Shamba Fm Radio
Official Page of Shamba Fm Radio. Sikiliza Live Online www.shambafm.co.tz
13/06/2026
MAFUNZO, VIFAA VYATOLEWA KUPIMA AFYA MTO LUKOSI - KILOLO
Kamati za Mazingira na Maliasili za Vijiji vya Mtandika na Lulindi Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, vimepatiwa vifaa pamoja na mafunzo ya vitendo ya kupima afya ya Mto Lukosi ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha usimamizi wa mazingira na uhifadhi wa vyanzo vya maji katika jamii.
Mafunzo hayo yametolewa na Bodi ya Maji ya Bonde la Rufiji (RBWB) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira (IUCN), yakilenga kuwajengea uwezo wanakamati katika kufuatilia ubora wa maji kwa kutumia viumbe hai na wadudu viashiria wanaopatikana kwenye mito.
Akizungumza baada ya mafunzo hayo, mmoja wa viongozi wa Kijiji amepongeza ushirikiano kati ya RBWB na IUCN kwa kuendelea kuzijengea uwezo jamii za maeneo ya vyanzo vya maji ili kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira.
Kwa upande wake Afisa Mazingira wa RBWB, Nelson Orotu, amesema mafunzo hayo yataisaidia jamii ya Mtandika kuwa na uelewa wa kisayansi katika kutathmini afya ya mto na kuchukua hatua stahiki za kulinda rasilimali za maji.
Wanakamati wa mazingira wameahidi kutumia elimu na vifaa walivyopokea kufuatilia afya ya Mto Lukosi na kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za uhifadhi wa mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
11/06/2026
SITHOLE MCHEZAJI WA KWANZA KUPATA KADI NYEKUNDU WC 2026
Yaya Sithole mchezaji wa timu wa taifa ya Afrika ya kusini amekuwa mchezaji wa kwanza kwenye mashindano ya kombe la dunia 2026 kupata kadi nyekundu.
Mchezaji huyo amepata kadi nyekundi kwenye mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Mexico ikiwa ni mechi ya ufunguzi wa kombe hilo mara baada ya kumfanyia faulo Rauli Jimenezi.
Mechi hiyo inapigwa kwenye dimba la Mexico city nchini mexico ikiwa ni mechi ya ufunguzi wa kombe la Dunia 2026 ambalo Marekani, Canada na Mexico ndio wenyeji wa mashindano.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Utalii Road
Iringa