Layers Pro
Tunawasaidia Wafugaji wa kuku Kuongeza Kipato Chao Kupitia Mbinu Bora za usimamizi wa mradi
19/04/2026
Tuna formula tatu katika mpangilio ufuatao na kila formula ina CFP yake
1.Chakula Cha vifaranga/starter mash hii formula inatumika kuchanganya chakula cha vifaranga kuanzia siku 1 mpaka siku 25
Mahindi paraza kilo 52
Soya kavu kilo 32
Mashudu ya alizeti kilo 9
Mafuta/oil kilo 2
CFP ya vifaranga kilo 5
Jumla kilo 100
𝐌𝐀𝐅𝐔𝐓𝐀 𝐘𝐀𝐍𝐀𝐓𝐔𝐌𝐈𝐊𝐀 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐂𝐇𝐀𝐊𝐔𝐋𝐀 𝐂𝐇𝐀 𝐕𝐈𝐅𝐀𝐑𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐓𝐔
2.Formula ya kuku wanaokua hii inatumika kuanzia siku 25 mpaka unapowauza au wanapoanza kutaga/ukiona yai la kwanza
Mahindi paraza kilo 45
Mashudu ya alizeti kilo 15
Pumba za mahindi kilo 25
Soya kavu kilo 10
CFP ya kuku wanaokua kilo 5
Jumla kilo 100
Hapa kwenye kuku wanaokua Kuna formula nyingine yenye pumba nyingi
3.Formula kwa ajili ya kuku chotara wanaotaga
Mahindi paraza kilo 45
Pumba za mahindi kilo 16
Mashudu ya alizeti kilo 14
Chokaa kilo 10
Soya kavu kilo 10
CFP ya kuku wanaotaga kilo 5
Jumla kilo 100
Hapa pia Kuna formula nyingine yenye pumba nyingi
Kuanzia siku 25 na kuendelea unaweza kutumia uduvi au dagaa k**a mbadala wa soya kavu kwa vifaranga tumia soya kavu pekee
Bei za CFP hapa Dodoma
1.Starter/vifaranga [kuanzia siku 1 na kuendelea]
Kilo 5 ni 17,000
Kilo 25 ni 75,000
2.Grower/kuku wanaokua [Kuanzia siku 25 na kuendelea]
Kilo 5 ni 14,000
Kilo 25 ni 60,000
3.Kuku wanaotaga[Baada ya kuona yai]
Kilo 5 ni 14,000
Kilo 25 ni 60,000
𝐊𝐢𝐥𝐨 𝟓 𝐢𝐧𝐚𝐭𝐨𝐬𝐡𝐚 𝐤𝐮𝐜𝐡𝐚𝐧𝐠𝐚𝐧𝐲𝐚 𝐜𝐡𝐚𝐤𝐮𝐥𝐚 𝐤𝐢𝐥𝐨 𝟏𝟎𝟎
𝐊𝐢𝐥𝐨 𝟐𝟓 𝐢𝐧𝐚𝐭𝐨𝐬𝐡𝐚 𝐤𝐮𝐜𝐡𝐚𝐧𝐠𝐚𝐧𝐲𝐚 𝐜𝐡𝐚𝐤𝐮𝐥𝐚 𝐤𝐢𝐥𝐨 𝟓𝟎𝟎
Mawasiliano 0752 912132 au 0718 192 378 kuagiza CFP
19/04/2026
Tuwekane sawa kuhusu soya
Soya imegawanyika sehemu kuu mbili : soya kavu/soyabean meal na soya mafuta/full fat soya
Soya ya mafuta hii inakuwa na protini 36% na mafuta 18% uwepo wa mafuta mengi inaifanya iwe na energy nyingi kuliko soya kavu
Soya kavu inakuwa na protini 45% au zaidi na mafuta 0.5-2% kwahiyo soya kavu ina protini nyingi na energy yake Iko chini kuliko soya mafuta
Hapa tunatumia soya kavu kwasababu tunalenga kupata protini ya kutosha kwa ajili ya ukuaji wa kuku
𝐒𝐨𝐲𝐚 𝐤𝐢𝐥𝐨 𝟓𝟎 𝐧𝐢 𝟏𝟎𝟎,𝟎𝟎𝟎, 𝐤𝐢𝐥𝐨 𝟏 𝐧𝐢 𝟐𝟎𝟎𝟎 𝐰𝐚𝐬𝐢𝐥𝐢𝐚𝐧𝐚 𝐧𝐚𝐬𝐢 𝐤𝐰𝐚 𝐧𝐚𝐦𝐛𝐚 𝐡𝐢𝐢 𝟎𝟕𝟓𝟐𝟗𝟏𝟐𝟏𝟑𝟐 𝐚𝐮 𝟎𝟕𝟏𝟖 𝟏𝟗𝟐 𝟑𝟕𝟖
Kuna classifications nyingi za soya ila hii ya kuangalia kiwango cha protini ndio mgawanyo sahihi kwa mfugaji
Mgawanyo/classification nyingine ni zile zinazoangalia mchakato wa uandaji mfano
De oiled cake [Soya Doc] k**a huu mfuko kwenye picha na hii ndio inapatikana masoko mengi inakuwa na protini 42-46%
Dehulled soybean meal hii inakuwa na protini 47-48% mchakato wake unahusisha kukoboa soya kabla ya kui process
Disclaimer
Haya sio maelekezo ya kitaalamu kuhusu namna ya kuandaa soya tunashauri ununue soya iliyoandaliwa.
