliko Mazingira Yangu, Yeye ni Mwaminifu na Atafanya Sawasawa na Neno Lake. Ninadumu Katika Ahadi Siku Zote Mpaka Nione Matendo Ya BWANA Mungu Wangu. Amen
🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
1 Wafalme 17:14 SRUV
[14] Kwa kuwa BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile p**a la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile BWANA atakapoleta mvua juu ya nchi.
Mwanzo 18:10, 13 SRUV
[10] Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.
[13] BWANA akamwambia Abrahamu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee?
✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm
- Telegram:
https://t.me/+kVDJ2ssIox84ZmU0
- page:
https://www.facebook.com/aganojipyasociety
- Instagram:
https://www.instagram.com/invites/contact/?i=194gcl43r688e&utm_content=mv6ciwm
- TikTok
https://www.tiktok.com/.emmanuel_cliff?_r=1&_t=ZS-9465dMbTBnY
- X (Twitter):
https://twitter.com/AganoSociety?t=SejAk4faxnqppJI8ppfnOA&s=09
- YouTube:
https://youtube.com/?si=ecWrgqiv5_IgXMM1
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Arusha
23306