Tmcs-cbe

Tmcs-cbe

Share

Tmcs cbe ni umoja wa wanafunzi wakatoliki kutoka chuo Cha Elimu ya Biashara CBE dar es salaam campus

27/04/2022

*MAKANISA MATATU KATIKA KANISA KATOLIKI.*

1. KANISA LA WASAFIRI.

Hawa ni wale walioko duniani, bado wanapita katika milima na mabonde katika safari ya Imani, hawa ni mimi na wewe! Tunahimizwa kutenda mema na kuwa wavumilivu.

Mathayo 5:3-11

3 “Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
4. Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.
5. Heri walio wapole, maana watairithi nchi.
6. Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.
7. Heri walio na huruma, maana watahurumiwa.
8. Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu.
9. Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.
10. Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
11. Heri yenu ninyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu."

2. KANISA LA WALIOKO TOHARANI, (PURGATORIO).

Hawa ni wale waliokufa wakiwa katika tumaini la wokovu, lakini hawakupata nafasi ya utakaso kamili katika ulimwengu, hii ni sehemu wanayopitia kwa ajili ya malipizi,

Nalo Kanisa la wasafiri wanao wajibu wa kuliombea kundi hili.

Zaburi 88,
4.Nimehesabiwa pamoja nao washukao shimoni, nimekuwa k**a mtu asiye na msaada.
10. Wafu je! Utawafanyia miujiza?
Au waliofariki watasimama na kukuhimidi?
(Upatapo nafasi soma Zaburi yote)

2 Wamakabayo 12:38-46

43. Pia alichangisha fedha kutoka kwa watu wake fedha ipatayo drakma elfu mbili, akaipeleka Yerusalemu kwa ajili ya dhabihu ya kuondoa dhambi. Yuda alifanya tendo hilo jema kwa sababu aliamini juu ya ufufuo wa wafu.
44. K**a asingekuwa na imani kwamba; wafu watafufuliwa, ingekuwa ni upumbavu na kazi bure kuwaombea marehemu.
45. Lakini akiwa anatazamia tuzo nzuri waliowekewa waliokufa wakiwa waaminifu kwa Mungu, hilo lilikuwa wazo jema na takatifu. Kwa hiyo Yuda alitolea dhabihu ya upatanisho ili watu wapate kuondolewa dhambi zao.

3. KANISA LA WASHINDI.

Hawa ni wale ambao wapo mbinguni, walioshinda vita ya imani duniani!

Zaburi 16:10
"Maana hatakuachia kuzimu nafsi yangu, wala humwachi mtakatifu wako aone uharibifu"

Mathayo 27;53
"Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu mpaka chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
Makaburi yakafunuka;
Ikainuka miili ya watakatifu waliolala;
Nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.

*NB:*
*Shamba, nyumba unayokaa ni ya marehemu pengine baba, ndugu au mama au ni matokeo ya jitihada ya mtu ambae ameshafariki. Elimu ulionayo ni jitihada za ndugu fulani ambaye pengine hayupo tena. Amani ulionayo ni matokeo ya watu waliopigana, saivi unakàa unachora nne, Dawa unazotumia ni watu walikaa chini wakatengeneza pengine hata hawakuzifaidi, saivi ukiumwa kidogo unaenda dukani/hospitali unapona mara moja. ALAFU MTU ANAKUJA ANAKUAMBIA-HAKUNA KUWAOMBEA MAREHEMU*.

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Address


Dar Es Salaam