Chama Cha Mapinduzi

Chama Cha Mapinduzi

Share

Ukurasa rasmi wa Chama Cha Mapinduzi. Chama Tawala Tanzania

15/05/2026

MUSOMA IMEITIKA โœ…

15/05/2026

๐—–๐—–๐—  ๐—›๐—”๐—œ๐—๐—”๐—ช๐—”๐—›๐—œ ๐—ž๐—จ๐—ž๐—ข๐—ฆ๐—˜๐—” ๐—ก๐—” ๐— ๐—”๐—”๐— ๐—จ๐—ญ๐—œ ๐—ฌ๐—”๐—ž๐—˜ ๐—Ÿ๐—”๐—ญ๐—œ๐— ๐—” ๐—ฌ๐—”๐—›๐—˜๐—ฆ๐—›๐—œ๐— ๐—œ๐—ช๐—˜ - ๐—ž๐—˜๐—ก๐—”๐—ก๐—œ

๐˜ผ๐™จ๐™š๐™ข๐™– ๐™ข๐™–๐™–๐™ข๐™ช๐™ฏ๐™ž ๐™ฎ๐™– ๐˜พ๐˜พ๐™ˆ ๐™๐™ช๐™š๐™ฃ๐™™๐™–๐™ฃ๐™– ๐™ฃ๐™– ๐™ข๐™–๐™ฉ๐™–๐™ง๐™–๐™Ÿ๐™ž๐™ค ๐™ฎ๐™– ๐™’๐™–๐™ฉ๐™–๐™ฃ๐™ฏ๐™–๐™ฃ๐™ž๐™–.

๐˜ผ๐™จ๐™ž๐™จ๐™ž๐™ฉ๐™ž๐™ฏ๐™– ๐™๐™–๐™ ๐™ช๐™ฃ๐™– ๐™ข๐™ ๐™ช๐™—๐™ฌ๐™– ๐™ฏ๐™–๐™ž๐™™๐™ž ๐™ฎ๐™– ๐˜พ๐™๐™–๐™ข๐™–.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndug. ๐—ž๐—ฒ๐—ป๐—ฎ๐—ป๐—ถ ๐—ž๐—ถ๐—ต๐—ผ๐—ป๐—ด๐—ผ๐˜€๐—ถ amesema ๐—–๐—–๐—  itaendelea kuzingatia ubora wa wagombea wenye uzoefu wa kujenga hoja na kutoa majawabu kwa wananchi kulingana na matakwa na matarajio yao.

Mwenezi Kenani amesisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakijawahi kukosea katika maamuzi yake na nyakati zote kimekuwa kikifanya maamuzi yenye kuzingatia mahitaji ya Watanzania kwa ujumla pasipo kujali itikadi za vyama vyao.

Aidha, Mwenezi Kenani amesema maamuzi ya chama yanapaswa kuheshimiwa na kila mwanachama huku akieleza kuwa hakuna aliye mkubwa kuliko chama.

Mwenezi Kenani ameeleza hayo leo tarehe 14 Mei 2026 wakati alipotembelea Tawi la veta lililopo shina No.5 kata ya Veta Mjini Musoma Mkoani Mara.

Photos from Chama Cha Mapinduzi's post 14/05/2026

BILIONI 16 ZAIDHINISHWA KUTEKELEZA AWAMU NYINGINE YA UJENZI WA HOSPITALI YA MWL NYERERE MARA

MUSOMA: Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amesema zaidi ya Sh bilioni 16 zimeidhinishwa bungeni kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Amesema hatua hiyo ni dhamira ya serikali ya kuhakikisha hospitali hiyo inakamilika kwa manufaa ya wananchi wa Mkoa wa Mara pamoja na maeneo jirani yanayonufaika na huduma zake.

Kihongosi ameeleza hayo leo Mei 14,2026 alipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa hospitali hiyo iliyopo katika Kata ya Kwangwa, Wilaya ya Musoma ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku 5 Mkoani Mara.

Akizungumza hayo Kihongosi amesema ujenzi wa hospitali hiyo ulianza miaka mingi iliyopita lakini ulipata nguvu mpya baada ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan akiwa Makamu wa Rais wakati huo kufuatilia utekelezaji wake na baadaye kuendelea kutoa fedha zaidi alipokuwa Rais wa Tanzania.

โ€œKatika bajeti iliyopitishwa hivi karibuni, Bunge limeidhinisha zaidi ya shilingi bilioni 16 kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa mradi huo huku kazi zikitarajiwa kuanza rasmi mwezi Julai,โ€ amesema Kihongosi.
Kihongosi amewapongeza watumishi wa afya wa hospitali hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya licha ya mazingira yenye changamoto, akisema huduma za afya zinahitaji moyo wa kujitoa na uaminifu mkubwa.

โ€œTumezungumza na wagonjwa na watumishi, wengi wao ni vijana, kazi mnayoifanya si rahisi lakini Mungu awaongoze na awalinde,โ€amesema Kihongosi.

Pia akijibu kuhusu suala la upungufu wa watumishi katika hospitali hiyo alisema taarifa zinaonyesha kuna upungufu wa watumishi kwani waliopo hawaendani na idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa, jambo ambalo amesema atalifikisha kwa Waziri mwenye dhamana ili lipewe kipaumbele.

Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo,Dk Osimund Dyegura amesema tangu mwaka 2021 zaidi ya Sh bilioni 32 zimetumika katika ujenzi wa majengo, ununuzi wa vifaa tiba na magari ya wagonjwa.

Want your organization to be the top-listed Government Service in Dodoma?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Address


Dodoma
0000