Afyapack01
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Afyapack01, Health/Beauty, Jamhuri, Bukoba.
14/02/2021
Ijue tezi dume kwa lugha rahisi kabisa!
Mnakumbuka enzi hizo utotoni mlikuwa mnashindana kurusha mkojo.. lakini uwezo huo taratibu ukawa una pungua, hatimaye ukapotea kabisa, mpaka sasa hivi pengine ukienda chooni kukojoa lazima usogelee tundu la choo vinginevyo utakojoa chini au utajikojolea.. kilichofanya unashindwa kurusha mkojo k**a ulivyokuwa mtoto ni tezi dume..wanaume wote wanazaliwa na tezi dume.
Utotoni tezi hii inakuwa ndogo ndio maana unaweza kurusha mkojo, kadri unavyokuwa na yenyewe ukubwa wake unaongezeka, kadri inavyokuwa ndivyo inapunguza ukubwa wa njia ya mkojo ndio maana uwezo wa kurusha mkojo unapungua... hadi unapofika ukubwani kuanzia miaka 40 kwa baadhi ya wanaume inakuwa na kuvimba kupitiliza hadi kuziba kabisa tundu la mkojo; hapo sasa ndio utaambiwa una uvimbe wa tezi dume, na kwa baadhi ya watu uvimbe huo unaweza kuwa kansa, hiyo ndio itaitwa kansa ya tezi dume. Tezi dume sio busha yenyewe ipo ndani, chini ya kibofu cha mkojo. Kazi yake kubwa ni kuzalisha majimaji ambayo huwa yanachanganyika na manii wakati mwanaume anapopiga bao, majimaji hayo yanarutubisha na kulinda manii.
Bahati nzuri ni kwamba bado madaktari wanaweza kupima na kujua iwapo uvimbe wako sio kansa au ni kansa kwa kipimo rahisi ambacho sio gharama sana na chenye usahihi mkubwa...kipimo hicho ni Kidole cha daktari.. pia daktari anaweza kuagiza kipimo cha ultrasound, kipimo cha damu au kutoa sampuli kutoa kwenye tezi dume na kwenda kupimwa maabara...! Wanaume msiogope kidole hata hao madaktari wenyewe huwa wanaenda kwa madaktari wenzao kupimwa na hicho hicho kidole, maana waswahili walisema mficha maradhi, kilio humuumbuwa!
Kwa sasa Tanzania unaweza kutibiwa bila kufanyiwa upasuaji .PIGA 0655269265
Share na wakulungwa wengine wajifunze pia!
14/02/2021
BAWASILI(HEMORRHOID)
ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa Damu ya ndani na ya nje ya sehemu ya haja kubwa. Wakati mwingine mishipa hiyo inaweza kupasuka na kuvuja damu chini ya haja kubwa na kusababisha kutoka kinyama au uvimbe sehemu ya haja kubwa. Tatizo hilo huathiri watu wote ila zaidi huathiri watu wazma.
KUNA AINA MBILI ZA BAWASILI
1.BAWASILI YA NDANI
-Ni aina ya Bawasli ambayo hutokea ndani ya mfereji wa hajakubwa na huwa haimbatani na maumivu yoyote yale na watu wengi hushindwa kujua kua wanatatizo hili.
2.BAWASILI YA NJE
Hii hutokea eneo la mwisho la mfereji wa hajakubwa na huwa inaambatana na maumivu makali na kuwasha kwa ngozi eneo la tundu.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Jamhuri
Bukoba