Kuagiza CFP au soya kavu tupigie 0752912132 au fika ofisini kwetu
Moshi Agrovet tunapatikana Dodoma, Majengo Sokoni pembeni ya CRDB MAJENGO
12/02/2026
𝗢𝗸𝗼𝗮 𝘇𝗮𝗶𝗱𝗶 𝘆𝗮 𝟮𝟬,𝟬𝟬𝟬 𝗸𝘄𝗮 𝗸𝘂𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗻𝘆𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗸𝘂𝗹𝗮 𝗰𝗵𝗮 𝘃𝗶𝗳𝗮𝗿𝗮𝗻𝗴𝗮
Kwa kawaida vifaranga wa chotara tulikuwa tunaanza kuwalisha chakula cha dukani kuanzia siku 1 mpaka 25 baada ya hapo tunaanza kuwachanganyia chakula kwa kutumia CFP ya kuku wanaokua
Sasa wafugaji wengi ambao wanatumia CFP wamekuwa wakihitaji CFP ya vifaranga ili wapunguze gharama
Ndio wapunguze gharama na hapa nitakupa ushuhuda huu
Tuliokoa 33,000 kwa kuchanganya chakula cha vifaranga na ukuaji wao uko vizuri sana, tulitumia hii formula 👇
Mahindi paraza kilo 52
Soya kavu kilo 32
Mashudu ya alizeti kilo 9
Mafuta/oil kilo 2
CFP ya vifaranga kilo 5
𝐉𝐮𝐦𝐥𝐚 𝐤𝐢𝐥𝐨 𝟏𝟎𝟎 𝐠𝐡𝐚𝐫𝐚𝐦𝐚 𝐲𝐚𝐤𝐞 𝐭𝐮𝐥𝐢𝐭𝐮𝐦𝐢𝐚 𝟏𝟒𝟔,𝟎𝟎𝟎, 𝐤𝐢𝐥𝐨 𝟏𝟎𝟎 𝐧𝐢 𝐬𝐚𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐦𝐢𝐟𝐮𝐤𝐨 𝟐 𝐲𝐚 𝐤𝐢𝐥𝐨 𝟓𝟎
Maana yake mfuko mmoja tumeupata kwa 73,000 wakati tungenunua tungetumia 89,500 kwa mfuko mmoja wa starter
Kwahiyo utaona tumesevu 16,500 kwa kila mfuko mmoja kwa kuchanganya chakula cha dukani vifaranga
Fanya hesabu ya gharama ya hii formula uone unaokoa sh ngapi hapo ulipo?
K**a kikwazo kwako ni bei ya soya kavu unaweza kuagiza tukakutumia mf Kuna mfugaji akaniambia alipo soya ni 2700 kilo moja wakati hapa Dodoma soya kavu kilo 50 ni 95,000 sawa na kilo moja sh 1900
Unaweza kuagiza soya kavu ukatumiwa, na huyu mfugaji hakuwa mbali sana ni wilaya fulani hapo Morogoro!
Mwingine yupo Arusha aliniambia soya kavu kilo moja ni 2500
Niliwahi kupigiwa simu na mama mmoja yupo Mbagala akasema ananunua soya kilo moja sh 3000!
Nataka kusemaje?
𝐊𝐮𝐭𝐞𝐧𝐠𝐞𝐧𝐞𝐳𝐚 𝐜𝐡𝐚𝐤𝐮𝐥𝐚 𝐁𝐨𝐫𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐠𝐡𝐚𝐫𝐚𝐦𝐚 𝐧𝐚𝐟𝐮𝐮 𝐢𝐧𝐚𝐡𝐢𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐦𝐚𝐚𝐧𝐝𝐚𝐥𝐢𝐳𝐢 𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐤𝐮𝐬𝐚𝐧𝐲𝐚 𝐦𝐚𝐡𝐢𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐲𝐨𝐭𝐞 𝐲𝐚𝐧𝐚𝐲𝐨𝐭𝐚𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐤𝐚𝐛𝐥𝐚 𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐜𝐡𝐚𝐧𝐠𝐚𝐧𝐲𝐚 𝐜𝐡𝐚𝐤𝐮𝐥𝐚 𝐡𝐚𝐬𝐚 𝐘𝐚𝐥𝐞 𝐚𝐦𝐛𝐚𝐲𝐨 𝐧𝐢 𝐚𝐝𝐢𝐦𝐮 𝐧𝐝𝐢𝐨 𝐲𝐚𝐧𝐮𝐧𝐮𝐥𝐢𝐰𝐞 𝐤𝐰𝐚𝐧𝐳𝐚.
