Anointing eye
We provide quality photography & videography service at affordable price contact us:
+255 659 97289
31/12/2017
LENARD'S DAY
FUTURE BOSS
21/12/2017
KANUNI 5 ZA KUWEZA KUFANIKIWA
1.JIAMINI: Kabla ya kufanya kitu chochote kile, unatakiwa kujiamini kwa kila unachotaka kukifanya. Kuna mwingine anataka kuwa daktari, lakini kila anapojiangalia, anaona kwamba hawezi kuwa daktari. Ndugu yangu, hata hao madaktari unaowaona, walipanga kuwa madaktari, hivyo wakajiwekea malengo ya kufika hapo walipokuwa. Simama kwa miguu na ujiambie kwamba unaweza kuwa unavyotaka kuwa.
Kuna wengine wanatamani wawe waandishi wazuri wa hadithi. Rafiki yangu, huwezi kuwa mwandishi mzuri k**a hujiamini. Kuna mwingine anaandika hadithi nzuri lakini hataki watu wazione, na hata wakiziona, hataki kusikia maoni yao kwa kuwa hajiamini.
Unapopanga kuwa mtu fulani, usiogope maneno ya watu, watu hao wameumbwa ili wakufanye usonge mbele. Huwezi kusonga mbele pasipo maneno mabaya ya watu, mtu anapokwambia hauwezi kufanya kitu fulani, wewe fanya ili wajue kwamba unaweza kufanya.
Wengine watakuja na kukwambia kwamba huwezi kuwa daktari kwa kuwa katika ukoo wenu hakuna daktari hata mmoja, usivunjike moyo, mwambie k**a hakuna daktari katika ukoo wetu, acha mimi niwe daktari wa kwanza. Unachotakiwa ni kuanza kujiamini tu.
2.USIOGOPE KUSHINDWA: Wengi wamekuwa hawafanikiwa katika maisha yao kwa kuwa wanaogopa kushindwa. Unaweza kuamua kufanya jambo fulani lakini kuna sauti ndani ya moyo wako inakwambia kwamba hautofanikiwa.
Usitake kukubaliana na sauti hiyo, jiambie mwenyewe k**a unaweza. Kuna watu wanatoa mamilioni ya fedha kuanzisha biashara fulani na mwisho wa siku wanafeli, ila wanachokifanya si kuachana nayo, wanajipanga na kuanza upya kisha kufanikiwa.
Rafiki yangu, hautakiwi kuogopa kufeli. Huwezi kuweza kila siku, unaposoma, jua kwamba kuna kufeli, unapofanya biashara jua kwamba kuna kuishiwa. Usitake kuwa mfanyabiashara huku ukijiambia kwamba utafanikiwa sana, kumbuka kwamba kuna wakati mambo huenda kombo.
Wanafunzi wengi wanaojiua ni wale waliofeli na wakati walijipa uhakika kwamba wangefanya vizuri. Mwanafunzi anasoma, anaongoza kwenye kila mtihani shuleni, unapokuja mtihani wa taifa na kufeli, anajiua kwa sababu hakutegemea hilo.
Wewe k**a mwanafunzi, k**a mfanyabiashara, hautakiwi kuweka kila kitu positive (chanya) bali unatakiwa kukumbuka kwamba wakati mwingine kuna negative (hasi)
Kushindwa ni moja ya mchezo, unachotakiwa ni kutokuogopa kwa kile unachotaka kukifanya.
3.USIWASIKILIZE WENGINE: Hili limekuwa tatizo kubwa kwa watu wanaotafuta mafanikio. Wengi wamekuwa wakiwasikiliza watu wengine. Mtu anapanga kufanya kitu fulani, ila anapoambiwa na watu wengine kwamba hatoweza kufanya kwa kuwa wengi walishindwa, naye anaacha.
