Machinga Tv
𝗛𝗮𝗯𝗮𝗿𝗶 | 𝗘𝗹𝗶𝗺𝘂 | 𝗕𝘂𝗿𝘂𝗱𝗮𝗻𝗶。
Official Machinga Tv page.
13/06/2026
Katika kuendeleza diplomasia ya utamaduni na kuthamini kahawa k**a urithi wa pamoja, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuimarisha urafiki, maelewano na ushirikiano wa kudumu kati ya wananchi wa Tanzania na Jamhuri ya Korea, hatua inayolenga kufungua fursa zaidi za kiuchumi, utalii na biashara kati ya mataifa hayo mawili.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Kahawa la Gongneung Forest Trail 2026 nchini Korea Kusini, Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea, Mheshimiwa Noel Kaganda, amesema kuwa tamasha hilo limekuwa jukwaa muhimu la kuitangaza Tanzania kupitia kahawa yake bora pamoja na urithi wake wa kiutamaduni.
Mheshimiwa Kaganda alieleza kuwa Tanzania huzalisha takribani tani 100,000 za kahawa kila mwaka, huku sekta hiyo ikisaidia maelfu ya wakulima na kuchangia kati ya dola za Marekani milioni 200 hadi 300 katika uchumi wa taifa.
Aidha, alisisitiza kuwa kahawa si zao la biashara pekee, bali ni nyenzo muhimu ya kuimarisha uchumi, kujenga urafiki kati ya mataifa na kukuza ubadilishanaji wa tamaduni huku akiongeza kuwa kupitia zao hilo, Tanzania na Korea zinaendelea kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii.
Mbali na kuitangaza kahawa ya Tanzania, Balozi Kaganda aliwaalika washiriki wa tamasha hilo pamoja na wageni wengine kutoka Korea Kusini kutembelea vivutio vya utalii vya Tanzania, ikiwemo Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na visiwa vya Zanzibar, ambavyo vinatambulika duniani kwa uzuri wake wa kipekee na vivutio vya asili.
Alibainisha kuwa kupitia diplomasia ya utamaduni na matumizi ya kahawa k**a daraja la kuunganisha watu, Tanzania inaendelea kujenga mahusiano imara ya urafiki, maelewano na ushirikiano wa muda mrefu na Jamhuri ya Korea, huku ikifungua milango ya fursa mpya za uwekezaji, biashara na utalii kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.
Kocha wa Dar City ameonyesha kufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake baada ya kuibuka na ushindi mnono wa vikapu 106 kwa 57 dhidi ya Magone katika mchezo wa Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya mchezo huo, kocha huyo alisema timu yake ilicheza kwa nidhamu, ushirikiano na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi jambo lililowezesha kupata matokeo hayo makubwa. Alisisitiza kuwa wachezaji walionyesha kujituma kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo na kutumia vizuri nafasi walizozipata.
Aidha, alieleza kuwa ushindi huo unawapa morali kuelekea michezo ijayo huku akiwataka wachezaji kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kutoridhika na matokeo ya sasa. Dar City ilitawala mchezo katika robo zote na kuonyesha ubora mkubwa wa kushambulia na kujilinda, hali iliyowafanya Magone kushindwa kuhimili kasi yao.
AMINI MKOSA Nahodha wa timu ya Kikapu ya DAR CITY amewapongeza wachezaji wenzake kwa ushirikiano wao mkubwa uliowapa nafasi ya kushinda vikapu 106 kwa vikapu 57 vya timu ya MAGONE katika muendelezo wa ligi ya kikapu ya Dar es Salaam inayochezwa uwanja wa DON BOSCO Upanga Jijini Dar es Salaam.
Upande wa pili Amini Mkosa amegusia ushiriki wao katika mashindano ya kimataifa kuanzia Kenya, Afrika Kusini na Nchini Rwanda katika ligi ya Kikapu Afrika hatua ya nane bora ilivyowapa uzoefu mkubwa ambao umewafanya waweze kupata ushindi katika mechi mbili mfululizo.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Dar Es Salaam