Baajun Health CARE

Baajun Health CARE

Share

Ushauri na huduma za kiafya

01/08/2022

MACHACHE KUHUSU UTUMBO MWEMBAMBA

Kutoka kwenye mfuko wa tumbo, chakula huelekea utumbo mwembamba. Utumbo mwembamba ni mrefu kuliko ogani nyingine yoyote ya njia ya chakula. Chakula huwa ndani ya utumbo mwembamba kwa muda mrefu kuliko sehemu nyingine za njia ya chakula. Katika utumbo mwembamba chakula hukutana na misusumo yenye vimeng’enya ambavyo hutoka kwenye kongosho na utumbo mwembamba. Vimeng’enya hivyo husaidia kuyeyusha chakula.

Utumbo mwembamba umegawanyika katika sehemu mbili, duodenum na ileum.

karibu sanaa... 0757 923300

DUODENUM...

30/07/2022

*LEO TUTAANGALIA MFUMO WA TUMBO*

*MFUMO WA TUMBO*

Mfumo wa tumbo ni wap? ni mahala ambapo Chakula huifadhiwa. Mfuko huo una uwezo wa kupanuka wakati unapopokea chakula na kusinyaa unapokuwa hauna chakula. Chakula huwa katika tumbo mwa muda wa saa tatu hadi nne. Muda huo hutegemea aina ya chakula. Chakula cha kabohaidreti, kwa mfano uji wa [mahindi]], huwa tumboni kwa muda usiozidi saa moja. Chakula cha protini kwa mfano nyama, huweza kukaa tumboni kwa muda wa saa moja au mbili.

Katika mfuko wa tumbo, kuna kuta za tumbo zina tezi (gastric glands) zitoazo misusumo ya gastriki (gastric juice) ambayo huwa na asidi ya haidrokloriki, uteute na kimeng’enya. Vimeng’enya vinavyotolewa tumboni ni pepsinogen, prorennin, rennin.

1. ASIDI YA HAIDROKLORIKI

Asidi ya haidrokloriki (HCl) husaidia kufanya mambo yafuatayo tumboni:

Husaidia kuweka mazingira ya asidi ili vimeng’enya vya tumbo viweze kufanya kazi, vimeng’enya vya tumboni hufanya umeng’enyaji kwa ufanisi katika hali ya uasidi.
Huvunja sukari tata (complex sugar) kuwa sukari rahisi,huua bakteria waliomo katika chakula, huanzisha ufanyaji kazi wa vimeng’enyo vingine katika tumbo. Pepsinogen na prorennin hubadilishwa kutoka katika hali ya awali na kuwa pepsin na rennin kwa mpangilio uliotajwa; hali ambazo hasa ndizo zifanyazo umeng’enyaji.

2.PEPSIN

Pepsin humeng’enya chakula cha protini na kuwa peptides, Pepsin hutolewa katika namna ya pepsinogen. Namna hii haiwezi kufanya mmeng’enyo mpaka itakapokutana na asidi; hivyo kuzuia kumeng’enya seli zinazoitoka katika tezi za tumbo.

3. RENNIN

Rennin hugandisha protini iliyo katika maziwa ili kimeng’enya cha pepsin kiweze kuivunja protini kwenda katika peptides. Kimeng’enya hiki pia hutolewa katika namna ya prorennin, ambacho huhitaji pia asidi ili kiweze kufanya kazi yake. Kimeng’enya hiki hupakitana sana katika matumbo ya mamalia wachanga walio katika kipindi cha kunyonya.

4. UTEUTE

Uteute wa tumbo hulinda kuta za tumbo ili zisikwanguliwe na asidi ya haidrokloriki na pepsin. Bila uteute huu tumbo linaweza kujimeng’enya. Kuna uhusiano wa karibu sana kati ya uteute huu, asidi ya haidrokloriki na ugonjwa wa vidonda vya tumbo (ulcers).

*BASI LEO TUMALIZE NA KAZI ZA TUMBO*

Kwa ufupi kazi za tumbo ni k**a ifuatavyo:

Hutumika k**a sehemu ya kutunzia chakula kwa muda mfupi kabla ya kuendelea umeng’enywaji katika sehemu nyingine za mfumo wa chakula, umeng’enywaji wa chakula cha protini huanzia katika tumbo. Kwa kutumia misuli yake, tumbo husaidia kuchanganya chakula na misusumo ya tumbo, hivyo kuboresha zoezi la umeng’enyaji tumboni.
Usharabiwaji wa maji, alkoholi na baadhi ya vitamini hutokea katika tumbo. Mfuko wa tumbo una misuli ambayo husinyaa na kutanuka mara nyingi, hivyo kwa muda wote chakula kinapokuwa kwenye mfuko huo huchanganywachanganywa. Kitendo hicho, pamoja na athari za misusumo iliyopo kwenye mfuko wa tumbo, husababisha kufanyika kwa tuitumbo (kwa Kiingereza huitwa chyme).

KARIBU KWA MAWASILIANO TUPIGIE SIMU NO
0757 923300.

Want your business to be the top-listed Beauty Salon in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Dar Es Salaam
Dar Es Salaam