Dodoma YOUTH Development Organization -doyodo
Youth Led org. that's empower young people in health, education, leadership and economically #Youth_opportunities. #Youth_empowerment
08/01/2026
📌 DOYODO YASHIRIKI TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA NAIA–AHW
DOYODO Tanzania imeshiriki kikamilifu katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Ajenda ya Kitaifa ya Kuwekeza katika Afya na Maendeleo ya Vijana Balehe (NAIA–AHW) kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 hadi 2024/25, kilichoandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Kikao hiki muhimu kilifanyika tarehe 22–23 Desemba 2025, kikilenga kutathmini mafanikio, changamoto na masomo muhimu katika utekelezaji wa nguzo sita za NAIA–AHW, zikiwemo:
✔️ Kuzuia maambukizi ya VVU
✔️ Kutokomeza mimba za utotoni
✔️ Kupambana na ukatili wa kijinsia na dhidi ya watoto
✔️ Kuboresha hali ya lishe
✔️ Kuhakikisha wasichana na wavulana wanabaki shuleni
✔️ Kuwezesha vijana kupata ujuzi na fursa za kiuchumi
Ushiriki wa DOYODO unaonesha dhamira yetu ya kuendelea kuwa mdau hai katika juhudi za kitaifa za kuwezesha vijana, kuchangia ushahidi wa utekelezaji, na kusukuma mbele ajenda za maendeleo jumuishi na endelevu kwa vijana wa Tanzania.
📢 Pamoja tunajenga kizazi chenye afya, ujuzi na fursa!
07/12/2025
*25/11/2025*
Mkurugenzi Mtendaji wa DOYODO na Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya Vijana Tanzania (TYDF), Ndg. Rajabu Juma Suleiman, ameongoza kikao cha robo ya tatu cha mwaka cha Wadau wa Kamati Tendaji ya TYDF.
Kikao hiki kimefanyika kwenye ofisi za Plan International Tanzania, jijini Dar es Salaam, kikiwakutanisha wadau wa maendeleo ya vijana pamoja na wajumbe wa Kamati Tendaji ya TYDF kwa mwaka 2025/2026. Ajenda kuu ya kikao ilikuwa kujadili mpango na utekelezaji wa TYDF kwa mwaka 2026, pamoja na mikakati madhubuti ya kuhakikisha jukwaa linafikia na kugusa kundi kubwa zaidi la vijana nchini.
Kikao kimeendelea kutoa mwelekeo thabiti wa kuimarisha ushirikiano na mshik**ano miongoni mwa wadau, kwa lengo la kufanya TYDF kuwa jukwaa jumuishi, linalosikiliza sauti za vijana na kutekeleza mipango yenye tija. DOYODO inaendelea kuthibitisha nafasi yake katika kusukuma mbele ushiriki wa vijana kwenye maendeleo ya taifa kupitia majukwaa shirikishi na yenye matokeo chanya.
25/08/2025
*Taasisi ya Dodoma Youth Development Organization (DOYODO)* imetambuliwa na kutunukiwa *cheti cha heshima* kwa mchango wake thabiti katika kuinua ustawi wa jamii kupitia programu shirikishi za vijana, elimu ya uongozi, afya, uchumi na teknolojia.
Cheti hicho kilipokelewa na *Mkurugenzi Mtendaji wa DOYODO na Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya Vijana Tanzania (TYDF), Ndg. Rajabu Juma Suleiman*, na kukabidhiwa na *Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima*, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, *kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango*, wakati wa Kongamano la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs).
Heshima hii inaonesha uthibitisho wa dhamira ya DOYODO kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa kupitia sauti na nguvu kazi ya vijana.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the organization
Telephone
Website
Address
Dodoma
Opening Hours
| Monday | 08:00 - 16:00 |
| Tuesday | 08:00 - 16:00 |
| Wednesday | 08:00 - 16:00 |
| Thursday | 08:00 - 16:00 |
| Friday | 08:00 - 16:00 |