Fursa Digital
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Fursa Digital, Digital creator, Dar es salaam, Dar es Salaam.
Kampuni nyingi hazina organization structure.. Inapelekea kupanga mgawanyiko mzuri wa madaraka, majukumu n.k
Mtu mmoja anafanya majukumu mengi na kupelekea kupunguza ufanisi.
Umewahi kukutana na mkuregenzi anafanya kazi mara za uadmin, marketing, sales ?
Umewahi kupewa cheo kikubwa lakini mshahara ukabakia ule ule..
Kuajiri kwa jinsia badala ya uwezo kunaweza kuifanya biashara ikose vipaji bora, mawazo mapya na ukuaji unaohitajika. Timu bora hujengwa kwa uwezo, si jinsia. Je, wewe unaonaje?
Hivi unajau unaweza kuta referee uliyemuweka kwenye CV yako ndio chanzo cha wewe hupati kazi..
Au umefanya interview hadi ya mwisho lakini huitwi
Inawezekana sio interview yako ni huyo referee wako.
Mara ya mwisho kuwasiliana nae ilikuwa lini?
Hizi ndio sababu zinakufanya kuwa invisible kazini.
1. Kuamini kwamba kazi yako itakutambulisha bila kuonesha.
Yes ni kweli kazi nzuri itakutambulisha lakini bila kushare regular update kwa kitu unachofanya au kufanikisha basi impact yako haitoonekana
2. Kutokuchangia kitu wakati wa vikao.. kuna mfanyakazi yeye akiwa kwenye kikao hachangi kitu hivo mawazo yake na mchango wake hauwezi kuonekana.
3. Kutokujenga mahusiano na wafanyakazi wengine au idara nyingine.
K**a unafanya kazi haujengi mahusiano mazuri na idara nyingine hii itakufanya pia kuwa invisible kazini
4. Kutokurekodi mafanikio yako..
Umefanya kazi takribani mwaka lakini ukiulizwa umefanikisha nini ndani ya miezi 6 iliyopita.
Ukikosa jibu basi tambua wewe ni invisible employee.
Hapa tunazungumzia impact yako ionekane kazini na sio kujipendekeza au uchawa.
Thamani yako inajulikana kazini ? Hata ukisema uondoke leo ?
Ukiingia wa mwisho kwenye chumba cha interview mtu wa mwisho
Kuna hasara zifuatazo
1. Panelist wanaweza kuwa wameshachoka hivo wasikuzingatie sana
2. Wanaweza kuwa wameshamchagua mtu wao tayari hasa kutoka kwa yule wa mwanzo aliye set standard.
Ila kuna faida za kuwa wa mwisho pia k**a zifuatazo
Kwanza ingia chumba cha interview ukiwa na Energy kubwa. Epuka kuongea kwa sauti ndogo, low energy.
Pili: tumia mbinu ya STAR METHOD kujibu maswali.
Kwa maana ya SITUATION, TASK, ACTION, REACTION.
Mfano unaweza kujibu hivi:
“Tulikuwa tunachelewa reports kila wiki (Situation), nikapewa jukumu la kurekebisha mfumo (Task), nikaanzisha mfumo mpya (Action), ucheleweshwaji wa report ukashuka kwa 70% (Result).”
Ya tatu: Tumia Impactfull word badala ya kusema nina passion, confidence, sijui mimi ni trustworth
Sema hivi: Mimi naweza kupunguza malalamiko ya wateja kwa asilimia 30%.
Hayo maneno yanaonesha impact sio maneno matupu.
Umewahi kukutana na tukio gani ulipoingia wa mwisho kwenye chumba cha interview ?
Ukifanyiwa interview wa kwanza set standard kiasi kwamba wale candidate wengine wakifanyiwa wanalinganishwa na wewe.
Jinsi ya kuset standard ni kwa kufanya vitu beyond candidate wengine wanavyofanya.
Jifunze changamoto moja kwenye position unayoiyomba kisha leta solutions. N.k
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Dar Es Salaam
Dar Es Salaam