Real Life In Christ Ministries.
pata mafundisho yatakayo kupa uzima wakimungu na kukuwezesha kugundua na
kupata utajiri na ushindi uliomo katika kristo Yesu Bwana wetu.(yohana 10:10)
03/01/2026
MKOA UNAOPOTEA KIUCHUMI: MBEYA
Mbeya ina potential kubwa, lakini hakuna mkakati wa kuibadilisha kuwa maendeleo halisi. Ardhi rutufu, hali ya hewa nzuri, na lango kuu la biashara kuelekea SADC – vilipaswa kuifanya “Johannesburg ya Tanzania.” Badala yake, mkoa umebaki kuzalisha bidhaa ghafi huku utajiri ukipita mikononi mwa wachache.
Zaidi ya 80% ya wakazi ni wakulima. Mahindi, mpunga, parachichi, maziwa na kahawa zinauzwa ghafi. Viazi na machungwa yanapotea, maziwa yanauzwa ghafi badala ya kuwa yoghurt au cheese, na kahawa inauzwa bila brand. Mini agro-processing hubs, packaging centers, na marketing clusters zinaweza kubadilisha kila kilo kuwa mapato halisi.
Uwanja wa ndege wa Songwe unakosa matumizi ya usafirishaji wa bidhaa. Mbeya ni Gateway to SADC, lakini bidhaa za mkoa zinashindwa kufika Lusaka au Lubumbashi. Dry port na distribution hubs zinaweza kuondoa kizuizi hiki.
Mbeya ina madini k**a mkaa, dhahabu, chokaa na marumaru, lakini uchimbaji mdogo hauungi mkono viwanda. Industrial parks zinazounga mkono value chain zinaweza kuongeza ajira na mapato.
Mkoa haujapata flagship project la kuvutia wawekezaji. Special Economic Zone kwa viwanda vya chakula na madini inaweza kuibua uwekezaji, kuongeza ajira, na kuifanya Mbeya kuwa kitovu cha biashara.
Potential bila mkakati ni gari la kifahari lisilo na mafuta. Ni wakati sasa wa kuigeuza Mbeya kuwa Injini ya Uchumi wa Kusini!
26/12/2025
Self-mastery is the quiet art of ruling oneself in order to live up to one’s full potential.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the place of worship
Website
Address
Dar Es Salaam
Dar Es Salaam
0768027086