RaiaPost
Raia wenzangu, habari ni msingi wa maendeleo na haki zetu. Tufuatilie Shughuli Zote Zenye Kuleta Maendeleo Kwa Taifa
❤️🇹🇿
25/11/2025
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali haitokuwa na mzaha na Watumishi wa Serikali Wazembe, Wavivu na Wala rushwa na kusema ikithibitika Mtumishi anafanya makosa hayo na kukwamisha utendaji asiishie kuhamishwa tu bali afukuzwe kazi.
Akiongea Jijini Dar es salaaam leo November 25,2025 kwenye mkutano wake na Wahariri wa Vyombo vya Habari, Mwigulu amesema ““Suala la nidhamu kazini hatutokuwa na mzaha nalo, uadilifu hatutokuwa na mzaha nao, bila nidhamu na uadilifu hatutotimiza malengo yaliyopo kwenye dira na Ilani, na nimewaelekeze Watendaji wa Serikali wasiwe na mzaha kwenye hili, na wale Wazembe, Wavivu, Wadokozi, Wala rushwa tutashughulika nao”
“Na nimeelekeza Mtumishi Mzembe na Mla rushwa asihamishwe akibainika na kuthibitika afukuzwe, hatuna uhaba wa Vijana wa kufanya kazi”
“Mh. Rais ameelekeza utaratibu wa kuwasikiliza Watanzania, na hili tumeshaelekeza kote kitakachofuata tutafuatiliana, ni kweli kuna baadhi ya maeneo kunakuwa na ulegevu wa utimizaji wa majukumu ya namna hii”
Credit
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Dar Es Salaam