KITAA RADIO FM
Bodaboda n Bajaj Music Entertainment Swali likaja kwangu nyimbo au video ambazo hazichezwi na ni nzuri
tufanye nazo nini ili na hawa wasanii wapate airtime?
Mkwawa alipigania ardhi yake.
Sisi tunapigania ndoto zetu.
Nyakati zimebadilika, lakini roho ya kutokata tamaa bado ipo. Kila hatua unayopiga kuelekea mafanikio ni sehemu ya urithi huo.
Hii ndiyo maana ya NYALU NATION.
Kwa sababu Mnyalu wa leo habebi mkuki...
Anabeba maono.
ONGEA NA HADHIRA YAKO K**A WATU HALISI, SI NAMBA
1. Unachohitaji ni Mashabiki 1,000 wa Kweli sio follower 1M wasio na msaada
2. Unaweza kuwa na followers 500,000+ lakini bado ukapata streams chini ya 100.
TAFAKARI KWAKINA KIDOGO
Followers si sawa na sapoti. Followers hawahakikishi streams. Followers hawajengi kazi ya muziki.
Kinachousukuma muziki wako mbele ni kuwa na watu wanaojali kwa dhati kile unatengeneza kwaajili yao — watu wanaosikiliza unapotoa kazi mpya, wanaoshare nyimbo zako, wanaokuja kukuunga mkono, na wanaobaki pamoja nawe katika safari yako.
Unachohitaji ni angalau mashabiki 1,000 wa kweli.
Sio watu wanaopita tu kwenye maudhui yako bila kujali, bali watu waliounganishwa kihisia na muziki wako pamoja na safari yako. Hao ndio wanaobadilisha releases zako kuwa mafanikio, posts zako kuwa engagement, na muziki wako kuwa kipato.
Acha kukimbizana na namba. Anza kujenga uhusiano.
1. Ongea na hadhira yako k**a watu halisi, si k**a takwimu.
2. Shiriki simulizi zako kuhusiana na kazi zako ili mashabiki waweze kuunganishwa nawe kihisia.
3. Kuwa thabiti katika kile unachofanya ili watu wasikusahau.
4. Jibu comments na DM ili kujenga mahusiano ya karibu.
5. Wape watu sababu ya kubaki kwako k**a walivyokuja
6. Tengeneza maudhui yanayozunguka muziki wako, si kuzungumzia maisha yako ya faragha.
7. Toa muziki kwa malengo na mpango maalum, si kwa kubahatisha. Kifupi wekeza rasilimali zote unapotaka kutoakazi
8. Jenga jamii (community), si idadi ya followers pekee.
9. Wafanye mashabiki wako wajisikie sehemu ya safari yako.
10. Wazawadie wanaokuunga mkono kwa uaminifu (shout-outs, maudhui maalum, zawadi za kipekee n.k.).
Kumbuka: Mashabiki 1,000 wa kweli wana thamani kubwa kuliko followers 100,000 wasiokujali.
Tulie wote
jaribu uone
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Address
Kijitonyama
Dar Es Salaam
1259