Initiative for Human Life Development
Work as partner to the government in order to meet millennium development goals.
22/09/2020
Taasisi ya IHLD inajipanga kuandaa Maonesho ya Bidhaa za Vikundi ya Wakina Mama Wajasiriamali Wadogo Tabata Segerea.
26/05/2018
Ushirikiano wako ni Faraja kwa Watoto wetu
17/05/2016
MDs' wa IHLD
27/04/2016
Bajeti
Leo nimeona tuzungumze kuhusu bajeti. Hili jambo limekuwa ni gumu sana miongoni mwetu.
Jambo muhimu ni kujua kiasi unachopata kwa mwezi ukitoa kodi zote, kiasi ambacho unatakiwa ukipangie matumizi.
Kwa kawaida yapo matumizi ya aina kuu mbili, haijalishi unafamilia au unaishi mwenyewe na aina hizo ni Matumizi ya Lazima na Matumizi ya Ziada.
Matumizi ya lazima ni kwa mfano:
• Fungu la 10
• Kodi ya nyumba
• Ada za shule
• Chakula
• Mahitaji ya nyumbani mfano; sabuni, mafuta n.k.
• Nauli / mafuta ya gari
• Bili za umeme, maji, msaidizi, mlinzi n.k
• Mawasiliano
• Matibabu
• Akiba
Mahitaji ya ziada ni k**a
• Nguo na viatu
• Michango na zawadi
• Burudani
Tenga kiasi kinachohitajia kwa kila kipengele kwa mwezi. Hakikisha fedha uliyotenga inatosha na usibadili matumizi ya fedha bila sababu ya msingi.
Fedha inayobaki kwa mwezi weka pembeni k**a akiba au unaweza itumia kwa matumizi ya ziada. Mara zote hakikisha umekamilisha matumizi yote ya lazima kabla ya kutumia kwa matumizi ya ziada. Na matumizi ya ziada yanaweza yakawa ni kila baada ya kipindi fulani mfano miezi mitatu hadi sita ili kuweka akiba zaidi kuliko kutumia fedha.
Hakikisha unaifuata bajeti yako k**a ulivyojipangia ili uweze kuona mafanikio.
Mwanzo itakuwa ngumu kidogo ila kadiri unavyojizoeza baadaye itakuwa rahisi sana.
Epuka kununua kitu bila kukipangia bajeti. Tumia pesa yako kwa busara kwa mafanikio yako na familia yako. Pia jitahidi kuwafundisha watoto jinsi ya kutumia fedha kwa uangalifu na kwa bajeti.
Bajeti haimaanishi ianzie kwa wenye uwezo mkubwa hapana, ianzie chini popote pale ili kujikwamua kutoka chini zaidi kwenda juu zaidi kimafanikio
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Dar Es Salaam
255