Mwl Elisha Mathayo
Teaching Word of God
06/01/2026
KUMFUATA KRISTO KATIKA UTUMISHI
Bwana Yesu asifiwe watumishi wa Mungu mnaendeleaje? Heri ya mwaka mpya 2026
Leo natamani tushirikishane Neno moja muhimu sana linalohusu utumishi wetu kwa Mungu (Kumtumia Mungu)
Neno la kusimamia ni kutoka katika injili ya Yohana 12:26
[26]Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
If any man serve me, let him follow me; and where I am, there shall also my servant be: if any man serve me, him will my Father honour.
Katika mstari huo Yesu anafundisha kitu muhimu sana kinachohusu utumishi wetu kwake kwanza anasema
akinitumikia na anifuate ... Hapa tunaelewa kwamba kumtumikia Mungu ni kumfuata Yeye kumfuata Kuna maana mbili
a) Maana ya kwanza ni Kumwamini awe Bwana na Mwokozi wa maisha Yako (Kuwa mfuasi wake)
b) Maana ya pili Ni kufuata maelekezo yake yaani kumsikiliza ....
Hapa tunajifunza kwanza mtu yeyote atakayesema anamtumikia Mungu lazima kwanza awe mfuasi wa Yesu yaani lazima Yesu awe Bwana na Mwokozi wake kikwelikweli lakini pia tunaona kuwa hakuna namna tunaweza kumtumikia Mungu k**a Hatufuati maelekezo yake hatufuati anachosema
1 Wakorintho 11:1
[1]Mnifuate mimi k**a mimi ninavyomfuata Kristo.
Be ye followers of me, even as I also am of Christ.
Mojawapo ya sababu ya Mtume Paul kufanikiwa katika huduma yake ni aliamua kumfuata Kristo( Kumsikiliza na kumwamini Kristo) ... HAKUNA KUFANIKIWA KWENYE HUDUMA BILA KUMFUATA KRISTO
KWA NINI NI LAZIMA/ MUHIMU KUMFUATA KRISTO KATIKA UTUMISHI?
1: Kazi sio yetu ni yake..Hii inatufanya tumfuate kwa kila kitu kwa sababu sisi sio wenye malengo na sisi sio wenye maono na kazi hiyo na kimsingi hata faida sio Yetu ni yake kwa hiyo k**a tunataka kumtumikia Mungu lazima tumsikilize kwa kila kitu
2;Yeye ndiye anaejua namna ya kuifanya kazi na ikaleta matokeo anayoyataka Yeye ....Ukweli ni kwamba Sisi tunaweza tukawa tunahisi tu au tuna uzoefu tu kwa namna ya kawaida ila kimsingi Mungu ndiye anaejua namna kazi inavyofanyika kila hatua ili ilete matokeo kwa hiyo lazima tumfuate na kumsikiliza yeye tu
3:Yeye ndiye atakayetulipa baada ya kazi..... Ukisoma huo mstari pale mbele unasema mtu akinitumikia baba atamuheshimu... Kwa lugha nyepesi Mungu atamlipa sasa Mungu hawezi kutulipa k**a tulifanya kwa mawazo na fikra zetu tu lazima tufanye k**a anavyotaka yeye ndipo atakapotulipa sawasawa na kazi yetu....
FAIDA ZA KUMFUATA KRISTO KATIKA UTUMISHI
1:Ukimfuata Kristo utafanya kazi ambayo
Mungu anataka ifanyike
2:Utafanyia kazi mahali ambapo Mungu
anafanyia
3: Utafanya kazi ya Mungu kwa wakati
ambao Mungu anataka ufanye (wakati
uliokubalika
Ndugu zangu, watumishi wenzangu ukitaka kazi yoyote au huduma yoyote unayoifanya ifanikiwe msikilize Mungu na mfuate Mungu Fuata anachosema hata k**a ni kigumu fanya tu hata k**a haujaelewa wewe fanya tu hata k**a unahisi tofauti wewe fanya kile Mungu amesema ... Utamuona Mungu kwa namna ya ajabu sana...
Nakutakia mwaka mwema uliojaa utumishi kwa uaminifu mkubwa mbele za Mungu Na Neema ya Mungu wetu mwema ikuhifadhi na kukutunza kwa jina l a Yesu ..
Ndimi rafiki yako
Mwl Elisha Mathayo
0713133123
Shetani ni adui lazima apingwe kwa jina la Yesu
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Iringa
Iringa
25/02/2024
22/04/2023