UTVTZ
Kituo chako cha habari zilizochujwa na kuandaliwa kwa ustadi na umakini.
Ikiwa leo ndio siku ya maziko ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei nchi hiyo na Marekani zimeanza kushambuliana kijeshi baada ya ukiukwaji wa mkataba wa usitishwaji vita uliosainiwa mwezi Juni.
Kutokana na mapigano hayo mtaalamu wa historia na matukio makubwa ya kidunia, Mbwana Alyamtu anatoa tathmini yake iwapo maziko hayo yatakamilika salama.
✍Ibrahimu Kilumbo
Mhariri |
Mama Shamim Khan, ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa mbunge mwaka 1985 na baadaye kuhudumu k**a Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, amesimulia historia ya kuanzishwa kwa banda la wanawake katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba.
Khan anaeleza kuwa baada ya kupata nafasi ya uongozi, aliona umuhimu wa kuwawezesha wanawake wengine kushiriki katika fursa za kiuchumi. Anasema wazo la kuanzisha banda la wanawake katika Maonesho ya Sabasaba lilitokana na dhamira yake ya kuwapa wanawake jukwaa la kuonyesha bidhaa zao, kukuza biashara zao na kujenga uwezo wa kiuchumi.
✍Halima Abdallah
Mhariri | John Mbalamwezi
Mwanaharakati wa kijamii, Shamira Mshangama anasema kuishi kwa kufuata ndoto na malengo yake kumemwezesha kufikia mafanikio mbalimbali. Anaeleza kuwa kutokuwa na hofu ya kufuatilia kile anachokitaka ni moja ya misingi iliyomsaidia kutimiza ndoto zake.
Kwa mujibu wa Shamira, changamoto inayowakabili wasichana wengi ni kutokuwa na maono na malengo yaliyo wazi.
Anasema wengi huishi kwa mazoea na kushindwa kujijengea msingi imara wa kile wanachotaka kufanikisha, hali inayowafanya kukubali kila fursa au mwelekeo unaojitokeza badala ya kufuata malengo yao binafsi.
✍Halima Abdallah
Mhariri | John Mbalamwezi
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Website
Address
Mandela Road
Dar Es Salaam
Opening Hours
| Monday | 09:00 - 17:00 |
| 20:00 - 21:00 | |
| Tuesday | 09:00 - 17:00 |
| 20:00 - 21:00 | |
| Wednesday | 20:00 - 21:00 |
| Thursday | 09:00 - 17:00 |
| 20:00 - 21:00 | |
| Friday | 06:00 - 21:00 |
| Saturday | 20:00 - 21:00 |
| Sunday | 09:00 - 17:00 |