Denzel Trainer
>OFFICIAL PERSONAL TRAINER OF HON. Jakaya Kikwete
>OFFICIAL PERSONAL TRAINER OF GSM GSM Group Of Companies
mtangulize Mungu katika kila siku ya maisha yako. Anza siku kwa sala, mwombe akupe nguvu, afya na hekima. Pale unapochoka, kumbuka kuwa Mungu hawaachi wale wanaomtumaini. Yeye anaona machozi yako, juhudi zako na ndoto zako.
Usikubali maneno ya kukukatisha tamaa
yakuzuie kusonga mbele. Wewe ni mwenye thamani, una kusudi, na maisha yako yana maana kubwa. Endelea kupambana, endelea kuamini, na endelea kufanya kazi kwa bidii.
Siku moja utatazama nyuma na kujivunia
kwamba hukukata tamaa.
Mungu akutie nguvu, akubariki na akuinue kutoka hatua moja kwenda nyingine. Kaa imara, tumaini lako liwe kwa Mungu, na kamwe usiache kuota makubwa🙏.
Ndugu yangu, usikate tamaa kwa kazi unayoifanya leo. Kila hatua unayopiga ukiokota machupa barabarani ni ishara ya juhudi, ujasiri na heshima ya kutafuta riziki halali. Watu wengi huona machupa tu, lakini Mungu huona moyo wako wa kufanya kazi kwa bidii na kutokata tamaa.
Kumbuka kwamba kila mafanikio makubwa huanza na hatua ndogo. Usidharau mwanzo wako, kwa sababu kesho yako inaweza kuwa kubwa kuliko unavyofikiria leo. Endelea kufanya kazi kwa uaminifu, nidhamu na moyo wa shukrani. Kazi yoyote halali ni ya heshima mbele za Mungu.
😂😂😂😂😂 HAPO KUNA MWISHONI KUNA MUDA MAMA YANGU KANIMAINDI SANAA.
NAOMBA MNIPIGIE KWA HUDUMA YA PERSONAL COACHING #0718942338
😂😂😂😂😂😂 Yaani hapo ukimuangalia tu Sura yake unaona kabisa Mwanafunzi wangu amenimaindi vibaya sana. Ameniambia nikimvunja shingo yake na Mumewe akimuacha yeye ataishi wapi? Au nataka aachike kisa kavunjika shingo? Hahahahahahah nimecheka ujue.
Ninapo ona Mwanafunzi wangu anafurahia namna ambavyo nadili naye basi hata mimi Mwalimu wake huwa nasikia raha sana, maana furaha yake inaashiria ni uzima na baraka kubwa sana kwangu na kwake yeye mwanafunzi wangu.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Telephone
Website
Address
Dar Es Salaam
14121