Ndugu yangu, hatuwezi kufanikiwa kwa kuwasiliza watu wengine. Mtu anakuja na kukwambia kwamba huwezi kuwa bilionea kwa kuwa mtaa wenu haujawahi kutoa bilionea, unatakiwa kuwaambia kwamba k**a hakukuwahi kutoa bilionea, basi mimi nitakuwa wa kwanza.
Unapoamua kufanya kitu, hautakiwi kusikiliza maneno ya watu, wewe fanya, hata k**a wengi watakuja na kusimama kinyume chako, usivunjike moyo, endelea kufanya kile ulichojiwekea moyoni mwako. Maneno ya watu yapo kwa kuwa ndiyo yatakayokufanya kusonga mbele.
Katika hili, nakumbuka hata mimi ilikwishawahi kunitokea, nilipoanza kuandika hadithi, kuna mengi yalizungumzwa kwamba siwezi, nawachosha watu kusoma hadithi zangu. K**a ningekuwa mtu wa kukata tamaa, ningeacha, lakini sikufanya hivyo, niliendelea kusonga mbele na mwisho wa siku kuyaona matunda yake. Usiwasikilize watu wengine wenye maneno ya kukatisha tamaa.
4.USIKATE TAMAA: Katika kutafuta mafanikio kuna mengi yanaweza kutokea. Kuna vitu vingine vinaweza kukukatisha tamaa na kujiona unashindwa kusonga mbele, hautakiwi kusimama, hautakiwi kuishia hapo bali unatakiwa kupandisha soksi na kusonga mbele zaidi.
Hauwezi kupata mafanikio k**a utakuwa mtu wa kukata tamaa, kila bilionea unayemuona alipitia hatua hii, kuna kipindi walikosa fedha, walivunjwa moyo lakini waliendelea zaidi mpaka kufanikiwa wa kuamini kwamba hakuna mafanikio pasipo kuumia.
Kwa siku kuna masaa 24, wanalala kwa masaa 6 na kufanya kazi kwa masaa 18 lakini wewe unalala kwa masaa 8 mpaka 9. Ndugu yangu, kumbuka kwamba huwezi kupanda ngazi huku mikono ikiwa mfukoni.
5.RUDISHA KWA JAMII: Hiki ndicho kitu muhimu kuliko vyote. Tunaishi katika maisha ya kimasikini sana, tunawaona watu wanaoteseka pamoja nasi, tunawaona watu wanaokosa chakula, fedha za matibabu.
Maisha ya kimasikini yametuzunguka kila kona. Rafiki yangu, tunapofanikiwa, tuwakumbuke wale tuliowaacha kule tulipotoka, kuna watoto yatima wanahitaji msaada, kuna wajane wanahitaji vitu kutoka kwetu, kuna wagonjwa na watu mbalimbali wenye matatizo. Tunapofanikiwa, tukumbuke kwamba tunatakiwa kurudisha asilimia kadhaa kwa jamii kwa kile tulichokipata.
Hatuwezi kufilisika kwa kutoa, toka nilipozaliwa mpaka leo hii, sijawahi kusikia mtu fulani amefilisika kwa sababu alisaidia sana watu wenye matatizo. Tunapoamua kutoa, amini kwamba Mungu atakupa maradufu
photo by samson kalemba Anointing eye
02/12/2017
Client: ARAFA
all photos by ANOINTING EYE STUDIOS
cc: Anyalov Steven Mtetemela
22/11/2017
UMENIKAMATA episode - 2 WAKATI - faida za kutumia wakati vizur na hasara za kutumia wakati vibaya. presented by SAMMY MMBAGA (doctor love) operators; RAMADHANI CHECHE, JUMA JUMA, DI...
21/11/2017
watch umenik**ata from AETV with Sammy Mmbaga
UMENIKAMATA episode - 1 Tambua thamani yako .
04/11/2017
"HE HAS TO BE A BOY Trust me " sister Arafa said that
Click here to claim your Sponsored Listing.
Contact the business
Telephone
Address
Arusha