UNI_Updates.tz
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from UNI_Updates.tz, Business Center, Dodoma.
11/02/2023
"Ni lengo letu kuwa UDOM iwe salama kwa wote ili kila unapokutana na mwenye uhitaji wa kujifunza, basi unamshauri kuja hapa kwetu kupata elimu bora. Na ile tufike ni muhimu kutambua kuwa kabla ya kuona chochote kwa mtu mwingine,ona kwanza kuwa yeye ni binadamu k**a yeye na mpe heshima anayostahili, si kwa namna alivyo bali kwa sababu tu yeye ni binadamu k**a wewe. Niwasihi sote tushiriki katika kupinga vitendo hivi kwa kuvunja ukimya bila kujali nani anafanya vitendo hivi vibaya" alisema Prof. Lokina.
Kwa kushirikiana na UNESCO,chuo kikuu Cha Dodoma Kimefanya kongamano mahususi lililofanyika hivi leo Kwa lengo la kupinga ukatili wa kijinsia hasa vyuoni. Akifungua Kongamano hilo lililokuwa na kauli mbiu inayosema" MAZINGIRA SALAMA! TOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA VYUONI", prof. Razak Lokina- Naibu Makamu mkuu wa chuo,taaluma,utafiti na ushauri,ame alilishukuru Shirika la UNESCO Kwa kuungana na chuo kikuu Cha Dodoma kupinga ukatili wa kijinsia ili kuhakikisha haki na usawa vinatawala.
Kadhalika,mratibu wa mradi wa UNESCO wa 03 PLUS Kwa upande wa Dodoma Bw. Faraja Msangi aliishukuru menejimenti ya chuo kwa kujidhatiti kuhakikisha ukatili wa kijinsia unapigwa Vita na kutoa elimu ili kudumisha haki na usawa.
11/02/2023
Akiwa ikulu ya DODOMA (Chamwino), Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezungumza na viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya juu(TAHLISO) na Shirika la vyuo vikuu na taasisi ya Elimu ya juu Zanzibar (ZAHLIFE) hivi Leo tarehe 11/02/2023,Kwa lengo la kuinua ubora wa Elimu nchini Tanzania.
Katika kutimiza lengo hilo,Mama Samia Suluhu Hassan ametambua pia changamoto zinazowakumba wanazuoni, ikiwa ni pamoja na pesa ya kujikimu kutokidhi mahitaji yao ya msingi hali inayopelekea wanazuoni hao kujinyima kwenye swala la Kula Kwa kujiwekea bajeti ya aftatu Kwa siku na wengine Kula mlo mmoja Kwa siku.kwa kulitambua hilo Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa agizo kuwa waongezewe pesa ya kujikimu."...unajipanga ule mara moja Kwa siku...sasa, waziri wa Elimu nenda kaangalie. Tutaanza na elfu kumi." Hayo ni maneno ya Mhe. Samia Suluhu Hassan akionesha kuwajali vijana Kwani ndio nguvu ya Taifa.
Kadhalika Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka vijana kujituma ili wawe msaada Kwa jamii katika kuinua maendeleo nchini ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira.
official
10/02/2023
Mchuano huu mkali wa kufunga semista umetarajiwa kufanyika siku ya Kesho terehe 11/02/2023 ukihusisha mechi nne Ambapo mechi zote hizo zitachezwa katika viwanja vya Chuo kikuu cha Dar-es-Salaam (UDSM)kumaanisha kuwa UDSM watakuwa kwenye viwanja vya nyumbani. TMDA VS UDSM itachezwa Ground No.1 kuanzia saa 7:30 AM,CBE na DIT watachuana katika kiwanja cha ground No.2 kuanzia saa 7:30AM ,TRA VS ARU watamenyana ground No.1 kuanzia saa 9:00AM, na bila kuwasahau TRA VS TPA watatoana jasho ground No.2 kuanzia saa 9:00 AM.Hakika kesho ni patashika nguo kuchanika katika viwanja vya UDSM katika mtanange huu mkali. Je Nani ataibuka mshindi kwenye kandanda hili?...kesho itafahamikaaaaaaaa......
10/02/2023
"Wakipata ujuzi huu unawawezesha kupata machapisho kirahisi na kuweza kuyatumia kirahisi katika majukumu yao ya utafiti, kufundisha na kufanya utafiti elekezi", Hayo ni maneno ya Dkt. Grace Msoffe Mkurugenzi wa huduma za maktaba katika chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) ambapo siku ya leo tarehe 10/2/2023,kurugenzi ya huduma za maktaba kwa kushirikiana na jumuiya ya wanataaluma Chuo kikuu cha Dodoma (UDOMASA), wameandaa mafunzo ya siku mbili yanayolenga kuongeza ujuzi kwa wanataaluma katika kutafiti taarifa mbalimbali za machapisho ambazo watatumia katika kufundishia,kufanya utafiti na kutoa ushauri elekezi.
_udom255
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Dodoma