Watetezitv
WATETEZI TV is a Not-For-Profit online Tv under the Tanzania Human Rights Defenders Coalition(THRDC). Watetezi Tv operates in lieu of all applicable laws.
Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Adv. Onesmo Olengurumwa, amesema Tanzania inaingia katika hatua muhimu ya maandalizi ya mapitio ya nne ya Universal Periodic Review (UPR) yanayotarajiwa kufanyika kati ya Oktoba na Novemba mwaka huu, huku akisisitiza umuhimu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kupata taarifa sahihi kuhusu hali ya haki za binadamu nchini.
Olengurumwa ametoa kauli hiyo katika mkutano wa maandalizi kuelekea mapitio ya nne ya UPR, uliozikutanisha baadhi ya asasi za kiraia na wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa pamoja na wadau wa maendeleo, kwa lengo la kujadiliana kuhusu masuala muhimu yanayopaswa kupewa kipaumbele wakati wa mapitio hayo yatakayofanyika Geneva, Uswisi.
Amesema UPR ni utaratibu wa Umoja wa Mataifa ulioanzishwa mwaka 2006 unaozihusisha nchi zote wanachama katika kutathminiana kuhusu utekelezaji wa wajibu wao wa kulinda na kuendeleza haki za binadamu, ambapo nchi huulizana maswali na kutoa mapendekezo ya kuboresha hali ya haki za binadamu.
Akizungumzia utekelezaji wa mapendekezo ya mzunguko uliopita, Olengurumwa amesema Tanzania ilikubali mapendekezo 108, lakini tathmini inaonesha kuwa zaidi ya nusu ya mapendekezo hayo hayakutekelezwa ipasavyo, huku mengine yakitekelezwa kwa kiwango cha sehemu na yaliyotekelezwa kikamilifu yakiwa chini ya asilimia 10.
Amesema UPR ni mchakato unaoweka uwajibikaji wa moja kwa moja kwa kuwa nchi hulazimika kutoa majibu kuhusu utekelezaji wa ahadi ilizozitoa katika mapitio yaliyopita.
Amesema mkutano huo pia unalenga kuhakikisha nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zitakazoshiriki katika mapitio ya Tanzania zinapata taarifa sahihi kuhusu hali halisi ya haki za binadamu nchini, ili ziweze kuuliza maswali yanayozingatia mazingira halisi ya Tanzania na kutoa mapendekezo yanayojibu changamoto zilizopo.
Mkutano huo umewakutanisha wawakilishi kutoka sekta mbalimbali, zikiwemo haki za watoto, wanawake, wafugaji, mazingira, uhuru wa kujieleza na makundi mengine ya watetezi wa haki za binadamu.
Rufaa ya kijana Nasry Lawrence Mkangala, anayetumikia kifungo cha miaka miwili gerezani, imeahirishwa tena baada ya gari la Magereza lililomleta mahak**ani kuondoka kabla shauri lake halijasikilizwa.
Kesi hiyo ilikuwa imepangwa kusikilizwa saa 8:00 mchana, lakini iliitwa saa 10:00 jioni, wakati ambapo tayari gari la Magereza lilikuwa limeondoka na washtakiwa waliokuwa chini ya ulinzi wa Magereza.
Akizungumza nje ya Mahak**a Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam, leo Julai 8, 2026, Wakili Paul Kisabo THRDC THRDC , Mkuu wa Idara ya Utetezi katika Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), alisema hali hiyo ilisababisha rufaa ya Mkangala kushindwa kuendelea kusikilizwa k**a ilivyokuwa imepangwa.
Hata hivyo, Mahak**a ilielekeza kuwa pande zote mbili ziwasilishe hoja zao kwa maandishi ili kurahisisha mwenendo wa rufaa hiyo.
Rufaa hiyo inasikilizwa katika Mahak**a Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam, mbele ya Jaji Elizabeth Mkwizu.
Nasry Mkangala ni miongoni mwa vijana waliok**atwa wakati wa matukio ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, na baadaye kufikishwa katika Mahak**a ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mbalimbali, yakiwemo uhaini, wizi, kuvunja duka na kukutwa na mali zinazodaiwa kuwa za wizi.
Mnamo Machi 18, 2026, Mkangala alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kukutwa na mali zinazodaiwa kuwa za wizi. Kufuatia hukumu hiyo, mawakili wake waliwasilisha rufaa katika Mahak**a Kuu wakipinga uamuzi huo
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
P. O Box 105926
Dar Es Salaam
00225