Mwl. Daniel Piniel
Mimi ni Nuru ya ulimwengu ikiwa Nuru ya Kristo imo ndani yangu. Hekima hunena!!
04/03/2026
NI NANI MWENYE AKILI KATI YA WANADAMU?
Ni yule afanyae bidii katika kumtafuta Mungu hasa katika nyakati hizi.
“Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, Aone k**a yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.” Zab. 14:2.
Basi tumtafute BWANA, kwa kuwa ni jambo jema lenye tumaini la waokovu wetu.
“Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;..” Isaya 55:6.
Kumtafuta BWANA ni agizo lenye kuhitaji utii, kwani lina thawabu kwao wamtafutao BWANA.
“Mtafuteni BWANA, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya BWANA.” Sefania 2:3.
“SIKU YA HASIRA YA BWANA INAKUJA”
Tumtafute BWANA ili tupate kuokolewa. Mwenye kufahamu Neno la Mungu na afahamu.
22/11/2023
ALIYEACHA VYOTE NDIYE APEWAYE ZAIDI KATIKA UFALME WA MUNGU
Kuna wakati watu wanaogopa kuacha vitu au watu walio nao ili wapate nafasi kwa ajili ya Mungu. Yawezekana watu hao ni marafiki wa karibu sana, au ndugu, mke au mume na hata nafasi za kazi (vyeo).
Hofu ya kutengana nao ndiyo inayokuwa kifungo cha utumwa wao wasiwe huru kutenda haki, na kusimama katika kusudi la Mungu.
Inawezekana kuna rafiki au ndugu ambaye amekuwa msaada sana, na alionesha upendo wakati wote wa dhiki yako, na hivyo huwezi kutengana naye japo inakupasa utengane naye ili upate kutenda haki na kulitimiza kusudi la Mungu.
Inawezekana pia ni nafasi (cheo) ambayo imekuwa ni mlango wa kupata riziki kwaajili ya maisha, na hivyo huwezi kutengana nayo japo inakupasa ili uweze kutenda haki na kulitimiza kusudi la Mungu.
Ndugu yangu, Neno la Kristo linasema;
“Hakika nawaambia, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au mke, au ndugu, au wazazi, au wana, kwa ajili ya ufalme wa Mungu, asiyepokea zaidi mara nyingi katika zamani hizi, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.” Luka 18:29-30
Ndugu yangu, fahamu kuwa mtu asikiaye Neno la Kristo na kulifanya, huyo ndiye mtu mwenye akili katika ufalme wa Mungu.
Neno la Kristo limeweka wazi kuwa hakuna mtu aliyeacha vyote kwaajili ya Ufalme wa Mungu kisha akapungukiwa katika maisha kwa maana ahadi katika hilo Neno ni kwamba, Mtu huyo aliyeacha vyote atapewa zaidi ya alivyokuwanavyo na kisha kupokea ahadi kuu ya Uzima wa Milele.
Ndugu yangu Uwe hodari katika kutenda yaliyo mapenzi ya Mungu, chagua lile lililo jema lenye ahadi ya Mungu.
Achana na kile ambacho kimekua kufungo chako cha kutokamilika katika Ufalme wa Mungu, ikiwa ni mtu au vitu. Kwa maana Mungu ametoa ahadi ya kuzidishwa zaidi na kisha ahadi ya Uzima wa Milele.
Usiache Mtu au Kitu chochote kikutenge na kusudi la Mungu kwa sababu ya kuogopa kupeteza. Fanya kwaajili ya Utukufu wa Mungu.
Mungu atusaidie.
08/11/2023
ROHO MTAKATIFU NDANI YANGU
“Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
12 Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.”
2 Wakorintho 2:11-12
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the place of worship
Telephone
Website
Address
Arusha
123