Ofisi ya Rais - Tamisemi

Ofisi ya Rais - Tamisemi

Share

Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI

Photos from Ofisi ya Rais - Tamisemi's post 29/05/2026

SERIKALI YASISITIZA MIFUMO YA KIDIJITALI KUSOMANA KUONGEZA UFANISI WA HUDUMA

OWM-TAMISEMI

Serikali imewataka Maafisa Tehama katika Sekretarieti za Mikoa nchini kuendelea kuimarisha matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuharakisha utekelezaji wa ajenda ya uchumi wa kidijitali nchini.

Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Nicholaus Mkapa, wakati akifunga kikao kazi cha Maafisa Tehama wa mikoa ya Tanzania Bara kilichofanyika Jijini Dodoma, ambapo amesisitiza umuhimu wa mifumo ya serikali kusomana na kubadilishana taarifa kwa usalama ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Amesema Serikali imeendelea kusimamia utekelezaji wa ajenda ya uchumi wa kidijitali kupitia uimarishaji wa miundombinu ya umma ya kidijitali (Digital Public Infrastructure), ikiwemo mifumo ya utambuzi wa wananchi, mifumo ya kubadilishana taarifa na huduma za malipo ya kidijitali zinazorahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali.

"Pamoja na mafanikio hayo bado tunao wajibu mkubwa wa kuhakikisha mifumo yetu inaongea, inabadilishana taarifa kwa usalama na huduma zote zinamfikia mwananchi kwa urahisi zaidi," amesema Bw. Mkapa.

Aidha, amewataka Maafisa Tehama kuhakikisha mifumo yote inayotumika katika halmashauri inaunganishwa na mifumo ya kitaifa, huku wakizingatia usalama wa taarifa za wananchi na utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2022 pamoja na miongozo yake.

Photos from Ofisi ya Rais - Tamisemi's post 21/05/2026

Tanzania yapanga miji kuepuka Msongamano

OWM-TAMISEMI

Serikali ya Tanzania imeeleza kuwa imejipanga kudhibiti ukuaji holela wa miji kwa kuelekeza nguvu kubwa katika upangaji wa maeneo ya pembezoni kabla hayajajaa makazi yasiyo rasmi.

Akizungumza katika Jukwaa la 13 la Miji Duniani (WUF13), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amesema kupanga miji mapema ni njia bora ya kuepuka gharama kubwa za kurekebisha miundombinu baadaye.

“Kuweka miundombinu baada ya maeneo kujengwa holela ni gharama kubwa zaidi kuliko kuyapanga mapema,” amesema Prof. Shemdoe.

Amesema miji ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Arusha inaendelea kukua kwa kasi, hivyo Serikali imeanza kutumia teknolojia ya GIS, katika upangaji wa viwanja na kutumia miongozo mipya ya maendeleo ya miji ili kuhakikisha ukuaji huo unakuwa endelevu.

Prof. Shemdoe pia ametaja miradi ya TACTIC na DMDP kuwa sehemu ya uwekezaji mkubwa wa Serikali katika barabara, masoko, mifumo ya maji ya mvua na miundombinu inayostahimili mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, amesema Serikali inaendelea kuwekeza katika masoko ya kisasa, vituo vya usindikaji mazao na maeneo ya kiuchumi ili kusogeza huduma na ajira karibu zaidi na wananchi pamoja na kupunguza msongamano Dar es Salaam.

Photos from Ofisi ya Rais - Tamisemi's post 21/05/2026

WAUGUZI VIONGOZI WATAKIWA KUIMARISHA MATUMIZI YA MIFUMO KATIKA UTOAJI HUDUMA

Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Prof. Tumaini Nagu, amewataka Wauguzi Viongozi nchini kuweka kipaumbele katika matumizi ya mifumo katika maeneo yote ya utoaji huduma za afya ili kurahisisha upangaji na ugawaji wa rasilimali pamoja na kuboresha huduma kwa wananchi.

Prof. Nagu ametoa kauli hiyo leo, Mei 20, wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa Wauguzi Viongozi unaofanyika katika ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma.

“Nimependa sana kaulimbiu yenu ya mwaka huu kwani inazungumzia masuala ya kidigitali, na maelekezo ya Serikali ni kutumia mifumo katika kutoa huduma. Hivyo hakikisheni kila huduma mnayotoa inaingia kwenye mfumo,” amesema Prof. Nagu.

Ameongeza kuwa katika zama hizi, kutotumia mifumo ya kidigitali ni kujichelewesha kiutendaji, kwani mifumo hiyo husaidia kurahisisha utoaji wa huduma na ukusanyaji wa taarifa muhimu zinazowezesha upangaji bora wa mipango na rasilimali.

15/05/2026

Kutana na Kikundi cha Vijana cha Zasmiba kutoka Halmashauri ya Jiji la Tanga, kilichoanzishwa mwaka 2018 kwa lengo la kuchakata taka za plastiki na kuzigeuza kuwa fursa ya ajira na maendeleo.

Kupitia mkopo wa asilimia 10 unaotolewa na Halmashauri kutoka mapato ya ndani, kikundi hiki kimefanikiwa kuongeza mtaji, kupanua shughuli za uzalishaji na kujikwamua kiuchumi.

Leo, Zasmiba kinaendesha kiwanda cha kuchakata plastiki na kutoa ajira kwa vijana 20 wanaofanya kazi k**a vibarua, hatua inayochangia kuongeza kipato na kuboresha maisha ya familia nyingi.

Msikilize Katibu wa Kikundi, Said Khalfan, akieleza namna mkopo huo ulivyobadilisha maisha yao na kuwawezesha kufikia mafanikio makubwa ya kiuchumi.


ya wananchi

Want your organization to be the top-listed Government Service in Dodoma?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


Goverment City, Mtumba. TAMISEMI Street
Dodoma