Leo vifaranga wetu wamefikisha siku ya 21 🔥 🔥 🔥
Gharama ya chakula kilo 100 tulitumia : 𝟏𝟒𝟔,𝟎𝟎𝟎
Formula tunayotumia 👇🏽👇🏽
𝟭.𝗠𝗮𝗵𝗶𝗻𝗱𝗶 𝗽𝗮𝗿𝗮𝘇𝗮 𝗸𝗶𝗹𝗼 𝟱𝟮
𝟮.𝗦𝗼𝘆𝗮 𝗸𝗮𝘃𝘂 𝗸𝗶𝗹𝗼 𝟯𝟮
𝟯.𝗠𝗮𝘀𝗵𝘂𝗱𝘂 𝘆𝗮 𝗮𝗹𝗶𝘇𝗲𝘁𝗶 𝗸𝗶𝗹𝗼 𝟵
𝟰.𝗢𝗶𝗹/𝗠𝗮𝗳𝘂𝘁𝗮 𝗸𝗶𝗹𝗼 𝟮
𝟱.𝗖𝗙𝗣 𝘆𝗮 𝘃𝗶𝗳𝗮𝗿𝗮𝗻𝗴𝗮 𝗸𝗶𝗹𝗼 𝟱
𝗝𝘂𝗺𝗹𝗮 𝗸𝗶𝗹𝗼 𝟭𝟬𝟬
1.Ulaji wa chakula / Feed intake - Uko vizuri...mpaka leo siku 21 wameshakula kilo 94 sawa gram 959.2 kwa kila kifaranga
2.Uzito / Body weight gain - wanaongezeka vizuri, daily gain ni above average -
Wastani wao ni gram 720
Uzito wa juu gram 840
Kwa uzoefu wetu vifaranga wa chotara siku 21 wakiwa na uzito wa juu ni gram 540 tulipokuwa tunatumia chakula cha dukani
3.Matatizo ya miguu / Leg problems-Hakuna
4.Choo Cha kuku / faecal dropping- Normal/Kawaida - angalia maranda utaona choo choo kikoje
5.Cannibalism/ Kudonoana -Hakuna
𝐊𝐚𝐦𝐚 𝐮𝐥𝐢𝐩𝐨 𝐬𝐨𝐲𝐚 𝐡𝐚𝐢𝐩𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚𝐧𝐢 𝐤𝐢𝐫𝐚𝐡𝐢𝐬𝐢, 𝐮𝐬𝐢𝐨𝐠𝐨𝐩𝐞 𝐭𝐮𝐧𝐚𝐥𝐢𝐟𝐚𝐧𝐲𝐢𝐚 𝐤𝐚𝐳𝐢 𝐢𝐥𝐢 𝐭𝐮𝐡𝐚𝐤𝐢𝐤𝐢𝐬𝐡𝐞 𝐮𝐧𝐚𝐩𝐨𝐜𝐡𝐚𝐧𝐠𝐚𝐧𝐲𝐚 𝐜𝐡𝐚𝐤𝐮𝐥𝐚 𝐮𝐧𝐚𝐩𝐮𝐧𝐠𝐮𝐳𝐚 𝐠𝐡𝐚𝐫𝐚𝐦𝐚 𝐛𝐚𝐝𝐚𝐥𝐚 𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐡𝐚𝐧𝐠𝐚𝐢𝐤𝐚 𝐛𝐮𝐫𝐞
26/09/2025
Tupo wazi Jumatatu mpaka Jumamosi karibu tukuhudumie tunauza dawa, chanjo, vitamin na vifaa vya ufugaji wa kuku
Sasa tumekuletea suluhisho la kuandaa chakula cha kuku chotara kwa kutumia CFP 🔥
Tunapatikana Dodoma Majengo Sokoni karibu na CRDB MAJENGO tupigie 0659632332
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Address
Weyula
Dodoma
41201
Opening Hours
| Monday | 07:30 - 19:00 |
| Tuesday | 07:30 - 19:00 |
| Wednesday | 07:30 - 19:00 |
| Thursday | 07:30 - 19:00 |
| Friday | 07:30 - 19:00 |
| Saturday | 09:30 - 19:00 |